Kwa nini utumie nguvu kiasi hicho?

Kwa nini utumie nguvu kiasi hicho?

Kuna wanaume wengine ni watu wa ajabu sana,anakutongoza kwa kutumia nguvu mno

Na kama hutomkubalia ataanza kukuchukia na wengine kukutolea mabango( Si ustaarabu kabisa)

Kutongoza kuna kukubaliwa au kukataliwa na mara nyingi sisi hupenda kwa hisia na tunatakiwa kupata muda ili kuruhusu hisia zetu zifanye kazi

Hivi umewahi kumtongoza mwanamke,ukajifanya hushoboki sana,ukawa unamtongoza kawaida,ila kawaida yenye kudhamiria halafu ukaacha kumfuatilia,baada ya siku kadhaa ukashtukia mwanamke anakutumia SMS mwenyewe?

Huwa tunafikiria kama mwanaume alikuwa serious au lah! Na je ni mvumilivu na vipi kama ana haraka ya kukubaliwa si anataka apate papuchi alale mbele,huwa ni mawazo ambayo huwa tunawaza,na tunapenda sana kujua ulikuwa na nani au una nani muda huo,uhusiano wako kwa wanawake ukoje,una wangapi? Hizo haraka zako mmmh!!

Hatupendi haraka za wanaume kwa sababu hatupendi kumuonyesha kila mwanaume uchi,unapochezea uchi wa mwanamke halafu unamuacha bila sababu maalumu huwa tunaathirka sana,na tunaumia sana

Sasa mwingine anakutongoza kama vita

Mlikuwa mnasalimiana baada ya kukutaa hakuna cha salamu tena,

Wanaume bwana!!
Tuchukulie nimekutongoza leo itakukuchukua mda gani kunikubalia?
 
Back
Top Bottom