KWA TUNAO ZALISHA BIDHAA ZENYE MTAZAMO TOFAUTI KWA WALAJI JE TUNAFANYAJE?

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,889
2,000
KWA TUNAO ZALISHA BIDHAA ZENYE MTAZAMO TOFAUTI KWA WALAJI JE TUNAFANYAJE?

Ni ukweli ulio wazi kabisa kuna basdhi ya product either Watanzania hatuna utamaduni wa kula au kuna upotoshaji.

1. Sungura- Hatuna utamaduni plus Upotoshaji kwamba ni paka na kadhalika na ingawa badhi ya Madhehebu hawali hii kitu.

2. Bata za aina zote- Utamaduni hatuna.

3. Kware- Utamaduni hatukuwa nao.

4. Kanga ndege- Hatuna utamaduni wa kula.

5. Mayai ya kuku wa kisasa- Kuna upotoshaji

6. Kuku Broiler- Upotoshshi kiasi fulani.

7. Uyoga- Hatuna utamaduni wa kula uyoga ingawa ni chakula bora kabisa.<

8. Baadhi ya mazao sitajataja majina.

Nilivyo taja hapo juu utakubaliana na mimi kwamba vingi huwa hatuna utamaduni wa kuvila na vingine ni upotoshaji.Na ni vitu muhimu sana na pia ni biashara kubwa sana.

Hivyo ni jukumu la wazalishaji kutoa elimu ya kutosha kwenye hili, Kuelemisha na kufanya kila njia ili kupata watu wengi wa kutumia.

Wengi wetu huwa tunaishia kupost tu Matangazo, unapost tangazo unauza Sungura ilihali unajua kabisa most ya watu hawali au wanapotoshwa au hawana utamaduni .

Sema ni ubinafisi ila kwa Mfano wazalishaji wa Sungura wangeungana na Kuchangia gharama za kutoa elimu ya kutosha leo hii tungekuwa na walaji wengi mno wa Sungura na tungepishana nao Sokoni wakiuzwa.

Bila elimu kwa watu tutakuwa tunadanganyana tu tutatumia nguvu nyingi sana tena mno.

Wazalishji wa Uyoga nao wakaungana na kutoa elimu kubwa watu wangehamasika sana.<br>

Kwa nini Muungano kwa ajili ya matangazo ni mihimu sana? Ni kwa sababu Endapo mimi pekee nikatoa pesa kutoa elimu ya nyama ya sungura ninao wafuga Dar&nbsp; basi nitakuwa nawafaidisha na wafugaji wengine waliko Mara au Mbeya au Arusha.

Ndo maana Tangazo la Cocacola ni moja tu Dunia nzima, Make Cocacola kwanza angetoa tangazo la kusifia soda ya Fanta basi hata Nyanza Bottle Mwanza angefaidika na Tangazo la Cocacola Kwanza ya Dar.Hawa wana joint moja kwenye Matangazo.

CHSHA FARMING
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,889
2,000
siwezi kula mikuku ya kisasa wala mayai yake.
Ila soda unakunywa, Juice unakunywa. unajua vyakula kama Mboga mboga zinakuzwa na nini? Hahahaa au ukiona ni kijani basi unao ni za Sili? Unakula Nafaka kama Ngano au hujui Ngano yote tunayo kula Tanzania inatoka Ulaya na America?
 
antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
2,206
2,000
Kuhamasisha ulaji wa broiler na mayai ya kisasa kwa wingi, nahisi itakuwa kazi ya kuchosha.. Ukiwa mkweli utatangaza kama wanavyonadi sigara
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,889
2,000
Kuhamasisha ulaji wa broiler na mayai ya kisasa kwa wingi, nahisi itakuwa kazi ya kuchosha.. Ukiwa mkweli utatangaza kama wanavyonadi sigara
Elimu ndo kikwazo kwetu. Make elijlmu tulizo zipata za kusoma Handout ndo zinatupa shida.

Layers ni kuku kama wengine. Na wanataga mayai sawa na ya kuku wengine, Hata kuku wa kienyeji kwa sasa wanafugwa kama layers tu.

na pia Mboga za majani na matunda na nafaka nyingine zinapigwa sana madawa.
Wewe unajua mboga unazo kula zinalimwa wapi? usha wahi fuatilia zinako limwa? Fanya hivyo one day

Hahahaaa
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,889
2,000
Kuhamasisha ulaji wa broiler na mayai ya kisasa kwa wingi, nahisi itakuwa kazi ya kuchosha.. Ukiwa mkweli utatangaza kama wanavyonadi sigara
Na unajua kwamba Broiler hufugwa kama kuku wa kienyeji? Usha wahi kuona? na nyama yake huwezi itofautisha na kuku wa kienyeji? Hahaha siku ukijua utaelewa.

Hata layers wanafugwa huria kabisa the same na kuku wa kienyeji.
 
David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
1,813
2,000
Ila soda unakunywa, Juice unakunywa. unajua vyakula kama Mboga mboga zinakuzwa na nini? Hahahaa au ukiona ni kijani basi unao ni za Sili? Unakula Nafaka kama Ngano au hujui Ngano yote tunayo kula Tanzania inatoka Ulaya na America?
ndugu yangu hivyo vyote unavyosema nimeacha kutumia miaka 10 iliyopita'situmii kinywaji chochote cha kiwandani ata watoto wangu nimeanza kuwazoesha kutotumia hayo majuisi ya kiwandani.
Kifupi nimeweza kubadili ulaji kwa 80%
 
CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,889
2,000
ndugu yangu hivyo vyote unavyosema nimeacha kutumia miaka 10 iliyopita'situmii kinywaji chochote cha kiwandani ata watoto wangu nimeanza kuwazoesha kutotumia hayo majuisi ya kiwandani.
Kifupi nimeweza kubadili ulaji kwa 80%
Mboga za majani huli? Nafaka huli yaani mahindi make yanatiwa mbolea pia ambayo ina bust ukuaji wao.

Hutumii aina yoyote ya matunda make yanapigwa sana Madawa.

Hivyo tajwa hapo juu labda uwe unalima mwenyewe hapo sawa.
Hizi ngano tunakula unajua wanazalisha vipi huko Urusi na Ukrine na Canada?

Je mayai unayo kula ya kienyeji una uhakika gani kama ni ya kienyeji? usije ukaniambia kiini. make hapo ndo tunapigiwa hapo kwenye kiini na ukimaliza notakuambia kiini linatengenezwa vipi? Achana na Dunia ya sasa.

Pia kama ni ya kienyeji vipi anaye uuza unajuaje kama siku wanataga walijuwa kwenye dozi?

Je anaye kuuzia maziwa je siku Ng'ombe anaumwa na kupewa dawa huwa yale maziwa anamwaga chini? make kama yuko kwenye Dozi sharti maziwa ya mwagwe.

Je nani yuko tayari kumwaga lita 30 au 50 au 100 chini? kisa Ng'ombe wake wako kwenye Dozi?
 
ivan don

JF-Expert Member
May 26, 2017
337
500

Sasa mkuu upo hapa kubishana na wachangiaji au kuwapa elimu ili kama walikuwa wrong kupitia wewe wajifunze
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,900
2,000
jipe muda wa kutosha kushika soko usiwe na haraka .. pia tangaza na anza na watu wa karibu...
 
David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
1,813
2,000
Je mayai unayo kula ya kienyeji una uhakika gani kama ni ya kienyeji? usije ukaniambia kiini. make hapo ndo tunapigiwa hapo kwenye kiini na ukimaliza notakuambia kiini linatengenezwa vipi? Achana na Dunia ya sasa.

Pia kama ni ya kienyeji vipi anaye uuza unajuaje kama siku wanataga walijuwa kwenye dozi?

Je anaye kuuzia maziwa je siku Ng'ombe anaumwa na kupewa dawa huwa yale maziwa anamwaga chini? make kama yuko kwenye Dozi sharti maziwa ya mwagwe.

Je nani yuko tayari kumwaga lita 30 au 50 au 100 chini? kisa Ng'ombe wake wako kwenye Dozi?
nafuga kuku mwenyewe sinunui mayai,kuhusu maziwa ya ngombe pamoja na nyama huwa situmii nina mzio navyo.
yakupasa uelewe nimekwambia nimeweza kubadili ulaji kwa 80%..sikatai kuna baadhi ya vitu havikwepeki lakini haiwezi kunipelekea nianze kula vitu vingne ambavyo vinaweza kukwepeka ndugu.
Kama unakula hao broilers wako wewe endelea kula
 
David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
1,813
2,000
Mboga za majani huli? Nafaka huli yaani mahindi make yanatiwa mbolea pia ambayo ina bust ukuaji wao.

Hutumii aina yoyote ya matunda make yanapigwa sana Madawa.

Hivyo tajwa hapo juu labda uwe unalima mwenyewe hapo sawa.
Hizi ngano tunakula unajua wanazalisha vipi huko Urusi na Ukrine na Canada?
Hahahaaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom