Kwa nini wakoloni walitupa uhuru kwa pamoja ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wakoloni walitupa uhuru kwa pamoja ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibokogiziba, Jun 12, 2011.

 1. k

  kibokogiziba Member

  #1
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipokua najaribu kupitia historia ya bara letu la Africa nilipata maswali mengi ambayo binafsi naomba msaada kwa wenye uwezo wa juu kuliko mimi. Natumai mtachangia kwa wingi ili niwe sawa kimtizamo.
  1. Kwa nini wakoloni walitumia nguvu kubwa sana kuingia barani Africa, na zama waafrica walipojipanga kidogo tu kudai uhuru wao hawa jamaa hawakutumia nguvu nyingi kupinga? Tizama waliondoka kwa upole tu tena kama vile wanasemezana, maana tuache kudanganyana wangesema watupige wangetumaliza maana silaha walikua wanazo au siyo.
  2. Baada ya kuachia makoloni yao(kama kweli tuliwafukuza mbona tuliendeleza urafiki na Yule Yule tuliemfukuza?) kwa mfano Tanzania imo katika umoja wa madola(hizi ni nchi zilizotawaliwa na waingereza) achilia mbali ufaransa na yale makoloni yao wanaushirikiano wa hali yajuu. (sasa iweje Yule adui ulomfukuza hivi sasa ndie rafiki mkuu) Napata hisia au kilikua kiinimacho tu ili wakajipange upya.
  3. Sasa cha kushangaza pale walipokwaruzana (mataifa makubwa)waliunda umoja wakujihami wao kwa wao kama NATO na umoja wan chi za mashariki USSR. Sasa acha zote hizo pale USSR na huu umoja wao ulipokufa hivi sasa wengi wa mataifa makubwa wanajiunga NATO (jee wanajihami kwa nani wakati umoja wa mashariki haupo?) Au ndo ile Berlin ya pili ya kuingia Africa nchi baada ya nchi na kufanya wanavyotaka?
  4. Tizama upokezi wa huyu waziri wa mambo ya nje ya marekani kama rais vile eeh? Huyu ndo baadhi yetu tunawaona wakombozi, hivi hawa si ndio wanaowapa shavu wakuu wetu na kutuachia mikataba wanayotaka wao. (kibaya zaidi tukigombana eti kidemokrasia tunataka wao ndio waje kutupatanisha) naona ile methali ya vita ya panzi…………………. Nimeisahau.
  5. Nani anajua mafuta ya Libya yanahitajika kiasi gani duniani, maisha ya watu wake ni nchi gani duniani walikua nayo. Ni rais gani Africa anaweza mwambia mhisani chukua 1% hata 10% mimi nipe 90%, still kitendawili. Hivi demokrasia ndio itatupa maisha bora au mtawala mwenyewe na misimamo yake mizuri, nani aniambie malkia uingereza anachaguliwa kila baada ya mda gani? Na jee hiyo ni demokrasia?
  6. Nahisi nchi za Africa zote zitaendeshwa kwa ukoloni mbaya zaidi na kama hatutakua macho wote kila siku tutauana kwa sababu ya demokrasia na zipo ajenda nyingi naziona waziwazi isipokua nashindwa nizipeleke wapi maana response yenu itasababisha nikupe maswali ninayohisi nawe yatakuumiza kichwa siku njema . nawakilisha!!!
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Uliishia la ngapi ndugu, ungekwenda shule haya yote ulio-uliza ungeyapata huko tena mengi na in deep! Kama elimu haikufika kwa kukimbia umande, nakupa pole-ila walaumu magamba kwani walifanya hivyo ili wakutawale kiurahisi!
   
Loading...