Kwa wale wenye magari na ambao hampandi daladala, hivi ndo vioja tunavyopata kwenye daladala wenzenu tusio na magari!

lossoJR

JF-Expert Member
Oct 11, 2012
2,711
2,382
Huku mambo ni moto,sijui ndio kuvurugwa na maisha...

Mlokole: "Nyimbo gani mnapiga?!? Wekeni nyimbo za Yesu.."
Konda: "Vipi wewe, Yesu bado hajatoa album...

Abiria: "Kuna Kiti au unasema panda tu!?"
Konda: "hao wengine wamekalia ndoo?! "

Abiria: "Embu punguzeni sauti ya redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu zinatushinda, tusikilize na zako!? hebu tupunguzie misheria"

Mmama: "Bwana ondoa gari joto sana!!",
Konda: "Usituzingue wewe, shuka upande fridge...."

Konda: "Anti, kuna siti pale nyuma, ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe, Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"

Sister duu: "Konda unanibana bwana..."
Konda: "mbona nguo ulizovaa huzisemi, kama ulitaka kujiachia ungekodi treni peke yako!!!"

Sharobaro: "Kuna kiti?! Kama hamna sipandi..."
Konda: "Kama unaogopa kukosa kiti si ungebeba cha kwako!!?"
 
Mleta mada umesahau kutuwekea picha

upload_2018-2-4_15-31-27.png
upload_2018-2-4_15-32-15.png
upload_2018-2-4_15-33-27.png
 
Baada ya ajira yangu ya pili nilianza kutumia gari yangu binafsi kwenda kazini na kurudi. Mwanzoni nikawa nainjoi kusikiliza mziki au radio nnayo taka kwenye gari au kupita njia za mkato kuwahi kazini au nyumbani.

Baadae nikaanza kuhusu kuna kitu nakosa nikawa nipo tuu. Nakumbuka nilipata shida ya macho nikapumzika kuendesha gari ikabidi niwe naenda kazini na usafiri wa umma. Yaani ile msongamano na watu kelele huyu nipishe huyu umenikanyaga mara nishikie mwanangu au nishikie mzigo wangu wamama wengine analazimisha kupanda gari iliyojaa na mwanae mgongoni akitegemea watu watampisha siti au mzee mtu mzima anapanda basi limejaa watu hawa hawa mpishi. Utamsikia kinda, oyaa nyie abiria hamna wazazi au? Inamaana hamuoni babu yenu ananing'inia mlangoni?
 
Na wenye magari ambao hawapandi daladala waje na mambo wanayo kutana nayo wanapo endesha magari yao
 
Nakumbukabsiki moja nilikuwa natoka Manzese naelekea Posta,gari lilipofika Akiba (DIT) lilisimama kwaajili ya kushusha na kupakia abiria,hapo kuna mdada alimuuliza Konda "kuna siti ya kukaa?" Haaaaaaa,makondakta ni wajeur sana alijibiwa "kwani hili gari limekuwa mtumbwi mpaka ukose siti"
 
Ukitaka ku injoi raha ya daladala,,panda daladala za usiku kuanzia saa 3 kwenda mbele mida ambayo unaeza kuta konda na abiria wake washapata 1 barid 1 motoo
 
Kuna mzee aligombania kuingia ndani ya Daladala la Gombo la mboto sasa kuna Dogo nikuwa nimekaa naye siti moja,kumuona mzee Dogo akamwita mzee aje akae.Dah,jibu lake watu hatuna mbavu"mzee kasema kijana Mimi siwahi siti nawahi usafiri"
 
Yaani ile msongamano na watu kelele huyu nipishe huyu umenikanyaga mara nishikie mwanangu au nishikie mzigo wangu wamama wengine analazimisha kupanda gari iliyojaa na mwanae mgongoni...

Mithili ya watoto wa daras la chekechea wanaoanza shule
 
Huku mambo ni moto,sijui ndio kuvurugwa na maisha...

Mlokole: "Nyimbo gani mnapiga?!? Wekeni nyimbo za Yesu.."
Konda: "Vipi wewe, Yesu bado hajatoa album...

Abiria: "Kuna Kiti au unasema panda tu!?"
Konda: "hao wengine wamekalia ndoo?! "

Abiria: "Embu punguzeni sauti ya redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu zinatushinda, tusikilize na zako!? hebu tupunguzie misheria"

Mmama: "Bwana ondoa gari joto sana!!",
Konda: "Usituzingue wewe, shuka upande fridge...."

Konda: "Anti, kuna siti pale nyuma, ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwenda zako wewe, Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"

Sister duu: "Konda unanibana bwana..."
Konda: "mbona nguo ulizovaa huzisemi, kama ulitaka kujiachia ungekodi treni peke yako!!!"

Sharobaro: "Kuna kiti?! Kama hamna sipandi..."
Konda: "Kama unaogopa kukosa kiti si ungebeba cha kwako!!?"
Yaani wewe jamaa ni hatari sana.
 
Ukitaka ku injoi raha ya daladala,,panda daladala za usiku kuanzia saa 3 kwenda mbele mida ambayo unaeza kuta konda na abiria wake washapata 1 barid 1 motoo
Aisee umenena mkuu hapo utaemjoy sana.
 
Na wenye magari ambao hawapandi daladala waje na mambo wanayo kutana nayo wanapo endesha magari yao
Hawana jipya mkuu zaidi ya kuibiwa pochi zao madirishani na kupigwa side mirrors
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom