Kwa wachambuzi wa siasa; Predict CCM reaction

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Sidhani kama CCM watakaa kimya, wakati Sumaye 'mpinzani' wao kaongea, tena kawalima.

Naamini hoja za UVCCM zilikuwa kama kimbwa kidogo kimetumwa kuchokoza mbwa mgeni, mbwa mgeni aking'ate, then, mijibwa mikubwa ipate sababu ya kumrarua mbwa mgeni. Sumaye kaingia mkenge, kang'ata haka kambwa kadogo. Mijibwa mikubwa inakoki sasa kummaliza..

Walisemwa wa kaskazini, kukawa kimya. Wamesemwa wa Pwani, tusuburie vishindo...

Sasa ni nani ataongoza mijibwa mikubwa ... Makamba, Chiligati, Tambwe (hana nguvu), au Mwenyekigoda kabisa?

Wachambuzi wa siasa, hebu predictini hapa, ili yakishatokea msianze kusema ooh, mi nilijua. Hebu semeni mnachokijua leo leo...
 
Hawa wata watuma UV-CCM na makamba, mkulu hawezi kujitokeza yeye ndiye aliye watuma UV-CCM kutengeneza njia ya kuwaondoa wapambanaji kwenye uchaguzi wa CCM ujao.

Ila VITA YA PANZI NI FURAHA YA ..............!!!!!!!!
na
ADUI MWOMBEE NJAA.
 
Tatizo UVCCM vimeshazidiwa nguvu mkuu...

Sitta kapiga, Kimaro kakanyaga, Sumaye kasigina kabisa. So havina tena nguvu, vitatoka vinabwabwaja matusi ambayo hakuna atakayevisikiliza. So atatokea 'baba' yao mmoja, au hata kundi la 'baba' zao, kuwasaidia.
 
vinapigwa mabomu kama libya
 
Kwa kuwa Sumaye kasema, MIJIBWA mikubwa lazima itaibuka tu kujaribu kumgaragaza FTS. Cha msingi hapa itabidi wapime kwanza reaction yao iweje kwa sababu utakuwa ndio mwanzo wa kuwapa umaarufu akina six na FTS kwa ajili ya kinyang'anyiro cha 2015
 
Sehemu ya akili inayofanya vipimo ipo ndani kidogo ya sehemu inayoropoka. Kwa bahati mbaya sehemu ya vipimo kwa hawa wenzetu imeliwa na virusi. So hawataweza kupima...
 
Makamba sasa hana meno CCM, yaani hamjui kuwa Mzindakaya alimwandikia barua ya kumwambia astep down si ndiyo maana siku hizi kafyata mkia. UVCCM nao hawamtaki wanamwambia anaropokaropoka.:lalala::msela:
 
FTS
six
Richmond
Locks
Mangoes

Nani kupewa nafasi ya kushindana na Dr PHD ??

Ninavyo ona fisadi mjanja kaamua kuoga mto Yordan baada ya kukubali unabii wa nabii wa Israel. Kawaacha wenzake kwenye kundi huku wakiwa wametengwa na ukoma wa UFISADI, wakati yeye ndiyo alikuwa jemedari wao wa vita. Hawa walio na sifa ya utakatifu kutoka nyumba zote mbili ile ya zamani ya ufisadi na hii mpya ambayo imekuwa mwanzilishi wa utakaso ndo hasa moja wapo atakuwa mfalme, kama mafisadi waking'ang'ania nyumba yao basi huyu wa nyumba mpya atawekwa wakfu na nyumba yake kupewa hati miliki. Sasa wenye ukoma wame panic hawajui pa kushika. Labda kutakuwa na neema ya kikombe cha babu, bila hivyo ndo wamepigwa ban ya milele kwenye uongozi.

Mpaka hapo ndo mchezo unavyosomeka hatujui baada ya half time kama hii set up itaendelea au vipi, time will tell. Lakini na mimi na turufu yangu hapo kwamba ambaye ana ukoma hatagusa kiti cha enzi either awe kwenye nyumba ya zamani au mpya. Its a decree and nobody can go against it.
 
Makamba hana matatizo, wenye matatizo na mtu kama huyu Sumaye, wakina Sitta, Mwakyembe, Magufuri nk ambao kila kukicha wanaona ccm imeachana na misingi yake lakini bado wamo, si waondoke ...
 
Shy rose aliuambia mkutano wa uvccm kuwa makamba ndo tatizo kwenye na ndo kasababisha kimeanguka, makamba akamwambia mbona ye anavaa nguo fupi na ana hawala CDM?
NI kama namwona makamba akimjibu sumaye kuwa, ameona uchafu wa mwenzake wakat ye hajaoga
 
Anyway na predict wataendelea kugombania urithi hadi 2015 kwani Baba kashindwa kusimamia mirathi yake?

Kinachoendelea sasa ndani ya Chama ni Uendawazimu na hii inadhihirisha udhaifu wa wa uongozi.

Lakini mkumbeni Baba wa Taifa, "Hatuchagui sura.... tunataka kiongozi anapoongea na tumwangalia usoni tuone kweli anamaanisha anachoikiongea"
 
Lazima tu atapatikana wa kusema baada ya Sumaye kunene, Lkn wadau kulikoni babu Makamba simsikii tena kulikoni au kamwachia uwanja mwanae Mweziwakwanza Makamba?
 
Back
Top Bottom