Ukweli1
JF-Expert Member
- Nov 19, 2013
- 550
- 333
Ninaongelea mahusiano ya muda mrefu yanayoweza fikia ndoa mahusiano mengine hapana.
Nimeandika maana mara nyingi wako (kwa kusoma post zao) watu wenye uhitaji kiukweli lakini unaona kabisa jamii imewasoma tofauti ila ni kutokana na wao walivyojiwakilisha.
Mambo ya kuzingatia unapokuwa unataka kupata mwenza kwa mtandao:-
Tumefika wakati ambao mambo mengi yanafanyika kwa internet.
Wako wanaopinga na wako sawa kabisa maana hata simu ya mkononi zilivyoingia zilipingwa sana kuhusu rays usiweke sijui wapi, sikilizia sikio sijui lipi wajanja wakawatengenezea stickers za kupunguza rays "Anti-Radiation Cell Phone Sticker" na watu wakanunua sasa tumeshasahau. Iko siku hili nalo litapita na kusahulika. "It is Just a Matter of Time" .
Chukua tahadhari:

- Username yako na picha yako inatoa taarifa kama uko serious au hapana. Chagua kwa makini.
- Weka umri wako na umri unaotarajiwa mwenza wako awe nao. Unaweza kutumia range kwa mfano umri wangu ni kati ya 30 na 47.
- Sema wasifa wako kwa kifupi na yale unayoyatarajia toka kwa mwenzio.
- Weka email address (tengeneza ya muda) maana sio kila mtu ana two usernames au atataka kukupm tumeshaona huku watu wakipeana mipasho sababu ya yalioyotokea kwa pm.
- Epuka kujibu kila swali, kumbuka sio sio kila swali unaulizwa ni swali mengine ni unategwa tu, ukijibu kila kitu kuna mahali utakosea au utakwazika na kuandika vibaya na kuharibu ujumbe wako.
- Usiwe desperate na mwenye haraka. "It is a characteristic of wisdom not to do desperate things" Henry David Thoreau.
- Kumbuka unavutia kile unachowakilisha kama unadanganya usishangae waongo tu wakawasiliana na wewe "You Attract What You Portray".
- Hahuhitaji kuelezea past relationships, kama kuna ulazima fupisha. Kuelezea sana yaliopita inafanya mtu serious kusita anajua mkishindwana ataanikwa na yeye.
- Usiwe mtu ambaye chochote kile twende mfano "dini yeyote", hii inaonyesha uko desperate au unatafuta mahusiano ya muda mfupi.
- Usiambatanishe namba ya simu au picha yako.
- Elezea usiyoyataka bila kumkwaza mtu kwa mfano: waliopata talaka, wajane na wenye watoto hizo ni sensitive issues ziepuke na kama utataka kusema basi tumia polite language. Ukikosea hapa comments utakazopata zinaweza haribu ujumbe wako wote.
- Pambanua na tofautisha ujumbe wa public na private mengine yaache kwa watakao wasiliana na wewe private (potential spouses).
Tumefika wakati ambao mambo mengi yanafanyika kwa internet.
Wako wanaopinga na wako sawa kabisa maana hata simu ya mkononi zilivyoingia zilipingwa sana kuhusu rays usiweke sijui wapi, sikilizia sikio sijui lipi wajanja wakawatengenezea stickers za kupunguza rays "Anti-Radiation Cell Phone Sticker" na watu wakanunua sasa tumeshasahau. Iko siku hili nalo litapita na kusahulika. "It is Just a Matter of Time" .
Chukua tahadhari:
- Internet ina victims and victors so handle it with care. Kuna wengi wameumizwa na kuna wengi wamefanikiwa.
- Internet inaweza badilisha mtazamo wako wa vitu kuwa mzuri au mbaya. Unaweza usijue ila wengi tukijichunguza kuna baadhi ya tabia mpya, kama jinsi ya kufikiri, jinsi ya kuandika, maneno fulani, tulikuwa hatuna kabla hatujaanza kutumia internet, na kuna baadhi ya tabia tumepoteza baada ya kuanza kutumia internet.
"The Law of Attraction states that whatever you focus on, think about, read about, and talk about intensely, you are going to attract more of into your life."
Nawatakia mafanikio mema
Kokote aliko huyo spouse wako mtakutana tu iwe kwa mguu, kwa gari, kwa mtandao au kwa kuunganishiwa, vyovyote vile, cha msingi be patient with yourself, be positive, omba muongozo kutoka kwa Mungu wako.