OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,677
- 120,360
Ukweli nasikia sauti ya kilio ktk kila kona ya Nchi. Swali langu ninani yuko tayari kuyatowa maisha yake kwaajili ya taifa?
Operesheni ya Makonda dhidi ya wauza madawa ya kulevya imefikia tamati wiki hii baada ya waziri mkuu kupiga marufuku utangazaji wa wauza madawa bila kuwa na ushahidi. Kwa hiyo hoja yangu haitausiana na masuala ya madawa ya kulevya.
Lakini nitatumia uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za watuhumiwa wa madawa ya kulevya kujenga hoja yangu. Watanzania wanatakiwa waelewe kwamba kuna watu wamepewa madaraka makubwa kuliko uwezo wao. Na katika kipindi cha teuzi za awamu ya tano kuna watu walipiga kelele sana, kwamba teuzi hizi hazijakidhi vigezo kabisa badala yake mamlaka ya uteuzi imefanya kumpa mamlaka mtu asiyependeka mahali Fulani ''usijempenda kaja''.
Kwa wale watumishi tunafahamu kwamba kabla ya kupewa substantive post ni lazima kwanza ufanyiwe vetting. Wana usalama wanakufukunyua kwanza kuona kama huna mawaa. Kwa wateule hawa wa awamu ya tano, naamini haikuwa hivyo.
Picha niliyoweka juu ni taarifa iliyoandaliwa na RC Makonda kwa vyombo vya habari ikisomeka ''MAJINA YA WATUHUMIWA MBALIMBALI WANAOJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA''. Ukisoma Between the lines ya orodha hiyo huwezi kuamini kama orodha imeandaliwa na Kiongozi Mkuu wa Mkoa, msomi wa level ya chuo kikuu, yaani Capital City yenye watu zaidi ya 5,000,000 inaongozwa na mtu wa namna hii.
Napenda kuwahoji wasomi walioko humu Jamiiforums, je hizi ndizo ethics za uandaji wa taarifa vyeti kama hizi. Je ninyi wanahabari ''vijipeperushi'' kama hivi vinakidhi vigezo vya kuwa chanzo cha habari katika vyombo vyenu?
Baadhi ya uandishi wa hovyo katika taarifa ya Mh.Makonda
- Matumizi ya majina yasiyo rasmi mf matumizi aka na majina mengine ya kihuni mfano Boss Chizenga, Deo Mchaga
- Matumizi ya jina moja la mtuhumiwa mfano Kiboko
- Kukosewa kwa majina ya watuhumiwa mfano Gaspal badala ya Gasper
- Kukinzana kwa majina ya watumiwa na wasifu alieleza mwasilishaji mfano Philemon Mbowe wakati mwasilishaji alimaanisha Freeman Mbowe
- Baadhi ya watu kutajwa kama waliitwa kusaidia upelelezi wakati orodha inasema watuhumiwa wanaojihusisha na madawa ya kulevya
- Kutaja majina ya kampuni kiajabu ajabu mfano Tanga Petrolium badala ya Petroleum
- Eti Parm Beach haaaaa haaaaa shule ya wapi hii inafundisha Parm badala ya Palm
Kwa nini sasa tuhuma za kugushi vyeti zisipate mashiko kwa uandishi huu wa msomi wa chuo kikuu?
Karibuni kwa michango