Nimekuwa nikifikiria sana juu ya hili swali. Kuna msemo kuwa ukijua chanzo cha tatizo basi utakuwa umepata nusu ya suluhisho lake. Watanzania wengi tuko kwenye kundi la kuganga njaa, iwe ni wakulima, wafugaji, watumishi wa serikali na hata wale wanaojiita ujasiriamali wadogo. Wengine hujiita wajasiriamali miaka nenda miaka rudi hakuna mabadiliko, maisha ni yale yale.
Sasa naomba tujadili kwa nini hatufanikiwi? Je ni kwa sababu ya kukosa mtaji? Ni kukosa elimu ya biashara? Je, ni masoko? Au ni sababu zipi unadhani wakulima wetu na wafugaji na wajasiriamali hawaendelei na hawafikii njozi zao. Karibuni kwa mjadala.
Mimi nimebaini sababu zifuatazo, lakini nakaribisha kama kuna criticism.
Usidhani nimesahau kuweka mtaji. Mtaji ni tatizo, lakini siyo tatizo kubwa sana kama hayo mengine tutakuwa nayo.

- Kufanya jambo kwa mhemko. Kwa mfano mtu anapata elimu fulani kuhusu biashara fulani au kilimo flani, then anaondoka na kwenda kufanya akitarajia mafanikio kama alivyosoma kwenye karatasi. Hakika, huyu mtu akija kufeli anakata tamaa na kurudi nyuma kabisa. Unakumbuka hata kwenye biblia Yesu aliposulubiwa na kufa, akina Petro waliamua kwenda zao kurudi kwenye uvuvi ambao ilikuwa kazi yao ya zamani hata kabla Yesu hajawaita? Kama siyo Yesu kuwatokea tena baada ya kufufuka, leo hii tusingesoma nyaraka zao na matendo makuu waliyoyafanya.
- Jambo la pili, watu wengi hawana taarifa sahihi kuhusu jambo wanalotaka kufanya. Kwa mfano, mtu anaenda kufuga kuku kwa sababu amesoma au amefundishwa kwenye semina ya ujasiriamali kuwa ufugaji unalipa. Anajenga banda na kununua vifaranga, lakini mchakato wa kuwalisha, kubaini ratiba za chanjo, kubaini dalili za ugonjwa etc, hachukulii seriously. Anadhani mambo yatajiendea tuu. Jirani yangu mmoja anafuga kuku wachache, lakini hajawawekea sehemu ya kutaga. Sasa kuku wake wanakuja kuingia jikoni kwangu na kwenye stoo wanataga humo. Mimi naokota mayai yeye wala hajui. hatuko serious.
- Kukosa uvumilivu
- Kukosa moyo wa kujituma
- Kukosa kuwa na njozi kubwa
Usidhani nimesahau kuweka mtaji. Mtaji ni tatizo, lakini siyo tatizo kubwa sana kama hayo mengine tutakuwa nayo.