kwa wakaka wa kitanzania tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa wakaka wa kitanzania tu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Smile, Apr 5, 2012.

 1. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Unakuta kijana kaanza kazi
  Miezi michache tuanachukua mkopo wa gari hapo anaishi nyumba ya kupanga
  20% ya mshahara nyumba ya kupanga maana hawezi kuishi uswahilini
  50% marejesho yamkopo wa gari
  10% mafuta yagari,matengenezo ,trafiki na kadhalika
  Hapo badopamba,kunywa miller maana eti hawanywi bia za Tanzania kisa huku maji machafu wanakunywavitu vya nje ,bado kuhonga kina smile
  Hapo tarehe kumi ikifika anaanza kutuma vi outlook hey bidada naomba unikopeshe elfu hamsinimdogo waku karudishwa shule… khaa mimi nimkopeshe mwanaume kwa misingi gani? Sina muda wa kufedheheshana kwa kudaiana na watu mastupid kwanza.
  Hivi huyu mtu anaangalia mbele kweli?
  Wazazi wako wangekuwa hivo wewe hata ungezaliwa kweli.
  Just imagine wazazi walikuwa tu walimu lakini mtoto wa kwanza tu wamemzalia kwenye nyumbayao
  Kwani gari ndo maisha? Kwanini ukubali kubeba mzigo ambao unaharibu furaha na direction yamaisha yako kwa vizazi vyako vyote hapa duniani?
  Kuna siku usafiri ulishawai kuwa wa shida hapa tz kwamba gari liwe ni muhimu sana? Ukitakakwenda popote si unaenda? Mbona kuna routehata ya masaki –gongo la mboto bwana? Magari kibao mia tatu yako tu
  Maisha ni safari ndefu
  Ni safari inayoitaji maamuzi ya busara na magumu
  Tumia akili na nguvuzako zote kuamua
  Familia na jamii na taifa vinakutegemea
  Acha kuishi kwa tamaa
  Acha kujifikiria mwenyewe
  Acha kuwa mbinafsi
  Wengine walijitesa ili wewe ufanikiwe
  Angalia kesho tunaishi kwa ajili ya kesho maana leo imeshapita

  Kijana wa kiume wa kitanzania jipange.

  Nawatakieni sikukuunjema my dears
  Ningetoa no yangututafutane tule sikukuuu sema kuna mtu kaniudhi ndo huyo ananipiga mizinga asubuhi hii
  Nahofia na nyiehuku mtanipiga mizinga na mimi kuudhianana mtu sipendi na mimi kudai naogopa
  Stay with my smile bye
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Bila ya kuwa hata na Kistarlet kina Smile wanadenguwa sana, sasa hivi hapa mjini gari siyo kwa ajili ya usafiri bali tuimpress Bitches. Mwenye nyumba haeshimiki hapa mjini kuliko mwenye gari.
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Unavojiexpress hivohivo utapata wanawake wa type yako iyoiyo
  Cheni bandia noti bandia
  Jifunze kuwa real utaumia
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa bado hivi wewe Mwanaume mwenye Prado na mwenye Nyumba chamazi sijui kete yako itaanzia wapi? usitake kujifanyafanya hapa wakati watu kama nyinyi mnashoboka hata kwa Ma V8 za serikali STJ.
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160

  Hivi mwanamke anaekupenda anaweza kukubali kuona unadhalilika hapa mjini kwa ajili ya starehe kweli?
  Mwanamke anaekupenda kweli lazima atakubali kukuvumilia na kukubali kusaidiana na wewe katika matatizo pia atakushauri kuhusumaisha. Ila kwa sababu mnapenda mauzo ndo ivo wanawake nao wanachungulia wallet wanokomba kilichopo wanawakimbia…utajijuna madeni yako
  Na cha kusikitisha hata wanapokula na kupanda hayo magariyenu tunajua ni mkopo mtupu na tunajua unawasumbua na kuwapa pressure
  Lakini kwa vile mmeamua kufa pressure kwa ajili yetutunashukuru
  Ila mimi nimewaambiatu vile nawapenda hapa
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dada smile nakubaliana na wewe mia kwa mia aisee umenena nazano wengi tutajifunza sana na hii post yako makini
   
 7. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Dah! Bi dada-hayo ndo mawazo ya ki 'wife material'. Naomba uwaconvince wadada wenzio ili nao wafikiri kama wewe...
   
 8. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mmh, ni mawaidha mazuri... inaonekana b/f wako huwa humchuni kabisa which is very kind of you
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako Smile unadhani ninachosema mimi ndivyo nilivyo, siko hivyo mimi binafsi nina gari yangu yangu Toyota Hilux Surf, Diesel Engen in good Condition lakini usishangae ukiniona napanda daladala maana siishi kwa hisia za watu wengine.

  Unachopaswa ukifahamu ni kwamba maisha yamebadilika sana na Watanzania wana dharau sana imefikia kama huna kitu cha kuonekana basi wewe si lolote, na ukumbuke kwa nature ya binadamu hakuna anayependa adharalaulike mbele ya jamii, hii ndiyo inachangia Watanzania wengi tunaishi maisha ya kuigiza, binafsi mimi sasa hivi nimeshajiondowa kwenye mambo ya kuchangia harusi kiholeholela kila mwezi. am original and not copy.
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nyie ndo mnaotufanya tuwe hivo
  Kwani zamani watu walivokuwa hawana hata mkokoteni walikuwa hawaoi?
  Acheni ulimbukeni wa maisha
   
 11. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Gari ni mipango tu. Kama mtu umesoma na umeelimika, gari haliwezi kuwa mzigo. Cha muhimu ni mipango na kuwa na sababu maalum ya kuwa na gari. Kwa mfano, unaweza kuwa unafanya kazi na unataka kujiendeleza kielimu at the same time. Kwa Dar es Salaam, lazima uwe na gari ili kufanikisha mizunguko yote kwa wakati!
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kwanini ununue gari then uipaki? hapo ndo naona unakosea mara mia zaidi
  Iyo hela si ungeinvest sehemu ingine mkuu
  Hujui iyo ni hela?
  Heri hata ungenunua hisa twiga cement au crdb usubiri gawio mwisho wa mwaka
  Kuliko unanunua gari m 15 then unaipaki unapanda dalalala?
  Ndo maana uchumi wetu haukui , na wewe ni muhujumu wa uchumiunatakiwa ushtakiwe mkuu
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kama amekaa kukamuliwa anakamulia tuu...uamuzi ni wake
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Nimeishi Ulaya na private tranport tulikuwa tunatumia weekend tu, weekdays tunatumia Public transport, nadhani huna ufahamu na unachokisema na wala hujui ni nini maana ya kumiliki gari yako binafsi.
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  by the way hapa nazungumzia wanaonunua magari kwa hela ya wasiwasi i mean waliofanya gari kuwa first priority kwao
   
 16. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Trust me- sosholojia ni muhimu sana duniani hapa. Watu wanafight to get in na kustay in...Usipokuwa na gari kuna class flani ya watu huwezi mingle nao hata kama kwa kipato mko sawa au umewazidi. Labda unataka umuoe bi shosti wa class flani kisha competitors wako wote wana magari...Yani Imani inawashuka sana nyie dada zetu...Kwa sababu hata ww ukienda kuomba ushauri kwa shostito wako atakuambia;'mwanaume lazima awe na uwezo wa kukutunza/lea' japo wewe una hela na zipo kwenye hisa huwezi prove uko na uwezo wakumlea kwenye macho yao...hapo tayari mwenye gari kachaguliwa.
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naamni baada ya muda utageukia jinsia ya pili.
   
 18. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mhhh hapa nasoma tuu comment nikipata wasaa nitapita na mimi nichangie
  Smile maisha ni namna utakavyoamua uyaishi
  Ukiamua wewe ni mtu wa kutaka kila unalofanya lionekane na watu au kwa ajili ya kufanya jambo fulani utaishia huko huko
  Ishi uwezo wako na mshahara au kipato chako kinavyotaka uishi na usimuige fulani au usitake kumfurahisha fulani eti na wewe uonekane
  Maisha hayaendi hivyo
   
 19. Kuku wa Kabanga

  Kuku wa Kabanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 804
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  Unafaa sana wewe.
   
 20. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  washauri vijana wenzio bwana
   
Loading...