tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,115
Kwa wafuatiliaji wa bunge la sasa watakubali kwamba bunge la zamani chini ya chama kimoja lilikua bora kuliko bunge la sasa.
Bunge la zamank wabunge wote walikua bize kutetea maslahi ya nchi na majimbo yao katika kutetea maslahi ya nchi walikua wanaungana kuisimamia Serikali na katika kutetea majimbo yao walikua bize kweli kweli kuwakilisha shida za majimboni kwao ili kutimiza ile dhana ya mbunge kuwa mwakilishi wa wananchi.
Lakini katika bunge la sasa imekua tofauti yaani wabunge wa chama tawala wamekua bize kuitetea Serikali kuliko nchi yao.
Hata ukitokea ufisadi ndani Serikali haikosi wabunge watetezi, rejea Esrow.
Hii imeingia mpaka kwenye bajeti hawana umoja hata pale mambo ya msingi yanapo achwa na kushughulikia mambo yasiyo ya kipaumbele.
Wamekua bize kutetea chama chao kuliko majimbo yao. Hii inatokana na kuhisi wakiponda utendaji wa Serikali watakosa ubunge na kwa siasa za sasa wanahisi watachujwa wasigombee kupitia chama cha CCM na ni ukweli CCM inafanya hivyo.
Tena kwa hii CCM ya huyu bwana mkubwa itakua maradufu kuwafyeka wapingaji wa utendaji wa Serikali maana wao hupenda zaidi kusifiwa tu.
Wabunge pekee ambao wamekua na jicho la tatu kuisimamia serikali ni wapinzani lakini sauti yao haifiki popote wanamezwa na wingi wa wabunge wa CCM ambao walipaswa kuisimamia Serikali ila sasa wameamua kuitetea Serikali bungeni.
Ndipo nasema bunge la sasa halifai kuliko lile la chama kimoja. Hii haimaanishi sipendi vyama vingi bali naisikitikia nchi yangu kuja kupata maendeleo itachukua muda mrefu sana mpaka wabunge waje waache kuyatumikia matumbo yao sio leo.
Jiulize kama mbunge ameshindwa kuwa mzalendo kwa nchi yake ambae ana uelewa mpana kutokana na kutembea kwake na kukutana na watu mbalimbali hivyo kuwa na uelewa mpana juu ya mambo ya msingi kwa nchi yake yuko hivi walivyo wabunge wetu je kwa mwananchi wa kawaida. Tunategemea mwananchi awe mzalendo huku wabunge wetu wako radhi nchi ife ila CCM ibaki?
Ukiona bunge linakubali kutoa keshi billion 500 zinunue ndege ila kwenye kilimo zinaenda billion 3 au billion 18 kwa nchi nzima tena kwa kutoa kidodo kidogo kwa nchi nzima utajua kuna mahala hatuko sawa.
Naupenda upinzani ila watawala wamefanikiwa kuuzika. Tuna safari kuusimamisha upinzani wa mawazo huru, zaidi ya upinzani wa vyama.
Maana kwa sasa walio na mawazo huru hata ndani ya vyama huonekana wanatumiwa na wapinzani wao hata kama wanachosimamia ni kwa masrahi ya nchi.
Mfano huyu mbunge Bashe na CCM wamekua na vitisho kwa wenye mawazo huru kutowarudisha kwenye kinyang’anyiro kwa awamu nyingine. Hivyo basi kwa wale wafuata maslahi huufwata na kubaki kusifia tuu.
Bunge la sasa ni la hovyo kuliko la chama kimoja.