Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

Illakwahhi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2017
Posts
465
Reaction score
744
Wanasayansi wengi wamekuwa wakielezea ulimwengu wetu kuwa ni dude kubwa mno lisilo kuwa na mwisho(means the universe size is almost infinity)
Leo hebu tuchambue na kuangalia ukubwa wa dunia yetu
Kabla ya kuendelea naomba kuelezea kidogo kuhusu Galaxy, huu ni mkusanyiko wa nyota,sayari na vyote vilivyoko katika ukanda husika,Galaxy hutofautiana sana kwa ukubwa ila ya kati inakadiriwa kuwa na nyota bilioni 400 na mabilioni ya sayari,Galaxy yetu inaitwa milky way ambayo ina mabilioni ya sayari na na nyota,hebu sasa twende kwa picha
1.Hii ni dunia yetu,sehemu tunamoishi
2:Huu ni mfumo wetu wa jua,solar system

3.Huu ni umbali kutoka duniani mpaka mwezini
katika umbali Huu wa mwezini mpaka duniani waweza Panga sayari Tisa na zikaenea!

4.Hii ni sayari ya Jupiter ni kubwa sana
Hicho kidoti kidogo amerika kaskazini
5.Huu ni mwonekano wa Saturn ukiweka dunia katika ringi zake,mwonekano wa dunia sita katika ringi zake

6.Hebu tulinganishe Jua na dunia,
Jua 1=dunia milioni 1!!!,yaani dunia kwenye jua inaingia mara milioni 1

7.Hii ni picha maarufu ya dunia iliyochukuliwa kutoka maili bilioni 4 ,hicho kidoti kidogo ni dunia

8.Tuliangalia kuwa katika jua dunia huingia Mara milioni moja

Hebu tulinganishe jua na nyota zingine
9.Kuna nyota inaitwa Articus ni Mara 16,000 ya jua,hicho kidoti kidogo ni jua

10:Kuna nyota inaitwa Alpha scropti ni kubwa Mara 690 milioni kuliko jua,hicho kidoti kidogo ni jua

11.Kuna nyota inaitwa VY Canis major ni kubwa Mara bilioni 2.9
Kuliko jua,hapo usisahau kulinganisha jua na dunia!

Hicho kidoti kidogo cha mwisho ni jua
12.Hebu tuangalia galaxy yetu,ni ukanda wenye nyota zaidi ya bilioni 400 pamoja na sayari zake
Ndani ya sekunde moja mwanga huzunguka dunia Mara saba na nusu,ukienda kwa speed hiyo ulitakuchukua miaka 100,000 kutoka katika ukanda wetu(milky way Galaxy)
13:milky way Galaxy ni kubwa sana,na hyo doti ya njano ni nyota tyu ambazo unauwezo wa kuziona kati ya mabilioni ya nyota


Najua umeshawishika kuona milky way Galaxy(ukanda wetu wa nyota ni mkubwa sana lakini nikuambia kuwa ni kidude kidogo sana ukilinganishwa na dubwasha kubwa la Galaxy liitwalo 1C1011,galaxy Hii ukienda na speed ya mwanga ambayo nilikueleza kuwa itakuchukua miaka 6,000,000
Milky way ni hicho kidoti kidogo kulinganisha na 1C1011 Galaxy

14.Hebu tuchukue Hubble telescope, picha Hii ina mabilioni ya Galaxy na kila Galaxy ina mabilioni ya nyota na sayari mabilioni pia na kila doti unayoona hapo ni galaxy nzima


Oooh umechoka[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2],subiri
Hii ni dunia

Tukizoom zaidi Hii ni solar system

Tukizoom tena tunaona majirani katika solar system katika picha nzima ya galaxy

Tukizoom tunaona milky way galaxy ni hicho kidoti!


Local galactic Group
Ni mkusanyiko wa galaxy zaidi ya 54 ikikadiriwa kuwa na gravitational force centre kati ya milky way galaxy na andromeda

Virgo Supercluster
Huu ni mkusanyiko wa galaxy zaidi ya 100 uliogunduliwa mwaka 2014,group hii ni moja tu kati ya milioni kumi ya namna hii!

Ulimwengu unaoonekana!
hapa tunaongelea pale ambapo darubini zetu na telescope zimeishia,kuna umbali wa 93 billions light years kwa diameter, kwahyo ulimwengu wote tunaoongelea tunaishia hapo kwenye huo mduara kinachoendelea baada ya hapo ni space na anga kwahyo anga halina mwisho,kwhy kwenye hyo mduara ndipo wanasayansi wanapoishia haimaanishi kuwa ndo mwisho wa ulimwengu la hasha,ila mpaka huo mpaka kuna galaxy billioni 400 kila galaxy moja ina mabilioni ya sayari na nyota,inakadiriwa kuwa kuna nyota nyingi katika anga kuliko vipunje vya mchanga dunia nzima


Kwenye huo mduara ndipo tulipoishia ila ulimwengu unapanuka kuliko speed ya mwanga unavosafiri,hebu fikiria mwanga ndani ya sekunde moja unazunguka dunia Mara 7.5 halafu ulimwengu unajitengeneza zaidi ya speed ya mwanga its really amaizing

Yaani ukitoka nje ya huo mduara tunaenda kugusa ulimwengu tusiojua,yaani sehemu ambazo telescope zetu hazijafika kuzichunguza,inamaana porojo zote hizi za mabilioni ya galaxy ni ndani ni mduara huo,
Kwahyo ukitaka kujua ulimwengu mzimaa

Unachukua ulimwengu tuuonao
Observable universe+unknown universe=Total universe

Nini maana ya ulimwengu tusiojua?(unknown universe?)
hii ni sehemu inayoendelea baada ya mduara huo ni sehemu hii ina nishati iitwayo dark energy ambayo inawezesha Galaxy mpya kuundwa kila siku, nyota,sayari na galaxy zinaendelea kujitengeneza kwa speed zaidi ya light na ukumbuke speed ya light unazunguka dunia Mara 7 ndani ya sekunde moja,kwahy kutokana na hali hii ulimwengu utakuwa mkubwa sana na binadamu hatutaweza kuuona mwisho wake

Je ulimwengu mzimaa kuna galaxy ngapi ?

Jibu ni zaidi ya trilioni mbili,ulimwengu huu ni mkubwa mno mno mno mno
Universe is really big

Paulo illakwahhi Jf member!
 
elimu ya science ya ulimwengu ni elimu ya kusadikika haina ukweli wowote wala haiingii akilini kama tutakuwa na uwezo wa kufikiri,binadamu hatuwezi kuishi kwenye dunia yenye shepu ya chungwa,na kama ingekuwa kweli tungekuwa tunaweza kuishi kwenye milima mikubwa kwa kuganda pembezoni mwa milima bila ya kuanguka.

dunia haiwezi kuwa duara na maji kuganda nje ya dongo la dunia na kisha iwe inaruka angani kwa speed na masafa tunayoambiwa hii haiwezekani kabisa,katika uhalisi wa maji hayawezi kupinda kufata umbo la nje la kitu chochote,maji popote yalipo ni lazima yawe level hio ndio sifa kuu ya maji,na ndio mana tunatumia lever za maji kujengea majumba ili kupata usawa wa nyumba

jua na mwezi ni vitu vipo sawa sawa na umbali wake kutoka ardhini ni sawa sawa kama tunavyoviona,pia kama utaangalia jua na mwezi utakuta vipo ndani ya wingu la blue havipo umbali wanaosema,pia mwezi hauna ardhi ya watu kwenda kutua,tukiwa hapa tunauona kuwa mwezi ni kitu kinapitisha mwangaza(transparent),utazame mwezi mchana utaliona wingu la buluu kwenye mwezi na usiku utaona wingu jeusi kupitia kwenye mwezi.

tumefundishwa gravity ndio inayotuzuia tusipeperushwe na speed ya dunia hiki ni kichekesho kikubwa,kwanini gravity haiwezi kuzuia mabofu na mifuko ya plastic na ni vyepesi sana, kwa ufupi hakuna gravity ni vitu vizito vinabaki ardhini na vyepesi vinakwenda angani

hatuwezi kufahamu kila kitu lakini upo uwezekano kuwa ukubwa wa dunia ndio hauna mwisho(infinity) wala sio duara na haizunguki wala kuruka,uhalisi ni kama tunavyoona kila siku dunia ipo tuli imetulia.
 
Na nini kinasababisha usiku na mchana
 
umewa
Umewai kupanda ndege mkuu haya majibu yote utayapata ukipanda ndege plane
 
Kwa mara ya kwanza umenifanya nifikirie tofauti na vile nilivyojifunza kuhusu the universe. You might have a point if somebody rethink deeply.
Swali la kujiuliza hizo pics za umbali wa thousands of kms from unkown source towards our galaxy zimepigwa kutokea wapi.? Na kama ni kutoka katika spaceships na setelite hivyo vyombo vilichukua muda gani kufika huo umbali wa thousands of km?
Nitarudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ