Kwa teuzi hizi; Rais Magufuli ni mwanademokrasia kuliko Kikwete?

Alama tatu za Mnafiki:

(1) Akizungumza husema uongo
ref: Alisema hatochagua upinzani sasa amechagua... Huu ni Uongo.

(2) Akiahidi hatimizi
ref; Aliahidi milioni 50 kila kijiji, kusitisha ajira kwa mwezi mmoja n k Yote hakutekeleza.

(3) Akiaminiwa hufanya khiyana.
ref. Kauli yake kuhusu michango ya maafa kule Kagera.
 
Sio kwamba anaua democrasia? Alitakiwa aweke mazingira kwa vyama vya upinzani vikue sio kuchukua viongozi wake wakuu vife. Kifupi anaua democrasia
 
Kikwete alikuwa mwanademokrasia wa kweli na hawezi kulinganishwa na hawa uchwala wasiopenda yeyote awe kinyume chao. Vinginevyo huyu asingezuia hayo aliyoyazuia!
 
Ni kweli ni yeye JPM aliyeapa kwamba hatochagua wapinzani, na mpaka sasa hajafanya hivyo. Hao aliochagua wanaitwa "wapinzani" na sio wapinzani, kama unaelewa kinachoendelea.
Nakuunga mkono kwa asilimia 100 kuwa hapa nchini kwetu kuna 'wapinzani' na Wapinzani.

Hebu tujikumbushe kidogo uanzishwaji wa ACT wazalendo.

Kilianzishwa wakati ule tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015, na wakati huo ndiyo CCM ipo katika mazingira magumu sana ya wananchi kukosa imani nayo.

Ilibidi CCM 'itafute' mkakati wa kujinasua na hali ile.

Wakalazimika 'kuanzisha' chama cha ACT na kumfanya huyo mama kuwa mgombea wa kitu cha Urais, katika mkakati wa kuzigawa kura za upinzani, hususani kura za wanawake, ili mgombea wa CCM ashinde kiulaini.....

Ngoja nitumie msemo aliokuwa anatumia Mwalimu Nyerere kuwa ukiunganisha dots ya mchezo mzima huo, wenye akili tulielewa nini kinaendelea.....

Jiulize swali moja tu jepesi, kama kweli Magufuli ni mwanademokrasia wa kweli zaidi ya JK, ni kwanini hizo teuzi zake hajachagua hata mpinzani mmoja toka kwenye vyama vikuu 2 hapa nchini vya Chadema na CUF?

Hapo unapata jibu kuwa bado Magufuli anasimamia msimamo wake alioutoa kule Zanzibar mwaka jana kuwa kamwe hatachagua mpinzani hata mmoja kwenye serikali yake.....

Hiki mnachokiona kinachofanywa na Magufuli cha kuwateua akina Ana, Mkumbo, Mrema and others ni kuteua 'wapinzani' katika serikali yake, ambapo in reality hao ni sawasawa tu na kuwaita kuwa amewateua wanaccm wenzake, kwa kuwa hao tunawatambua kuwa ni Sisiem- B!
 
Habari wakuu,
Tumeshuhudia teuzi katika serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr John Pombe Magufuli. Tofauti kabisa na matarajio yetu na wengi ameweza kuteua wapinzani kuingia katika serikali yake tena, tena amethubutu kabisa kuweka mpinzani kuwa kiongozi mkubwa wa mkoa.

Tunaona kwenye uteuzi wa huyu mama Anna Elisha Mghwira, mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro. Pia tumeweza kuona katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo.

Mheshimiwa Magufuli pia siku za nyuma mtakumbuka alimteua mwenyekiti wa TLP Mh Agustino Lyatonga Mrema kuwa mwenyekiti wa bodi ya taifa ya Parole. Zaidi ya hayo Rais Magufuli alidiriki kuruhusu wimbo wa wimbo wa Ney wa Mitego ambao ulikuwa na baadhi ya maneno yaliyoonekana kuwa na ukakasi kwa serikali yake.

Mambo kama haya hayakuonekana kwa sana kipindi cha Mh Kikwete japo uteuzi wa mpinzani ninaokumbuka ni wa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mh James Mbatia kuwa mbunge wa kupitia zile nafasi kumi za rais.

Pamoja na ukweli kuwa Mh Magufuli ameonekana kuwa mwiba mchungu kwa demokrasia kupitia matamshi yake, lakini matendo yake yanaonesha dhahiri kuwa yeye ni mwanademokrasia mzuri sana.

Je, haitoshi kusema Mh Magufuli ni mwanademokrasia kuliko mtangulizi wake Dr Jakaya Kikwete?
Nawasilisha..
Wewe wasema
 
Kama kweli huyo Magu ni mwanademokrasia wa kweli kuliko JK, hebu tujiulize maswali machache kwa kufanya comparison.

Ni kwa nini enzi za JK, vyama vya upinzani vilikuwa na Uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa wakati hivi sasa imezuiwa hadi 2020?

Swali la 2, ni kwanini JPM ameteua Kaimu Jaji Mkuu kwa kipindi kisichojulikana, wakati jambo hilo halikuwahi kufanywa na Rais mwingine yeyote kati ya marais wote waliomtangulia?

Swali la 3, ni kwanini JPM amezuia Bunge kuonyeshwa Live, ambapo wananchi almost wote wanataka kuliona Bunge lao Live ili wawaone wawakilishi wao Bungeni namna wanavyochangia michango yao mbalimbali Bungeni?

Swali la 4, ni kwnini JPM katika teuzi zake za watendaji serikalini ambazo katika utaratibu wa Utumishi wa Umma wanapaswa wasionyeshe ushabiki wa wazi wazi wa vyama vyao vya kisiasa wanavyovipenda, lakini tumeshuhudia katika teuzi za JPM za nafasi kama za maRC, maDC, maDED na nafasi nyingine za aina hiyo akiteua almost 99% makada wa CCM?

Swali la 5, ni kwanini huko Bungeni kunaonekana zipo juhudi kubwa zinazofanywa na maspika wa Bunge letu ambao ni makada wa CCM pamoja na wabunge wenzao wa CCM kuhakikisha kuwa wabunge wote wa upinzani wanaosimamia kwa dhati maslahi ya wapigakura wao, wanapewa 'vifungo' ambavyo hata havimo hata kwenye kanuni zao za Bunge kama walivyofanyiwa akina Mnyika, Bulaya na Halima Mdee, kama siyo maagizo kutoka juu?

Kwa hayo maswali machache, jibu liko dhahiri kuwa ukifanya comparison ya JK na JPM, kuwa nani ni mwanademokrasia wa kweli, naamini kwa hizo 'facts' nilizotoa ni dhahiri kuwa JK anamzidi kwa mbali sana JPM katika suala la kuimarisha demokrasia hapa nchini.
 
Yes ana fqnya Demokrasia nzuri zaidi kwa Matendo inatia moyo ili kuongeza ufanisi Wa utendaji Tumpe nafasi mama Anna Mngwira aonyeshe Yale aliyokuwa anatarajia let us wait for her and Dr Kitila
 
Wadau mnalichanganya sana hili neno 'wapinzani'. Mpaka sasa sijamuona mpinzani aliyechaguliwa wala kuteuliwa.
 
Habari wakuu,
Tumeshuhudia teuzi katika serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr John Pombe Magufuli. Tofauti kabisa na matarajio yetu na wengi ameweza kuteua wapinzani kuingia katika serikali yake tena, tena amethubutu kabisa kuweka mpinzani kuwa kiongozi mkubwa wa mkoa.

Tunaona kwenye uteuzi wa huyu mama Anna Elisha Mghwira, mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro. Pia tumeweza kuona katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo.

Mheshimiwa Magufuli pia siku za nyuma mtakumbuka alimteua mwenyekiti wa TLP Mh Agustino Lyatonga Mrema kuwa mwenyekiti wa bodi ya taifa ya Parole. Zaidi ya hayo Rais Magufuli alidiriki kuruhusu wimbo wa wimbo wa Ney wa Mitego ambao ulikuwa na baadhi ya maneno yaliyoonekana kuwa na ukakasi kwa serikali yake.

Mambo kama haya hayakuonekana kwa sana kipindi cha Mh Kikwete japo uteuzi wa mpinzani ninaokumbuka ni wa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mh James Mbatia kuwa mbunge wa kupitia zile nafasi kumi za rais.

Pamoja na ukweli kuwa Mh Magufuli ameonekana kuwa mwiba mchungu kwa demokrasia kupitia matamshi yake, lakini matendo yake yanaonesha dhahiri kuwa yeye ni mwanademokrasia mzuri sana.

Je, haitoshi kusema Mh Magufuli ni mwanademokrasia kuliko mtangulizi wake Dr Jakaya Kikwete?
Nawasilisha..
Ila dini yetu imesahaulika kabisa
 
Tazama aina ya mpinzani alieteuliwa na jk kisha tazama Kwa jicho la tatu aina ya wapinzani anaowateua jpm nazani utapata jibu
 
Hamjamsikiliza vizuri kasema anateua mtu anaeweza kumwajibisha muda wwt.
 
Tatizo nyie mnaojiita wapinzani ambao ni wapinzani uchwara mnapenda kulialia sana,wakina mrema,kitira mkumbo na mama anna kuteuliwa kwao tayari mnasema vyama vyao ni CCM " B", ninahuakika 100% ata kama magufuli leo angemteaua baba yenu mbowe suga dady wa wema sepenga bado baadhi mngesema mbowe ni kibalaka wa CCM tokea zamani na wengine mngekuja hadharani na kukana kuwa mbowe ni jembe letu hawezi kuteuliwa na rais maghufuli na ushahidi wa video ya kukana ungepatikana ata kama amesha kula kiapo ikulu. chadema kwa siasa za maji taka nawanyoshea mikono.
 
Habari wakuu,
Tumeshuhudia teuzi katika serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dr John Pombe Magufuli. Tofauti kabisa na matarajio yetu na wengi ameweza kuteua wapinzani kuingia katika serikali yake tena, tena amethubutu kabisa kuweka mpinzani kuwa kiongozi mkubwa wa mkoa.

Tunaona kwenye uteuzi wa huyu mama Anna Elisha Mghwira, mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro. Pia tumeweza kuona katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo.

Mheshimiwa Magufuli pia siku za nyuma mtakumbuka alimteua mwenyekiti wa TLP Mh Agustino Lyatonga Mrema kuwa mwenyekiti wa bodi ya taifa ya Parole. Zaidi ya hayo Rais Magufuli alidiriki kuruhusu wimbo wa wimbo wa Ney wa Mitego ambao ulikuwa na baadhi ya maneno yaliyoonekana kuwa na ukakasi kwa serikali yake.

Mambo kama haya hayakuonekana kwa sana kipindi cha Mh Kikwete japo uteuzi wa mpinzani ninaokumbuka ni wa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mh James Mbatia kuwa mbunge wa kupitia zile nafasi kumi za rais.

Pamoja na ukweli kuwa Mh Magufuli ameonekana kuwa mwiba mchungu kwa demokrasia kupitia matamshi yake, lakini matendo yake yanaonesha dhahiri kuwa yeye ni mwanademokrasia mzuri sana.

Je, haitoshi kusema Mh Magufuli ni mwanademokrasia kuliko mtangulizi wake Dr Jakaya Kikwete?
Nawasilisha..
nachojua ACT ni Akiba ya Chama Tawala
 
Ivi JPM mimi mboana hanichagui shule imo kichwani.Huyo mama alitakiwa atafutiwe nafasi nyingine.Kama vipi aniteue ukuu was Wilaya Kibiti.
 
Ivi JPM mimi mboana hanichagui shule imo kichwani.Huyo mama alitakiwa atafutiwe nafasi nyingine.Kama vipi aniteue ukuu was Wilaya Kibiti.

Mkuu hapangiwi cha kufanya, ukimpangia ndo umeharibu kabisaa..
 
Back
Top Bottom