Kwa nini wazanzibari waaliruhusiwa kuuvunja muungano, lakini watanganyika tunawekewa mipaka?

Status
Not open for further replies.

Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,437
3,457
Mwaka jana. wazanzibari waliujadili muungano na kuamua kuuvunja kwa kuitambua Zanzbar kuwa ni nchi. Mipaka ya kuujadili ama kuhoji juu ya muungano wanawekewa watanganyika tu, maana wazanzibari walishaujadili siku nyingi na wakaamua kuuvunja. Yaani Zanzbar imekuwa dogo janja na Tanganyika Kubwajinga? Hili hatutakubali. Tunaitaka Tanganyika yetu au la mabadiliko ya katiba ya Zanzbar yanayoitambua Zanzbar kuwa nchi yafutwe na wote tubaki watanzania tu.
 
Mkuu, hasara mnayo ninyi mliopoteza Tanganyika yenu. Sisi Zanzibar yetu tunayo na tunaendelea kuhakikisha inakuwa imara na huru zaidi. Kama mnategemea Mungu atawaletea Tanganyika yenu kutoka mbinguni bila kufanya jitihada, mnajidanganya.
 
Chintu: mbona unalala usingizi usio na hata jonzi ila bado hujachelewa jua halijatoka. Mim nashangaa sisi watanganyika hatuna katiba, bendera wala serikali ya kwe2, hii nch sijui ya namna gani? Tuwape tu zanzibar uhuru wao wa kujiongoza kama nchi huru itambulike kimataifa, si kuwakandamiza. Watanganyika 2amke kutafuta taifa le2. Tusiwafanye Mzee Nyerere na Mzee Karume ni malaika, sasa kuna wasomi weng wenye kupambanua mamb. Ki ukweli muungano umetosha kila mtu achukue chake afanye maendeleo yake co kila ck kujadili kero za muungano, tumechoka na vikao vyao visivyo na tija.
 
Nakulilia TANGANYIKA walikuzika na sasa nayaona matumaini ya kuwa utafufuka mama yangu.
Nawapongeza wazenj kwa juhudi zao.
Mi kama mtavunja au msivunje naitaka tu Tanganyika na wazenj wanaitaka tanganyika ili kujadiliana nayo mambo ya muungano vingnevyo watajadili vp na Tanzania?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom