Kwa staili hii itatugharimu muda mrefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa staili hii itatugharimu muda mrefu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by oba, May 24, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli uliowazi kuwa watanzania walio wengi wakipewa nafasi ya kueleza nini chanzo cha matatizo na umaskin wetu huitupia lawama serikali hasa kwa kushindwa kuratibu maendeleo na ukombozi wetu.
  Moja ya mambo ambayo yananikera sana katika usimamizi na uendeshaji wa shughuri za serikali ni kitendo cha kuingia kwenye ofisi fulani ukiwa na shida na kukutana na askari kufuli akining'inia mlangoni eti kwasababu mhusika yuko kwenye kikao au amesafiri.
  Huwa ninajiuliza ofisi ni ya serikali au ya mtu binafsi?iweje mtu akisafiri au kwenda kwenye kikao ofisi ifungwe?hakuna utaratibu wa mtu kubaki na ofisi atleast akaendeleza huduma kwa wateja?wafanyakazi kama hao wanachukuliwa hatua gani na wasimamizi wao?au wanaogopa kumwachia ofisa mwingine asije akagundua madudu na uozo unaofanywa kwenye ofisi hizo?
  Kwa staili hii, na kwa kukosa uwajibikaji wa viongozi na wafanyakazi katika level zote,hatuwezi kupata maendeleo leo wala kesho.
  Nawasilisha!
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Mkuu nafikiri haya hayajaanzia kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini yameanzia juu huko hakuna uwajibikaji mtu anahesabika ndio ofisi na kama hayupo ina maana ndio ofisi haipo
   
Loading...