Kwa Rafiki yangu Mpendakula ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Rafiki yangu Mpendakula !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, Jun 2, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  C/o Chukua Chako Mapema, Kwetu, Hupati kitu
  P.O.Box 0000 Ulaji.[FONT=&quot]
  [/FONT]


  Rafiki Mpendwa,[FONT=&quot][/FONT]

  Wanyonge wasema hawataki utapeli wa kibanda cha Abdul na Malaika hewa.[FONT=&quot][/FONT]

  Pole sana kwa mtafaruku na mtaharuki uliokupata kutokana na harakati za Panya Buku zinazokutibulieni mlo wenu. Nasikia wale nao waliokondeana na kunyondeana kwa njaa nao eti wameanza kumshangilia Panya Buku. Kwa kweli hawa nao ni hatari sana maana wanaweza kumpandisha mtu joto la tumbo kiasi cha kumfanya atembee na gari lenye choo. [FONT=&quot] [/FONT]

  Katika hali hiyo,inabidi muwe makini sana katika kupambana na Panya Buku na hawa waliokondeana na kunyondeana kwa njaa. [FONT=&quot][/FONT]

  Nimezisikia hoja zenu kuhusu Panya Buku kwamba si mdudu mzuri kwa kuwa anawatibulia mlo wenu mnono. Bahati mbaya hoja hizo ziliwasahau wale wasiokuwa na mlo, achilia mbali ulionona,ambao wamekondeana na kunyondeana kwa njaa. Bila shaka wakati mnatoa hoja hizo hamkujua kuwa wale waliokosa mlo kwa njaa wangewasikia. Bahati mbaya zaidi hawa jamaa wamewasikia. Niliwashuhudia wakisema: "Alaa, kumbe mnakula! Bora Panya Buku awatimue!![FONT=&quot][/FONT]

  Sasa basi, bahati mbaya nyingine kubwa zaidi, ni pale mlipo 'wavaa' wanyonge waliokondeana kwa njaa kwa kuwaambia kwamba na wasimuendekeze Panya Buku kwa kuwa eti hata wao atawadhuru. Hapa nadhani aliyependekeza hoja hiyo ama hawajui wanyonge hawa au hayuko karibu nao. Pengine labda tuseme aliteleza? [FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]

  Hapana, hili la kuteleza silioni. Nadhani hayuko karibu nao na hivyo hawajui.Maana ni vipi utamwambia mtu mwenye njaa; asiyekuwa na chakula,ajihadhari na Panya Buku kwa kuwa eti atamtibulia mlo wake! Mlo gani? [FONT=&quot][/FONT]

  Kana kwamba hiyo haitoshi, zikaja hoja nyingine kwamba eti wale waliokondeana kwa njaa hawatumii akili zao na macho yao. Kwamba eti wangeliweza kufikiri na kujitazama, wangeliona kuwa si kweli kwamba wamekondeana ! ! ![FONT=&quot][/FONT]

  Rafiki yangu Mpendakula, [FONT=&quot][/FONT]

  Najua aliyetoa hoja hii si mchovu wakufikiri. Nia yake ilikuwa 'kuwazuga' tu wanyonge hawa waliokondeana kwa njaa ili nao wakubali kuwa na wao pia ni wenye kupata mlo wa mapochopocho na hivyo pia wajione kuwa wapo sawa na akina Mpendakula ambao wanapambana na Panya Buku anaewatibulia mlo wao.[FONT=&quot][/FONT]

  Nadhani mtoa hoja hiyo yakutaka kuwazuga waliokondeana kwa njaa, kutegeshea hoja yake kwenye ule mtazamo dhaifu kwamba watu wengi siku hizi hawapendi kuambiwa wamekonda. Amesahau kwamba mwenzie Panya Buku kisha pita kuwafafanulia kuwa kukondeana kwao sio tu kunatokana na njaa; bali njaa hiyo inachangiwa pia na akina Mpendakula wanaofakamia mlo pamoja na ule ambao ungewaendea wale waliokosa chakula. [FONT=&quot] [/FONT]

  Hata hivyo, nimegundua kuwa watu hawa walioathiriwa kwa njaa tayari walikwisha anza kutambua sababu za wao kuwa katika hali ya njaa na umasikini uliokithiri; alichofanya Panya Buku ni kuwaongezea ufafanuzi kwa ufasaha tu. [FONT=&quot] [/FONT]

  Hayo niliyashuhudia wakati nilipowakuta wakiijadili hii hoja ya kwamba hawatumii akili yao na macho yao ndiyo maana hawajioni kuwa nawao eti "wamenenepeana" kama akina Mpendakula. [FONT=&quot] [/FONT]

  Katika mjadala huo alisimama mmoja wao na kusema: "Ndugu zanguni tuliokondeana, hoja hii dhaifu ni ya kizamani, tena iliyokwishapitwa na wakati. Ni hoja itokanayo na hekaya za akina Abunuwasi. Leo mtu akikuletea hoja ya namna hiyo maana yake kakufanya wewe punguani usiokuwa na elimu hata ya kianzio. [FONT=&quot] [/FONT]

  Kauli hiyo iliitikiwa na sauti za "endelea,endelea",ikiwa ni maombi yakumtaka aendelee kufafanua toka kwa wale waliokuwa wakimsikiliza katika mjadala ule. [FONT=&quot] [/FONT]

  Yule bwana aliendelea kusema kwamba katika moja ya hekaya hizo ambazo zimo kwenye vitabu vya watoto wa shule, kuna hadithi ya mtu mmoja aitwae Abdul. [FONT=&quot] [/FONT]

  Alihadithia kuwa Abdul alikuwa Mpenda kula vya watu, pasipo kuwajibika. Hivyo siku moja alitunga uzushi wa kupatia mali toka kwa watu. [FONT=&quot] [/FONT]

  Alijenga kibanda pembeni ya mji. Ndani ya kibanda hicho akatandika zulia na juu ya zulia hilo, kwa pembeni akaweka kiti na viatu mbele ya hicho kiti. [FONT=&quot] [/FONT]

  Aliendelea kuhadithia kwamba baadae Abdul akaenda kuwatangazia watu kuwa ndani ya kibanda kile kuna malaika aliyemuagiza amuandalie kibanda hicho ili apate kukutana na kuongea na watu wema. Kwamba watu wenye madhambi hawangeweza kumuona na kuongea nae. [FONT=&quot] [/FONT]

  Bwana yule alihadithia kwamba Abdul alitambua kuwa watu wengi hawapendi kukiri hadharani madhambi yao. Hivyo kila aliyeingia kwenye kile kibanda alidai kuwa kamuona malaika amekaa kwenye kiti kile na akiwa amevaa vile viatu. Miongoni mwa watu wale alikuwepo pia Mfalme ambae Abdul alimpelekea koti hewa toka kwa yule Malaika hewa! Kama zawadi na Mfalme akalipa fadhila kwa kumpa Abdul vipande[FONT=&quot] elfu moja vya dhahabu ampelekee Mfalme hewa! Kama zawadi ![FONT=&quot][/FONT][/FONT]

  Hivyo yule bwana alihitimisha maelezo yake kwa kutolea mfano wa kisa hiki cha utapeli wa Abdul, na zile kauli za kutaka kuwatapeli kwamba eti wao hawajakondeana isipokuwa hawajioni tu jinsi walivyo nenepa!
   
Loading...