Kwa staili hii 'hapa kazi tu' inapoteza ladha

Chura

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,345
2,296
Rais wa awamu ya tano aliingia madarakani kwa sera ya "hapa kazi tu" ikiwa na maana ya kufanya kazi na kukuza uchumi. Watanzania wabatakiwa kufanya kazi ili nchi iendelee ni jambo lisilopingika na kwa kuonyesha ni jinsi gani Taifa litapiga hatia kiuchumi aliorodhesha mambo kadhaa ambayo yataambatana na Sera ya "Hapa Kazi tu" kuhakikisha kwamba maisha yamtanzania wa chini yanapata unafaa sawa na mtanzania wa kima cha juu na kati Tanzania ya viwanda, ajira kwa vijana, mahakama ya mafisadi na milioni hamsini kwa kila kijiji.

Mengine yamekamilishwa kama la mahakama ya mafisadi (majengo) tunasubiri kuona utendaji kazi wake haya ndo nilidhani kuwa Mh Rais angeyasimamia vizuri zaidi. Watanzania wengi wakiwa katika hali ya kusubiri ajira kupitia Viwanda na maisha bora tuliyoahidiwa kupitia falsafa ya "Hapa kazi tu" cha ajabu yanaanza kuibuka mambo ambayo yananifanya nijidharau kwamba
pengine sikuielewa vizuri siasa ya "Hapa kazi tu" na yafuatayo ni mambo
ambayo yanifanya nipate shida kuilewa hii falsafa au pengine ni U turn.

1: Kukataza mikutano ya siasa

Kuna msemo unasema " ili ufanikiwe unahitaji marafiki lakini ili ufanikiwe zaidi unahitaji maadui" Huwezi ukapiga hatua kama hutakua na watu wakukosoa.Ni ndoto tena za mchana kufikiri kuwa utaendelea kwa kuzungukwa na watu ambao wanakusifu kwa kila jambo. Tunahitaji watu wakukosoa ili tuboreshe na kufanya vizuri zaidi. Moja ya kazi ya vyama vya siasa (upinzani) ni kuikosoa serikali kwa maslahi ya wananchi wote kutazama mikusanyiko ya vyama siasa ambayo imewekwa kikatiba mosi kukataza Taasisi zingine zifanye kazi maana kwa vyama ambavyo havina Majimbo vitajinasibu vipi? Ni dhahiri kuwa tamko hilo linapingana dhana ya "Hapa kazi tu" Pili ni dalili mbaya za kuelekea kufikia malengo tunayoyatarajia kupitia falsafa ya "Hapa kazi tu" maana kutakuwa hakuna wakukemea pindi ambapo mambo yataenda kombo ni lazima wawepo wakusema ili wenyeuskani warudi nyuma wajipange.

2.Utumbuaji majipu kwa kufuata hisia (Emotions)

Majuzi rais alimtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa Bagamoyo Bi Azimina kwa sababu zilizotajwa kuwa ni kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi japo haikutajwa wazi ni utendaji upi huo kwa taarifa kutoka kwa mmoja wa mawakili maarufu inatajwa kuwa rais alimtumbua mama huyo kwa kuwa alitoa ushahidi uliowawezesha wapinzani kushinda kesi. Falsafa inasema ''Hapa kazi tu'' na kazi watu wanafanya kazi ila wanakwamishwa na mambo ya binafsi (personal issues). Sidhani kama ajira zitapatikana kwa kuhukumu namna hii nilidhani rais angekuwa anachakarika kuhahakisha waliokula fedha za Escrow na Epa cha ajabu wanahukumiwa wale wanao onekana wanasaliti chama. Adhabu za utumbuaji kama huu nilidhani zingewaangukia mabosi wa polisi waliojidharirisha kwa kuingia mikataba mibovu na yenye kutia aibu kama ile ya Lugumi.

3.Kukamata wapinzani

Jana inasemakana mbunge wa Singida kupitia CHADEMA Tindu Lissu alisafirishwa kwa gharama na ulinzi mkali kuelekea Dar es Salaam kujibu tuhuma za uchochezi. Hatukatai mtu kuwajibishwa kutokana makosa lakini je inamantiki katika dhana ya "Hapa kazi tu" mtu anakamatwa anapelekwa mahakaman anashinda kesi zaidi ya Mara nne. Huku matumizi yanabanwa mpaka wafanyakazi wengine wanaombwa kujigharamia ili kusudi waweze kuhamia Dodoma cha ajabu idara fulan unatumia mabano hayo kukamata watu ambao mwisho wa siku wanashinda kesi. Kuliko kutumia fedha na nguvu nyingi kukamata wapinzan ni vyema ikazitumia kuhahakisha kwamba zile milioni hamsini zinatua vijijini na viwanda vinajengwa au pengine Jeshi la polisi liachwe lifanye kazi kwa weledi watu wakamatwe kitaaluma na sio kisiasa hali inayoitia hasara serikali.

Mh Rais akazanie mambo ambayo aliyowaaminisha watanzania kuwa angeyefanya kama kutengeneza ajira kupitia viwanda, kufunga mafisadi nk.
Leo unakamata vijana kwa kuonekana Dodoma wakati wakurugenzi waliocheza na Lugumi wanapeta. Vivyo hivyo kwa viongozi wengine wasiitumie falsafa ya "Hapa kazi tu " ili waogopwe na watendaji wadogo bali waitumie ili kuhahakisha like walk chon it a lamia watanzania kwa kuwapa ushindi 2015 kinatimizwa. Kuna baadhi ya viongozi wamenza kuitumia falsafa hii ya "Hapa kazi tu" kuwakomesha watu wenye visasi nao. Haya yote hayana maana Watanzania wanatarajia maendeleo kupitia ''Hapa kazi'' na sio U turn hizi zinaweza zikwamisha Tanzania ya viwanda na uchumi wa kujitegemea.

Nachomekea tu afu napita zangu...
 
Yako mengi nashangaa mpaka sa iv Ikulu ipo kimya

Lugumi
Richmond
ESCROW
IPTL

Mengine tuliwasamehe ccm ila hadi haya makubwa mmeshindwa kutueleza nini kinaendelea
 
Walio karbu nae wanaogopa kumshauli kwa kuogopea kutumbuliwa tuliambiwa kwenye kampeni huyu ni brudoza a k a katapira
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom