Stream line
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 393
- 239
Kodi ya majengo ilikuwepo. Lakini hakuna aliyeitilia maanani. Kuanzia mwaka jana kodi imewekewa mkazo na raia wengi wameanza kuitikia. Ila, tatizo ni TRA. ukienda ofisi za Kata unapewa demand note.
Hii imetoka TRA. Inazo namba zote na ni halali tayari kwa malipo Benki, ukijichanganya kwenda kujua habari ya kodi hii hapo ndo utaona maajabu.
Unaambiwa jengo lako lina limbikizo la kiasi kadhaa. ukitaka kujua ni kwa miaka mingapi hupati jibu la muda. Imefikia sehemu zingine wanakwambia kalete risiti za nyuma ulizolipia.
Swali TRA wanauhakika gani kuwa kodi hii imekuwa ikifuatiliwa na kutekelezwa na wamiliki wa majengo?.
Ikumbukwe kuwa wengi wa wamiliki waliojitosa kulipa kodi hii walikuwa ni waliopewa leseni za makaazi ili waweze kukopa. Na waliokuwa hawana haja ya mikopp hawakujihusisa na kodi hiyo. pia leseni hizi zilitolewa kwa wasio na viwanja vilivyopimwa.
Kupunguza maneno, Naishauri serikali iachane na miaka ya nyuma. Tukubali hasara tuanze upya tulipe kodi kama ndo kwanza inaanza. Mazingira haya yatamfanya kila mwenye jengo kuwa rafiki na kodi hii.