Kwa wakatoliki tafadhali...

Kwa wakatoliki tafadhali...

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,493
Reaction score
12,453
Mapendo...jamani naombeni ufafanuzi wa hii sala baada ya komunio kipengele cha "KUOMBA" kinasema hivi......"Yesu mwema uko moyoni mwangu sasa,huwezi kuninyima kitu.Basi sitaki mali,wala heshima,wala furahaNakuomba kitu kimoja unipe neema zako nisitende dhambi tena,nikuche, nikupende."

hapo kwenye nyekundu ndipo panaponipa wakati mgumu wa kutafakari naombeni ufafanuzi wadau.....

jumapili njema.
 
Nitaweka pingamizi mahakamani hicho kipengere kisijadiliwe mpaka biblia ifanyiwe mapitio na kusahihishwa
 
Hizo ndio ibada za watu walizozitunga kuwapoteza vipofu wenzao, FREEMASON wanahusika hapo
 
Mapendo...jamani naombeni ufafanuzi wa hii sala baada ya komunio kipengele cha "KUOMBA" kinasema hivi......"Yesu mwema uko moyoni mwangu sasa,huwezi kuninyima kitu.Basi sitaki mali,wala heshima,wala furahaNakuomba kitu kimoja unipe neema zako nisitende dhambi tena,nikuche, nikupende."

hapo kwenye nyekundu ndipo panaponipa wakati mgumu wa kutafakari naombeni ufafanuzi wadau.....

jumapili njema.

Maandiko yanasema tafuteni kwanza ufalme wa Mungu. Hapo unaomba neema tu toka kwa Mungu, Na mengine yote utaongezewa kama maandiko yasemavyo.
Tatizo kwetu Wakatoliki ni kuwa Sala zetu zimeshatungwa, tena hadi sehemu ya maombi unaambiwa ..(taja), ndio maana yote haya yanakuja.
Nadhani kikubwa kujua pia hapo, nini nini maana ya Neema ambayo Mtu anaiomba:-

Nukuu:

(2). MAANA YA NEEMA.
Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,"Neema, neema imefunuliwa" na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya neema?

  1. Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au sifa aliyonayo mtu.
  2. Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote.
  3. 1. Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7). Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu alitaka pia kufuta kabisa kizazi cha Wausraeli na kubaki na Musa tu kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (YOHANA8:29).Alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (WAEBRANIA 4:14-15). Yesu huyu anayempendeza Mungu ndiye aliyekufa msalabani na Baraba aliyekuwa mhalifu mkubwa akafunguliwa. Kama Baraba alivyofunguliwa pamoja na ukosaji wake, kila mwanadamu amefunguliwa, akiamini tu. Mbele za Mungu kila mtu amepimwa na kuonekana amepungua (DANIELI 5:27). Sasa kwa kuamini tu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu pale msalabani, sisi tunaokolewa. Watu wengi hawaokolewi kwa sababu hawajui tunaokolewa kwa neema tu kwa njia ya imani peke yake (WAEFESO 2:5). Kazi aliyoifanya Yesu msalabani imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda bila sisi kuifanya. Ni kama ambavyo bondia anavyopigana ulingoni kwa shida kubwa na kasha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha, mke wake aliyebaki nyumbani bila kupigana naye atakuwa milionea. Hii ndiyo neema.
  4. 2. Uwezo wa kushinda bila kutumia nguvu zetu- Neema ni uwezo wa kushinda dhambi na kumtumikia Mungu apendavyo. Neema ndiyo inayotufundisha (inayotuwezesha) kukataa ubaya na tama za kidunia na kuishi kwa kiasi na haki na utakatifu (TITO 2:11-12; WAGALATIA 2:8). Maisha ya wokovu siyo ya kutumia nguvu zetu au kujitahidi. Uweza wa Mungu unatimilika kwetu katika udhaifu wetu yaani kutokuweza kwetu. Hatupaswi kujitumainia wenyewe katika kufanya lolote (2 WAKORINTHO 1:8-9).

Kwa Mtazamo wangu Mkuu.
 
Hizo ni sala zilizotungwa kwa hekima ya mwanadamu na bible inasema HEKIMA YA MWANADAMU NI UPUMBAVU MBELE ZA MUNGU sala aliyoigiza Mungu ni hii BABA YETU ULIE MBINGUNI,JINA LAKO LITUKUZWE,UFALME WAKO UJE,MAPENZI YAKO YATIMIZWE,HAPA DUNIANI KAMA HUKO MBINGUNI,MALIZIA NA WEWE ULI UELEWE BANA NA UACHE KUKARIRI LITRUJIA YA MWANADAMU.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Mapendo...jamani naombeni ufafanuzi wa hii sala baada ya komunio kipengele cha "KUOMBA" kinasema hivi......"Yesu mwema uko moyoni mwangu sasa,huwezi kuninyima kitu.Basi sitaki mali,wala heshima,wala furahaNakuomba kitu kimoja unipe neema zako nisitende dhambi tena,nikuche, nikupende."

hapo kwenye nyekundu ndipo panaponipa wakati mgumu wa kutafakari naombeni ufafanuzi wadau.....

jumapili njema.
Kanisa langu linakuahidi mali, heshima na furaha...! Kazi kwako!
 
Ndio shida ya kukariri neno moja tu na kuacha kujifunza muktadha wa sala/habari nzima. Maana ya sala hiyo ni kwamba siku zote tuombe neema ya Mungu na vitu/mahitaji vitakuja tu kutokana na neema za Mungu. Nabii Suleiman alipoambiwa na Mungu kwamba aombe chochote na atapewa,yeye aliomba HEKIMA tu. Hakuomba msululu wa mahitaji ya kidunia. Lakini vitabu vitakatifu vinasema alikuja jaaliwa hekima pamoja na utajiri mkubwa!. Bado naona hiyo sala haijakosewa,tuombe neema na mengine yote tutapewa kwa ziada!
 
Mapendo...jamani naombeni ufafanuzi wa hii sala baada ya komunio kipengele cha "KUOMBA" kinasema hivi......"Yesu mwema uko moyoni mwangu sasa,huwezi kuninyima kitu.Basi sitaki mali,wala heshima,wala furahaNakuomba kitu kimoja unipe neema zako nisitende dhambi tena,nikuche, nikupende."

hapo kwenye nyekundu ndipo panaponipa wakati mgumu wa kutafakari naombeni ufafanuzi wadau.....

jumapili njema.

Ukisoma maneno baada ya ayo mekundu ndo utaelewa......kwamba hatumwombi mali,heshima wala furaha,lakini kikubwa ni neema zake zituongoze tusifanye dhambi ambazo ztatutenganisha na yeye ambaye ndiye muumba wetu
 
Mapendo...jamani naombeni ufafanuzi wa hii sala baada ya komunio kipengele cha "KUOMBA" kinasema hivi......"Yesu mwema uko moyoni mwangu sasa,huwezi kuninyima kitu.Basi sitaki mali,wala heshima,wala furahaNakuomba kitu kimoja unipe neema zako nisitende dhambi tena,nikuche, nikupende."

hapo kwenye nyekundu ndipo panaponipa wakati mgumu wa kutafakari naombeni ufafanuzi wadau.....

jumapili njema.

...Nina kushauri ukahudhurie mufundisho ya Kanisa Katoliki; "soma KATEKISIMU YOTE YA KANISA KATOLIKI" ukishafuzu' rudi hapa jamvini ukawafundishe ambao siyo Wakatoliki kama wewe...!
"Tumsifu Yesu Kristu..."
 
sio lazima kuongea vitu vya kukaririshwa, unaweza kutumia maneno tofauti na hayo.
 
Hizo ni sala zilizotungwa kwa hekima ya mwanadamu na bible inasema HEKIMA YA MWANADAMU NI UPUMBAVU MBELE ZA MUNGU sala aliyoigiza Mungu ni hii BABA YETU ULIE MBINGUNI,JINA LAKO LITUKUZWE,UFALME WAKO UJE,MAPENZI YAKO YATIMIZWE,HAPA DUNIANI KAMA HUKO MBINGUNI,MALIZIA NA WEWE ULI UELEWE BANA NA UACHE KUKARIRI LITRUJIA YA MWANADAMU.
...ndugu yangu wewe umeharibu kabisa!
Sisi Wakatoliki tunase hivi "Ufalme wako ufike..."

...tena kwa taarifa yako: "Sala zote za Kanisa Katoliki zinatoka kwenye Biblia"
...sijui ni sala zipi unazosema wewe!
 
Ha ha ha ha ha haaaaaaaaa. When you join JF, you won't get bored or stressed.
 
...ndugu yangu wewe umeharibu kabisa!
Sisi Wakatoliki tunase hivi "Ufalme wako ufike..."

...tena kwa taarifa yako: "Sala zote za Kanisa Katoliki zinatoka kwenye Biblia"
...sijui ni sala zipi unazosema wewe!

mh, kweli mkuu!
 
Maandiko yanasema tafuteni kwanza ufalme wa Mungu. Hapo unaomba neema tu toka kwa Mungu, Na mengine yote utaongezewa kama maandiko yasemavyo.
Tatizo kwetu Wakatoliki ni kuwa Sala zetu zimeshatungwa, tena hadi sehemu ya maombi unaambiwa ..(taja), ndio maana yote haya yanakuja.
Nadhani kikubwa kujua pia hapo, nini nini maana ya Neema ambayo Mtu anaiomba:-

Nukuu:

(2). MAANA YA NEEMA.
Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,¡±Neema, neema imefunuliwa¡± na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya neema?

  1. Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au sifa aliyonayo mtu.
  2. Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote.
  3. 1. Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7). Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu alitaka pia kufuta kabisa kizazi cha Wausraeli na kubaki na Musa tu kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (YOHANA8:29).Alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (WAEBRANIA 4:14-15). Yesu huyu anayempendeza Mungu ndiye aliyekufa msalabani na Baraba aliyekuwa mhalifu mkubwa akafunguliwa. Kama Baraba alivyofunguliwa pamoja na ukosaji wake, kila mwanadamu amefunguliwa, akiamini tu. Mbele za Mungu kila mtu amepimwa na kuonekana amepungua (DANIELI 5:27). Sasa kwa kuamini tu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu pale msalabani, sisi tunaokolewa. Watu wengi hawaokolewi kwa sababu hawajui tunaokolewa kwa neema tu kwa njia ya imani peke yake (WAEFESO 2:5). Kazi aliyoifanya Yesu msalabani imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda bila sisi kuifanya. Ni kama ambavyo bondia anavyopigana ulingoni kwa shida kubwa na kasha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha, mke wake aliyebaki nyumbani bila kupigana naye atakuwa milionea. Hii ndiyo neema.
  4. 2. Uwezo wa kushinda bila kutumia nguvu zetu- Neema ni uwezo wa kushinda dhambi na kumtumikia Mungu apendavyo. Neema ndiyo inayotufundisha (inayotuwezesha) kukataa ubaya na tama za kidunia na kuishi kwa kiasi na haki na utakatifu (TITO 2:11-12; WAGALATIA 2:8). Maisha ya wokovu siyo ya kutumia nguvu zetu au kujitahidi. Uweza wa Mungu unatimilika kwetu katika udhaifu wetu yaani kutokuweza kwetu. Hatupaswi kujitumainia wenyewe katika kufanya lolote (2 WAKORINTHO 1:8-9).

Kwa Mtazamo wangu Mkuu.
...kwenye "blue"

Tatizo kwetu Wakatoliki ni kuwa Sala zetu zimeshatungwa, tena hadi sehemu ya maombi unaambiwa ..(taja)

"inaoneka wewe umerithishwa! wala siyo Mkatoliki halisi..."

"yawezekana wakati unajifunza mafundisho ya Komunyo na Kipaimara' ulikuwa unawaza lini mafundisho yataisha ili ufanyiwe sherehe! Ndiyo maana huku yashika mafundisho ya KATEKISIMU"

...kanunue kitabu cha KATEKISIMU uanze mafundisho upya!

"kuhusu maombi katika Ibada ya Misa yameandaliwa kutoka na LITURJIA ya siku husika, kuanzia Mwanzo wa Ibada, Liturjia (liturujia) ya Neno, Liturjia ya Ekaristi, Ibada ya Komunyo na Ibada ya Kumalizia..., vyote vinatoka kwenye mwambata wa Biblia Takatifu...!"

*jitahidi kuwa unabeba vikuza Imani, hasa kuendana na KALENDA YA LITURUJIA ya Kanisa Katoliki...!
 
Tatizo mleta mada hata ukristo haumuhusu,walewale,hapo unapotaka ufafanuzi panaeleweka sana,tumia akili utajua inamaanisha nini
 
Back
Top Bottom