Habari wakuu,
Tumeshuhudia teuzi katika serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr John Pombe Magufuli. Tofauti kabisa na matarajio yetu na wengi ameweza kuteua wapinzani kuingia katika serikali yake tena, tena amethubutu kabisa kuweka mpinzani kuwa kiongozi mkubwa wa mkoa.
Tunaona kwenye uteuzi wa huyu mama Anna Elisha Mghwira, mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro. Pia tumeweza kuona katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo.
Mheshimiwa Magufuli pia siku za nyuma mtakumbuka alimteua mwenyekiti wa TLP Mh Agustino Lyatonga Mrema kuwa mwenyekiti wa bodi ya taifa ya Parole. Zaidi ya hayo Rais Magufuli alidiriki kuruhusu wimbo wa wimbo wa Ney wa Mitego ambao ulikuwa na baadhi ya maneno yaliyoonekana kuwa na ukakasi kwa serikali yake.
Mambo kama haya hayakuonekana kwa sana kipindi cha Mh Kikwete japo uteuzi wa mpinzani ninaokumbuka ni wa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mh James Mbatia kuwa mbunge wa kupitia zile nafasi kumi za rais.
Pamoja na ukweli kuwa Mh Magufuli ameonekana kuwa mwiba mchungu kwa demokrasia kupitia matamshi yake, lakini matendo yake yanaonesha dhahiri kuwa yeye ni mwanademokrasia mzuri sana.
Je, haitoshi kusema Mh Magufuli ni mwanademokrasia kuliko mtangulizi wake Dr Jakaya Kikwete?
Nawasilisha..