Kwa nini watuhumiwa wa ufisadi wana nguvu sana ndani ya CCM?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
543
Mambo kadhaa sasa yanaonyesha kuwa watuhumiwa wa ufisadi wana nguvu ndani ya CCM na TZ kwa ujumla.Mfano katika uchaguzi mkuu ulioisha wameripotiwa kuwakampenia baadhi ya wagombea na wamepita Ubunge.Katika uteuzi wa nafasi mbalimbali serikalini watu wao pia wapo,katika uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi pia wamo na sehemu zingine nyingi.Sasa kwenye ugombea Uspika wa Bunge pia nguvu yao imeonekana.Ina maana sasa TZ tunakubali shinikizo la wenye fedha hakuna kabisa namna ya kuachana nao?
 
Nguvu ya mamba iko ku mayi. Mayi ya fisadi ni CCM. Wewe hulijui hilo? Watakucheka watu.
 
Mambo kadhaa sasa yanaonyesha kuwa watuhumiwa wa ufisadi wana nguvu ndani ya CCM na TZ kwa ujumla.Mfano katika uchaguzi mkuu ulioisha wameripotiwa kuwakampenia baadhi ya wagombea na wamepita Ubunge.Katika uteuzi wa nafasi mbalimbali serikalini watu wao pia wapo,katika uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi pia wamo na sehemu zingine nyingi.Sasa kwenye ugombea Uspika wa Bunge pia nguvu yao imeonekana.Ina maana sasa TZ tunakubali shinikizo la wenye fedha hakuna kabisa namna ya kuachana nao?

Njia pekee ya kuachana nao ni kuwakamatia bunduki. Maana kupitia sanduku la kura wanatununua na kuchakachua.
 
Njia ya bunduki si watatumia fedha zao kukodi Jeshi,vipi njia ya amani ya ngvu ya umma?kweli si siri tena kuwa TZ imetekwa,sasa na akili zetu nazo zimetekwa?Tuikomboe nchi yetu hata kabla ya 2015.
 
Bila mafisadi ndani ya sisiem, unyonge na udhaifu ndani ya chama hicho ungejieleleza vipi?

Mafisadi kama kundi la viumbe adimu..lipo na lina kazi..

Bila kundi la viumbe hawa..uimara, umadhubuti, ujasiri haki na heshima itajijenga vipi?

Lipo ili Yaanzishwe mapambano dhidi yao ..na Ushindi na heshima ya Mwanadamu ifikiwe...Bila mafisadi thamani ya kweli ya mtanzania Haitajitafsri kwenye jamii...!!!

Bila mafisadi ndani ya Chama... Misingi na mafunzo ya hekima ya Mwalimu Nyerere havitakumbukwa, kuliliwa na kuhitajika...ili vieleweke sasa kuliko alipokuwa hai!!

Mwanadamu hafundishiki bila kwanza kuoneshwa jambo la msingi ...akalichezea... na baadae kulihitaji kwa maumivu makali...!! SO MAFISADI WANA KAZI ...Wakiangamiwzwa ..tutaipata ile Tanzania tuliyokuwa tunaililia ..enzi za mwalimu lakini sasa tumeipata kwa JASHO LETU WENYEWE! Hilo tutakalolitumia kuwafuta ndani ya Chama na jamii ya Kitanzania.
 
Ama kweli ufalme wa mbingu watafika wachache,lakini wakumbuke kilio cha wengi ni kilio cha mungu,kila jambo lina mwisho,wako wapi akina kumzu banda na wenzie,lakini poa tu kila jambo lina mwisho
 
-CCM ya sasa sio ile ya JEMBE na NYUNDO ya enzi zile,

-Azimio la Arusha na misingi yake ya haki na usawa ilishakufa zamani,

-Waasisi wake wote wameshatangulia mbele za haki na waliobaki hamna kitu,

Matokeo yake hiyo vacuum iliyobaki imezibwa na hawa maharamia!
 
Mambo kadhaa sasa yanaonyesha kuwa watuhumiwa wa ufisadi wana nguvu ndani ya CCM na TZ kwa ujumla.Mfano katika uchaguzi mkuu ulioisha wameripotiwa kuwakampenia baadhi ya wagombea na wamepita Ubunge.Katika uteuzi wa nafasi mbalimbali serikalini watu wao pia wapo,katika uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi pia wamo na sehemu zingine nyingi.Sasa kwenye ugombea Uspika wa Bunge pia nguvu yao imeonekana.Ina maana sasa TZ tunakubali shinikizo la wenye fedha hakuna kabisa namna ya kuachana nao?

Kwa sababu ndo wenye pesa nyingi wanauwezo wa kutembeza mshiko haki ikapotea.
 
Njia pekee ya kuachana nao ni kuwakamatia bunduki. Maana kupitia sanduku la kura wanatununua na kuchakachua.

Bwana hmethod hata Avatar yako inakupinga hebu iangalie vizuri tena. Hili unaloongea haliwezekani Tanzania.
 
Back
Top Bottom