Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 5,896
- 11,792
Kuna sababu nyingi sana, licha ya kuwa midrange za Samsung hazitumii sana zile strongest processor ukifananisha na simu za Kichina ila bado kuna sababu nyingi kwa nini watu wanapenda sana Samsung na leo nitakuambia kwa nini hizi simu ni kipenzi cha wengi
Na inapokuja suala la flagship, hakuna kama Samsung. Simu zao ni 99% perfect
Zifuatazo ni sababu kwa nini Samsung ni kipenzi cha wengi
1. Samsung zinatoa software update miaka mingi sana
Samsung hutoa update za muda mrefu sana hadi miaka saba. Chukua tu mfano Samsung Galaxy A16 ambayo hapa Mbeya inauzwa 365,000/= ila inapata update kwa 6 years, midrange nazo kama Galaxy A36 zinakuja na Android 15 na inapata updates hadi 7 years later. Angalia competition yake, hiyo A36 inashindana na Redmi Note 14 Pro+ ila Redmi Note 14 Pro+ inakuja na Android 14 ambayo tayari iko mwaka mmoja nyuma na inapata only 3 years of OS updates kwa hiyo mwisho ni Android 17, ila A36 itaenda hadi Android 22
2. Simu za Samsung zina design nzuri sana
Simu nyingi za Samsung zina design nzuri na simple tu. Kwa mfano ukiangalia sasahivi makampuni ya Kichina yanaweka kamera za maduara makubwa nyuma ya simu zao ili waweze kufit sensor kubwa na features zao nyingine ila ukiiangalia Samsung Galaxy S25 Ultra design yake ni simple tu, kamera 3 kubwa na ndogo mbili wamemaliza. Hawajazizungushia wala nini
3. Goodlock
View: https://youtu.be/ECOvFJMIsNk?si=e9ZREKAfYQVHeN0z
Hiki kitu wengi hawajui ila app ya Goodlock inaweza kubadilisha kila kitu kwenye simu yako ya Samsung na inapatikana Galaxy Store kwa watumiaji wa Samsung pekee
Goodlock inaweza kubadili style za Recent apps, inabadili style ya Soundbar, inabadili rangi za wallpaper, clockstyle, jinsi ya ku customize app drawer. Yani unabadili kila kitu humu, ukitaka sound bar unaifanya iwe ya duara, ndefu, au nyembamba ushindwe wewe tu.
Angalia video hiyo hapo juu kuhusu kila unachopaswa kujua kuhusu Goodlock
4. Simu za Samsung zimekamikika kila kona
Mona ya sifa ya simu za Samsung ni kwamba huwa zimekamilika kila kona. Mfano hizi S25 series unakuta zinatunza sana chaji, zina performance kubwa na hazi overheat, zina kamera kali zote ya mbele na ya nyuma, zina design nzuri, zina speaker nzuri, zina software nzuri na zinapokea updates hadi miaka 7, zina best AI ever kwenye simu, zina software nzuri sana yenye features nyingi, na bonus nyingine kuwa simu za Android kwa hiyo hakuna limitation za kijinga kijinga kama za iPhone. Bado zinaongeza kitu ambacho kampuni nyingine hawakupi mfano "Samsung DeX". Feature hii unapata kwenye Samsung tu, labda na Motorola. Kwenye Motorola inaitwa Smart Connect (zamani ilikuwa inaitwa "Ready for". Hata hivyo Smart Connect sio nzuri kama Samsung DeX. Na ukiondoa Motorola hamna kampuni nyingine yenye hii feature, isipokuwa Samsung tu. Na bado kuna app ya Goodlock ambayo inakupa extended customisation ambazo zitablow your mind, na mpaka sasa hakuna kampuni nyingine yenye app kama Goodlock
Pia flagship za Samsung (Ultra series) zinakuja na S pen, ni stylus pen ambayo ni useful kwenye activities nyingi sana
Ukitaka kujua Samsung DeX ni nini pitia hapa
https://www.pcmag.com/explainers/what-is-samsung-dex-how-to-use-your-galaxy-phone-on-a-tv-or-monitor
5. Simu za Samsung zina features nyingi sana kwenye software up
View: https://youtu.be/U3pEoy3dIt8?si=j7Vyiqa4ZafU9F3S
Angalia hiyo video, Samsung ina feature nyingi sana
6. Samsung in apps nzuri sana
Ni nani mwingine amegundua kuwa watu wanalalamikia wana bloatware kwenye simu za Kichina ila hawalalamikii kwenye Samsung? Sababu ni kwamba bloatware za Kichina ni useless na sio nzuri kama za Samsung
Za Samsung ni useful na ni nzuri mfano Samsung Messages na Samsung Dialer ni application nzuri sana kwa ajili ya kuoiga simu na kutuma message
Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Samsung video player app inasupport kucast video kwenye original aspect ratio yake ili ichukue nafasi kubwa iwezavyo kwenye TV tofauti na video Player nyingine ambazo zinacast tu shape ya simu, unakuta kama video haijai kwenye simu na kwenye TV haijai hivyo hivyo, haziwezi ku take advantage ya screen kubwa ya TV na aspect ratio yake. Video player ya Samsung inaweza kufanya hivyo na ukiondoa video player ya Samsung video player nyingine asilimia kubwa haziwezi. Video player nyingine ninayoijua inaweza kufanya hivyo ni VLC tu, ila hizi KM Player, MX Player, U Player, sijui Mi Video zote chenga tu inapokuja suala la ku cast, hususani video ambazo sio 21:9
6. Samsung zipo available kila kona duniani
Kila kona Samsung zinapatikana. Haijalishi upo Marekani au upo Togo, sijui Uganda Samsung ni rahisi kuzipata. Hii ni tofauti sana na simu za Kichina mfano Oppo au vivi unakuta hapa Bongo zipo zile mbaya mbaya tu na ukipata nzuri basi ni used au bei wanakuchapa. Unaweza kuzunguka Tanzania nzima usipate vivo V30 ila ukiambiwa utafute Samsung Galaxy A36, Mungu wangu hadi Kibaigwa unazikuta full box kabisa 😅😅
7. Flagship za Samsung zina vioo vizuri sana
Umeona hicho kioo kilivyo cheusi, hiyo ni S25 Ultra.
Flagship za Samsung zina vioo vizuri sana. Vina mwanga mkali, vinadisplay rangi nzuri, vigumu, imara na vyeusi sana hata mbele ya macho vinavutia. Sure hata ukichukua vioo vya Xiaomi 15 Ultra, vivo X200 Ultra navyo ni vyeusi sana ila ukifananisha na kioo cha Samsung Galaxy S25 Ultra utaona cha Samsung ni cheusi zaidi.
Mwisho wa siku nunua simu unayoipenda. Mimi napenda sana Xiaomi. Wewe unapenda simu gani?