Kwa wale watoto wa wafugaji mlitokaje huko maana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wale watoto wa wafugaji mlitokaje huko maana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mbasamwoga, Sep 28, 2011.

 1. m

  mbasamwoga Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  leo nimekumbuka sana maisha niliyopitia wakati wa utoto na ujana wangu, nimetokea kwenye familia ya wakulima na wafugaji, ama kweli yale ndiyo yalikuwa maisha halisi ya mwafrika. Nilichunga ng'ombe nusra nisisome shule, kila asbh tulikuwa tunaenda kuchunga/ kulisha kundi la ng'ombe wapatao 200 na mbuzi wengi na kondoo wengi. Kule porini tulipokuwa tukichunga tulifanya vittuko vingi sana,
  tulikuwa tunapiganisha madume ya ng'ombe kama leo ninavyoona mieleka! Pia kila watu walishangilia dume la kundi lao, hii wakati mwingine ilileta ugomvi.
  Tuliwatumia ngombe kama farasi kuvuka sehemu zenye tope au mito.
  Tulikuwa tukinywa maji machafu ambayo hii leo hata kuyagusa naogopa.
  Tulikuwa tunaficha vyakula kama ndizi miwa na maziwa huko polini ili viliwe kesho yake.
  Kuoga ilikuwa ndoto hasa kutokana na kukanyaga majini mda mwingi.
  wazee hawakupenda utoe ajenda za kwenda shule unaweza kupewa adhabu ya kuchunga mfululizo
  chakula cha usiku kilikuwa kikiliwa saa 5 usiku ili angalau kuchelewesha mda wa kulala ili kuimarisha ilinzi wa mifugo.
  Wazee walioa kwa mahari kubwa mpaka ng'ombe 80.
  Ng'ombe hauzwi mpaka shida ifike shingoni
  aliyebahatika kwenda shule ni yule tu aliyeweza kujua kusoma kabla ya kuanza shule...... Hii ndo ilinitoa maana nilikuwa najichanganya na wale wanaosoma huku wanachunga weekend hatimaye mzee nikajua baadhi ya maneno na nikajua kuhesabu mpaka mia kuandika baba, mama n.k
  yaani we acha tu..... Ndo mpaka leo tuko tuna excell mzeeee wewe je!!! Ongezeeni

  daaah...... Leo sijui na mimi ningekuwa nagombana vita ya wafugaji na wakulima... God is great
   
Loading...