kwa nini wanawake hawatoi sifa au kukandia?

http://ardictionary.com/One/1365Mwanamke nikama secretary kwa boyfriend wake, ama mumewe!! kama alivyo secretary asivyoweza kutoa siri za ofisi nje. The one who keeps, or is intrusted with, secrets.

Big up wadada wote na wamama wotee!!!!!!!!!!
 
Nahitaji sana kuelewa hili, mara nyingi humu utakuta topic nyingi zinahusu wanawake wa sehemu fulani sijui watamu, sijui wanajua mapenzi, sijui wanawe utakuta wanaume wanajitoa, wanachangia kweli experience zao na wanawake wa aina mbalimbali, wenye kutoa sifa haya, wenye kutoa dharau nao wapo, sasa nachoshangaa ni kwamba mbona wanawake wao huwa hawatoi experience zao kuhusu wanaume wa mikoa mbalimbali au nchi mbalimbali? sababu ni nini? au wamefundwa kuficha siri za wenzi wao?, au ni aibu? au hawana experience ya kutosha? ( which is understandable maana wanawake si donoa donoa kama wanaume) ni nini haswa?

Mbona huwa zinatoka nyingi. Niliona mmoja ameeleza kumzimia baba mkwe na kueleza jinsi mume wake alivyo mvivu. Mwingine alikuwa anatafuta mbinu za kumnasa mme wa mtu. Tatizo ninaloliona hapa anapotoa hoja mwanamke wanawake wenzake wanakuwa mstari wa mbele kumshambulia na kuhakikisha hoja haiendelei. Utakuta kinamama wamempa majina ya kila aina na kunukuu vifungu kibao vya misahafu kuonyesha jinsi gani alivyo mpambe wa shetwani. Inawezekana hilo linawakatisha tamaa wengine wenye nia ya kupata ushauri kuhusu wanaume au waume zao.
 
Si ndio wanaona aibu jamani? wengine waume na wachumba zao wamo humu kwa hiyo anaona bora achangie kwa kuona aibu kwa hiyo hawezi kuwa mkweli. Ila kuna wengine mbona wanajiachia tu kwa kuwa wawazi?
 
Back
Top Bottom