Kwa wabunifu wa helicopter nchini

ishengom

Senior Member
Jul 23, 2012
152
67
Mimi kwa mtazamo wangu nimeona Tanzania kuna vipaji vingi sana, hasa baada ya kuona mbunifu wa helicopter huo Ruvuma na Arusha, hawa ni vijana ambao wamekuja na idea mbazo zinahitaji mkono wa serikali na kama kweli tunahitaji Tanzania ya viwanda basi majibu ndo haya, tayari hawa watu wana idea nzuri sana ambazo zinaweza kupatiwa mitaji ili waweze kutengeneza helicopter zenye ubora zaidi kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini ambazo ni cheap na kuweza kuuza kwa bei nafuu kwa watanzania na pia nchi za nje.

Usafiri huu ni muhimu hasa kwa nyanja nyingi kwa mfano kutumika kuwapeleka wamama wajawazito hospital huko vijijini ambako hospital zipo mbali na barabara hazipitiki na tunaweza kusambaza helicopter hizi kwa kila kituo cha afya kilicho karibu tanzania nzima ktk kuokoa maisha ya mama na mtoto,pia sio vijijini tu hata mjini kwenye vituo vyote vya zima moto hizi helicopter zinahitajika sasa basi wakati umefika kjanzia ngazi ya chini ya serikali za wilaya ,mkoa hadi taifa wakuu wa wilaya tuache na kushadadia kutoa studio za bure za kurikodi mziki tu...kama alivyofanya makondo kule kinonfoni lkn pia tutazame upande huu wapili ambao unafaida kubwa sna kwa taifa,ktk kutatua matatizo ya ajira.

Imagine tuwe na kiwanda Ruvuma na Arusha tutatengeneza ajira ngapi??
Wito wangu serikali kuanzia ngazi ya wilaya ambao w1tu hawa watapatikana wamewe msaada wa hali na mali na pia ktk kuw1ung1nisha na wataalam wetu waliosemea vyuo mbalimbali duniani waungane tutengeneze helicopter zetu ambazo zitakuwa affordable !
Wakuu wa wilaya huku ruvuma na arusha igeni fanyeni hii kazi na taifa litawashukuru sna
 
Vipi sheria za anga la bongo? Maana umesemea kimataifa pekee
 
Ni vizuri tukajikita katika kujifunza kutembea kuliko kuanza kufikiria kuruka,kama zilivyo hatua za makuzi kwa mwanadamu,maendeleo pia yana hatua zake.Kuanza kutiana ujinga wa kutengeneza helkopta wakati tumeshindwa hata kuwa na uzalishaji wa kutosha wa bidhaa muhimu kama sukari ni aina nyingine ya sanaa kama ilivyo sanaa ya kupiga push-ups jukwaani.

Tunaishi katika dunia ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia wake,hali hii inasababishwa na porojo za watawala u-chwara wanaowajaza upepo Watanzania kwa ahadi za kisanii na viapo feki eti wamejitoa kuwaletea Watanzania maendeleo huku mtanzania wa kawaida wa kule Nyang'holongo Mbogwe -Geita akiendelea kuusaka mlo mmoja wa siku kwa tochi.

Ni jambo jema kuwa na ndoto za maendeleo,lakini ukimkuta mtu anajisifia kuota ndoto ya kupaa angani mithiri ya ndege wakati hana mabawa,mtu huyo anapaswa kupuuzwa zaidi ya upuuzi wenyewe.Kuliruhusu Taifa kuishi katika dunia ya kufikirika-dunia ya ndoto ni kujifanya Taifa liwe duni kifikra na kuzalisha kizazi cha wavivu wa kutumia misuli ya ubongo katika kufikiri.

Nimepata bahati ya kuzunguka karibu robotatu ya vijiji vyote nchini,naelewa hali halisi ya ufukara wa watu wetu,yapo maeneo ambayo bado yanaishi katika zama za kati za mawe,sasa ninapomsikia mtu anayeota ndoto ya "Tanzania ya viwanda" huku Taifa letu bado halina hata uwezo wa kutoa huduma bora za msingi kwa watu wake,nampuuza mtu huyo hata kama ni msomi wa kiwango cha PhD kwa maana PhD yake yaweza kuwa na maana ya "Permanent head Disorder"

Tanzania si Dar,Arusha,Mbeya,Tanga na Mwanza pekee.Ni sehemu yote iliyo ndani ya mipaka yetu.Watu wavivu wa kufikiri wanajaribu kupima maendeleo kwa kuangalia maisha ya miji mikubwa huku wakiuacha ukweli uliodhahiri wa umasikini na ufukara wa kutisha wa sehemu kubwa ya Watanzania.

Badala ya serikali kujikita katika ubunifu wa kauli za kusisimua za maendeleo ya kufikirika,ni wakati sasa serikali yetu tukufu chini ya "mtukufu Rais wetu" mheshimiwa JPM irudi na kujitafakari upya na ikubali kuwa Changamoto zetu hazitokani na uhaba wa viwanda badala yake ijikite katika kuboresha hali za watu wake kwa kuwaandalia mazingira bora yanayowawezesha hata wale wanaotumia jembe la mkono,jasho lao liendane na kile wanachokipata.

Tukiendelea kumkamua masikini wa Taifa hili kwa kumrundikia utitiri wa kodi katika kila bidhaa na huduma,tutamfanya awe duni
 
Mi nadhani zitaruka tu! Zikishakamikika, wataletea wataalam wazikafue na zitafanya kazi tu. Kwani hao wanaozitengeneza walianza vipi? Tuwe na mawazo chanya jamani!
 
Kuna viwango vipo vimewekwa. Kama havijafikiwa hawatoruhusiwa kuruka!

Sina uhakika lakini mojawapo inawezakuwa njia mbadala ya kuzalisha nishati/kusukuma hicho kifaa kama injini itazima ghafla!
Huwa wanatakiwa kutengewa eneo lisilo na makazi ili wajaribu taaluma zao ili kuweza pia kupata alternatives mbali mbali baada ya kugundua mapungufu
 
Ila za nje huko ndo zinaruhusiwa na sheria za anga.
Watu inabid wakae waache kutumia akili za kufungiwa na wazungu mkuu, tufike sehemu tuishi sisis kama sisi sio nchi ufanye kitu chako cha maendeleo alafu eti unamgeukia mzungu akuruhusu kukitumia, MAD! MAD! MAD! Tunawachekaga Korea kaskazini sasa hapa ndo utaona walivyo na akili, mawazo mazur huja namna hii then watengew eneo serikali iwape fund changamoto zipo ila wakikusanya idea wakichanganya na wataalau wa hizo fan watatoa kitu kizuri.
 
Unazungumzia chombo kitakachoruka na mtu ndani au kwa rimoti?

Kama ni kwa rimoti naunga mkono hoja na hayo yanafanyika sehemu nyingi sana za nchi za wenzetu.

Lakini kama ni ya kuruka na mtu ndani huwa naona vinakaguliwa kwanza na taasisi inayosimamia vyombo hivyo.
Upo sahihi kabisa.
 
Helikopta ilishagunduliwa zamani sana.Hata wewe unaweza kuunda gari na huo sio ubunifu
 
Mimi kwa mgazamo wangu nimeona tanzania kuna vipaji vingi sana ,hasa baada ya kuona mbunifu wa helicopter huo ruvuma na arusha ,hawa ni vijana ambao walekuja na idea mbazo zinahigaji mkono wa serikali,na kama kweli tunahitaji tanzania ya viwanda basi majibu ndo haya,tayark hawa watu wana idea nzuri sna ambazo zinawezwa kupatiwa mitaji ili waweze kutengeneza helicopter zenye ubora zaidi kwa kutumia .alighafi zinazomatikana nchi ambazo ni cheap,na kuweza kuuza kwa bei nafuu kwa watanzania na pia nchi za nje,
Usafiri huu ni muhimu hasa kwa kyk nyanja nyingi kwa mfano kutumika kuwapeleka wamama wajawazito hospital huko vijijini amabako hospital zipo mbali na barabara hazipitiki,na tunaweza kusambaza helicopter hizi kwa kila kituo cha afya kilicho karibu tanzania nzima ktk kuokoa maisha ya mama na mtoto,pia sio vijijini tu hata mjini kwenye vituo vyote vya zima moto hizi helicopter zinahitajika sasa basi wakati umefika kjanzia ngazi ya chini ya serikali za wilaya ,mkoa hadi taifa wakuu wa wilaya tuache na kushadadia kutoa studio za bure za kurikodi mziki tu...kama alivyofanya makondo kule kinonfoni lkn pia tutazame upande huu wapili ambao unafaida kubwa sna kwa taifa,ktk kutatua matatizo ya ajira
Imagine tuwe na kiwanda ruvuma na arusha tutatengeneza ajira ngapi??
Wuto wangu serikali kuanzia ngazi ya wilaya ambao w1tu hawa watapatikana wamewe msaada wa hali na mali na pia ktk kuw1ung1nisha na wataalam wetu waliosemea vyuo mbalimbali duniani waungane tutengeneze helicopter zetu ambazo zitakuwa affordable !
Wakuu wa wilaya huku ruvuma na arusha igeni fanyeni hii kazi na taifa litawashukuru sna
Sawa lakini injini ya volkswagen? Jamani tusiwe kama hatujaenda shule ili kuweza kurusha ndege angani lazima uwe umejifunza vitu kama aerodynamics hii ni sayansi ya kurusha vitu angani, aerofoil, kuunda mabawa yawe na uwezo wa kunyanyuka kwa kuruhusu hewa ipenye kwa urahisi, aerobics kuongeza oxygen angani,aerobatics hapa kuhakikisha ndege haianguki kama jiwe toka angani inapoingia kwenye matatizo kama spinning etc ,aerate namna ya kuingiza hewa ndani ya kitu nk. ningeshauri hawa wataalamu wetu wapya wapelekwe kujifunza aerospace kwa sababu wanachokifanya sio ugunduzi mpya wapo wataalamu wa hiyo fani wapelekwe shule. Tunao engineers wengi waliofuzu air craft engineering and design unataka kusema wote hao ni mbumbumbu kwa kutokuona injini ya volkwagen kurusha helikopta??? Kwa taarifa helikopta ni ndege ngumu kutengeneza na kuirusha kuliko ndege ya kawaida!!!
 
Warujusiwe kuruka
Nashangaa hakuna taarifa ya habar imeonesha ubunifu huo
Watu kama hawa hawazaliwi mara mbili kama taifa tuwatumie vzur
 
Mimi niliposikia tu kuna Helicopter zinatengenezwa wazo lililonijia haraka haraka ni kwamba zitengenezwe Helicopter nyingi alafu wakati wa kuzitest watumike wale wakorofi wote wanaosumbua GAVOO....ndio wakuwe abiria.....haswa hawa vijana wa Baavichwa watakaokamatwa.....bila kumsahau yule aliyetukana.
 
Unazungumzia chombo kitakachoruka na mtu ndani au kwa rimoti?

Kama ni kwa rimoti naunga mkono hoja na hayo yanafanyika sehemu nyingi sana za nchi za wenzetu.

Lakini kama ni ya kuruka na mtu ndani huwa naona vinakaguliwa kwanza na taasisi inayosimamia vyombo hivyo.
Nadhani watajaribu haohao wanaoziunda...watavaa Helmet then wana fly.
 
ole wenu muangukie nyumba yangu.
1467887756887.jpg
hata mimi naweza kubun samak lakin aogelei.
 
Back
Top Bottom