Asubuhi: Nunua mikate/maandazi jioni, asubuhi tayarisha chai yako nyumbani.
Mchana: Kama ulivyosema unakula nyumbani, tayarisha msosi wako nyumbani (ubwabwa, ugali, mihogo, ndizi, viazi), badilisha mboga mara moja kwa wiki. (mboga za majani, samaki, kuku, ngombe). Ikiwa hukuathiriwa na Tanesco unaweza kuweka mboga yako kwenye jokofu. Pia unaweza kupika siku moja ukala siku mbili au tatu. Kazi yako kupasha moto tu.
Usiku: Tayarisha cha mchana cha kutosha ili kinachobaki kikufae usiku.
Ukifanya haya unaweza kupunguza kwa nusu au angalau robo ya matumizi yako