Kwa Usajili huu mzuri na Kabambe kabisa unaofanywa na Yanga SC sasa, bila shaka Makocha wao wapya kutoka nchini Hispania ni hawa wafuatao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,568
108,910
Kutokana na Usajili wanaoufanya sasa ambao 'Kitaalam' na 'Kiufundi' ni wa Kipumbavu (Kipopma) ukiachilia mbali ni wa Kimasikini pia, Mabingwa wa Kutochukua Kikombe chochote ndani ya Miaka Mitatu Yanga SC tayari wameanza Kututambulisha 'Kisiri' Makocha wao wapya ambao nahisi watakuwa ni hawa Wawili wafuatao...

Kocha Mkuu

Wakili Msomi Simon (Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC)

Kocha Msaidizi

Injinia Hersi (Bosi Mwakilishi kutoka GSM)

Endeleeni tu Kusajili 'Kipuuzi' hivyo bila kuwepo kwa Kocha Mkuu au kupata Ushauri, kisha Ligi ikianza Simba SC ikiwa Bingwa mseme imenunua.
 
Utajuaje, labda yalikuwa ni mapendekezo ya kocha kabla hajaondoka?

Kocha ' anayependekeza ' jambo huwa ' anafurushwa ' kama ' alivyofurushwa ' DJ wao Luc Eymael? Hivi huko Vyuo Vikuu huwa mnaenda Kusoma?
 
Kocha ' anayependekeza ' jambo huwa ' anafurushwa ' kama ' alivyofurushwa ' DJ wao Luc Eymael? Hivi huko Vyuo Vikuu huwa mnaenda Kusoma?
Moron! Kupendekeza jambo ndio kinga ya kufukuzwa ukifanya fyongo? Yaani afanye ujinga halafu aachwe tu kisa aliwahi kupendekeza jambo?! Hizi akili za wapi?
 
Unajuaje kama kocha anayekuja ndo alopendekeza hao wachezaji wanaosajiliwa?

Cha muhimu hawavunji sheria yoyote ya Fifa, Caf au Tff waachwe wafanye wanavotaka.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kiukweli Yanga iwe na kocha isiwe na kocha ilikuwa ni lazima isajili tu kwa sababu walikuwa na timu dhaifu sana mwaka huu. Na ili Yanga isimame imara ilibidi ikimbizane na muda kusajili aidha kwa kutumia ripoti ya kocha aliyetimuliwa au kamati ya ufundi isitoshe Dk. Msola ni kocha kitaaluma na hata yawezekana wakatumia maoni ya Master Boniface Mkwasa kusajili kwani alikuwa na timu hadi karibia mwishoni mwa ligi.

Kutengeneza timu ya ushindi inachukua si chini ya miaka miwili na ukweli huu mchungu lazima mfadhili, viongozi na wanachama wa Yanga walijue hili kwani ndiyo njia sahihi ambayo Simba waliipitia kwa takribani miaka miwili kabla ya kuwa na timu ya sasa ya ushindi ambayo Yanga kala 4, Azam kala 2 na Namungo kala 2 wote hao ni kuanzia mshindi wa pili mpaka wa nne kwenye ligi (VPL).

Ombi langu kwa wanamichezo wenzangu tusiwakatishe tamaa Yanga bali tuwape moyo na tuwaeleze ukweli kuwa wasitegemee kupata matokeo mazuri hivi karibuni kwani ndio kwanza wanaanza kutengeneza timu ya ushindi. Na wasiwe na kiherere cha kufukuza makocha kila siku na kusajili wachezaji wapya kila mara. Wawe na utaratibu wa kusajili wachezaji wapya wachache angalau 6 kila msimu badala ya wanavyofanya sasa kusajili wachezaji 20 kwa msimu mmoja.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kiukweli Yanga iwe na kocha isiwe na kocha ilikuwa ni lazima isajili tu kwa sababu walikuwa na timu dhaifu sana mwaka huu. Na ili Yanga isimame imara ilibidi ikimbizane na muda kusajili aidha kwa kutumia ripoti ya kocha aliyetimuliwa au kamati ya ufundi isitoshe Dk. Msola ni kocha kitaaluma na hata yawezekana wakatumia maoni ya Master Boniface Mkwasa kusajili kwani alikuwa na timu hadi karibia mwishoni mwa ligi. Kutengeneza timu ya ushindi inachukua si chini ya miaka miwili na ukweli huu mchungu lazima mfadhili, viongozi na wanachama wa Yanga walijue hili kwani ndiyo njia sahihi ambayo Simba waliipitia kwa takribani miaka miwili kabla ya kuwa na timu ya sasa ya ushindi ambayo Yanga kala 4, Azam kala 2 na Namungo kala 2 wote hao ni kuanzia mshindi wa pili mpaka wa nne kwenye ligi (VPL).

Huo 'udhaifu' wao umesababishwa na Sisi 'Mashabiki' au ni 'Upopoma' tu wa Viongozi wao ambao walichokiwekeza sana tu ni 10% ya Wachezaji?
 
Umeongea kitu cha maana sana, shida ya wale GSM wanacheza na akili za mashabiki wao maadamu wao biashara zao wanafanya badala ya kujenga timu.
Chukulia mfano ka nilivyosikia kwenye chombo kimoja cha habari kua kuna tetesi leo wakawapiga panga wachezaji 16. Ina maana wanaenda kusajili wachezaji zaidi ya kumi msimu huu.
Sasa unajiuliza wanajenga au wanabomoa.
Simba msimu uliyopita iliwaacha kwa wakati mmoja wachezaji tegemeo ndo maana ilianza kwa kusua sua.
Sasa unasajili Wachezaji 16 unategemea waingie kwenye mfumo kwa wakati mmoja sio kweli.
Fraga ingekua yeye ndo anatakiwa alete matokeo hapo hapo tusingemjua ubora wake, lakini alianza kuingia kwenye mfumo taratibu saizi ameshakua kipenzi cha mashabiki.
Timu inatengenezwa haitokei kama ajali.
 
Huo 'udhaifu' wao umesababishwa na Sisi 'Mashabiki' au ni 'Upopoma' tu wa Viongozi wao ambao walichokiwekeza sana tu ni 10% ya Wachezaji?
Ulichoandika ni kweli lakini naomba nisilitumie hilo lako ni kali sana kwani nawaheshimu sana viongozi wa Yanga. Kikubwa kilichoisibu Yanga ni ombwe kubwa sana kati ya mfadhili, wachezaji na viongozi. Mfano mzuri jiulize ilikuwaje pamoja na utovu wa nidhamu wa kiwango cha lami aliouonyesha Morison lakini alipandishwa ndege kwenda Kagera na uongozi ulinywea ukapata kigugumizi kabisa. Je ni nani alitoa hiyo amri Morison aende Kagera? Na sasa pamoja na wapenda mpira wengi kupiga kelele kuhusu usajili unapofanyika walau basi baada ya mfadhili kumaliza makubaliano na mchezaji basi wakabidhiwe viongozi wamsainishe mkataba mchezaji kwenye ofisi za klabu ili mchezaji awajibike kwa uongozi wa klabu moja moja lakini wapi makosa yale yale bado yanarudiwa. Wachezaji sijui wanasainishwa wapi maana hakuna hata "banner" ya Yanga wala ya mfadhili. Na mambo yakienda hivi hivi tutegemee huko mbele yatakuja kujirudia yale yale ya Morison na Eyamel kuwa hawawatambui viongozi wa klabu na vile vile uongozi hautaweza kuwachukulia hatua yoyote.

Lakini yote kwa yote mimi bado ombi langu ni moja tuwaombee Yanga mfadhili, viongozi na wachezaji wakae pamoja watengeneze timu yao ikae vizuri kwani hakutakuwa na Simba imara bila kuwa na Yanga imara.
 
Pamoja na Uyanga wangu ila katika kipindi hiki viongozi wote wa Yanga hawatumii akili kabisa.
Kuwa na adui mwerevu ni bora zaid kuliko kuwa na rafiki mjinga. Yanga wanawekeza kwenye ujinga wakitegemea mashabiki wao nao ni wajinga. Kwa mtu mwenye akili timamu na sajili hizi za Yanga yetu atagundua Simba wanaenda kuwa mabingwa tena msimu unaoanza, sioni Mo akikosea popote kwenye kutafuta wachezaji wa kuziba mapengo.
Sio dhambi kuiga utulivu wa Simba hata kama ni wapinzani wetu, sasa ona uhuni wa kina Injinia na genge lao wanachikifanya. Katika kipindi hiki wangeanza na Mwalimu halafu yeye aje afanye kazi hiyo kutaalam.
Ni mjinga tu atasema ni mapendekezo ya kocha na kama ni yake sasa kashaondoka huyo anayekuja wana uhakika gani ataendana na hao wachezaji tena mwanzo wa msimu kabisa?
Kama Injinia na wenzako mna hela papara za nini kusajili? Hata zikibaki siku 5 unaweza mnunua yoyote kama kweli una hela. Hawa wote wanaosajiliwa wanakopwa tu kuhuni.
 
Binafsi kama mshabiki wa Yanga, mpaka sasa naona mchezaji aliyesajiliwa na kujitosheleza kila idara, ni Bakary 'Nondo' Mwamnyeto tu.

Kwa upande wa hao wengine naona ni wachezaji wa kawaida sana. Sijui lakini, ila kuna umuhimu kwa viongozi wa timu kufanya usajili kwa umakini. Yaani Waziri Junior ndiyo atubebe msimo ujao kwenye ukame wa mabao uliotukumba msimu huu!!!

Atanisamehe tu, ila simuamini hata kidogo.
 
mbumbumbu huu usajili unawauma sana, na bado!
cha kushangaza wamegeuka ma tactician, ma Agent na washauri wakuu wa Yanga, cha kujiuliza ni lini adui yako wa kivita akakushauri mbinu za kumpiga!
Kwa sababu ya ushabiki utasema hivyo, hivi ulishawahi kujiuliza kua kwa nini mwisho wa msimu huu Kagere hachezi?
Au ulishawahi jiuliza kwa nini Nchimbi alivyokua Police Tanzania alikua anafunga afu huku Yanga alikua anazurula tu?
Hatusemi kwa sababu ya ushabiki ila tunaangalia kiufundi zaidi. Kagere saizi achezi kwa sababu anashindwa kukifanya kile kocha anataka afanye akiwa pekeake mbele.
Kagere anafit zaidi kwenye mfumo wa mastraika wawili.
Unasajili Wachezaji bila kocha wanakuja kuingia kwenye mfumo baada ya mechi Tisa huko sasa hadi hapo mtakua wa ngapi kwenye msimamo. Na je timu ka simba na Yanga zitaweza kustahimili isipate matokeo mazr mechi kumi si mtakua mmevurugana hadi kwenye uongozi
 
Binafsi kama mshabiki wa Yanga, mpaka sasa naona mchezaji aliyesajiliwa na kujitosheleza mila idara, ni Bakary 'Nondo' Mwamnyeto tu.

Kwa upande wa hao wengine naona ni wachezaji wa kawaida sana. Sijui lakini, ila kuna umuhimu kwa viongozi wa timu kufanya usajili kwa umakini. Yaani Waziri Junior ndiyo atubebe msimo ujao kwenye ukame wa mabao uliotukumba msimu huu!!!

Atanisamehe tu, ila simuamini hata kidogo.

Ebu pendekeza ni mchezaji gani wa ndani anastahili kuchezea Yanga kama mtu mfano wa waziri Jr hastahili?
 
Naona Uzi wa kinafki na wachangiaji wanafki. Pilipili usiyoila !!

Izungumzieni Azam kwasababu wananunua wachezaji pia !!
 
Pamoja na Uyanga wangu ila katika kipindi hiki viongozi wote wa Yanga hawatumii akili kabisa.
Kuwa na adui mwerevu ni bora zaid kuliko kuwa na rafiki mjinga. Yanga wanawekeza kwenye ujinga wakitegemea mashabiki wao nao ni wajinga. Kwa mtu mwenye akili timamu na sajili hizi za Yanga yetu atagundua Simba wanaenda kuwa mabingwa tena msimu unaoanza, sioni Mo akikosea popote kwenye kutafuta wachezaji wa kuziba mapengo.
Sio dhambi kuiga utulivu wa Simba hata kama ni wapinzani wetu, sasa ona uhuni wa kina Injinia na genge lao wanachikifanya. Katika kipindi hiki wangeanza na Mwalimu halafu yeye aje afanye kazi hiyo kutaalam.
Ni mjinga tu atasema ni mapendekezo ya kocha na kama ni yake sasa kashaondoka huyo anayekuja wana uhakika gani ataendana na hao wachezaji tena mwanzo wa msimu kabisa?
Kama Injinia na wenzako mna hela papara za nini kusajili? Hata zikibaki siku 5 unaweza mnunua yoyote kama kweli una hela. Hawa wote wanaosajiliwa wanakopwa tu kuhuni.
Tatizo Watanzania huwa wanafikiri usajili mzuri ule wa wachezaji wa kigeni. Kwa Yanga wachezaji waliowasajili kwa sasa wote wako vizuri na ndio hao walikuwa wanawakatisha pumzi hata wachezaji wa kigeni waliopo Simba, Yanga na Azam. Ila hoja inaweza kuwa kuacha wachezaji 16 sio afya kigumu.
 
Mjichanganye tu utopolo PILATO yule wa As vita anakuja tutawapiga 20,

simba chama toka langu kindergarten
 
Back
Top Bottom