Kwa nini UK na RUSSIA kama hawapendani?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Ukiifuatilia habari mbalimbali hasa za waUK kana kwamba hawawapendi warusi na wanaponda kila kitu Chao.
Kwenye EURO football tournaments waingereza na warusi walipokutana walipigana ngumi hadi kupelekea warusi wengine kufukuzwa ufaransa kwa kosa la kuwachokoza wenzao.Kijana wa kirusi andre ashervin aliyekuwa anachezea Alsenal alifukuzwa Uingereza na inasemekana alikuwa na wenzake wakihusishwa kuwa mashushushu wa FSB kutoka Russia.

Meli la kivita la kirusi lilipopita pwani ya uingereza, walianza kukosoa kuidharau. Wengine kwenye mitandao wanasema linachafua mazingira na mimoshi, meli ya kizee na kila neno.

Historia inaonyesha kama sio USSR na jeshi Lake chini ya Stalin yaani red army kuingilia Kati kumdhoofisha Hitler uingereza ingeishia Pabaya ww2.

Wafuatilaji wa mambo hii inaweza kusababishwa na nini...
 
Hawa jamaa walikua allies for centuries since vita na Napoleon hata katika vita ya kwanza ya duania. Mapinduzi ya Urusi mwaka 1917 yalileta mvutano kiaina lakini katika vita ya pili ya dunia walikua allies tena.

Katika vita baridi mwaka 1947-91 kulikua na tensions kibao zilizopelekea mavutano mengi na matishio ya kuingia viwanja vya vita.

Mwaka 2014 mahusiano kati yao yalifikia pabaya. Serikali ya UK wakishirikiana na France na Germany, waliiwekea vikwazo vya kuiadhibu Russia katika European Union kwa kile waziri mkuu wa Uingereza (wakati huo) David Cameron alichosema ni kutokana na Urusi kuichukua rasmi Crimea na kwa serikali ya Urusi kusapoti sera ya utengano huko Ukraine.
 
Na kifo cha Alexandr Litvnenko kiliongeza tension pale Putin alipokataa kupeleka watuhumiwa kukabiliana na mashtaka.
 
Huyu jamaa alionekana msaliti na kuugua kwake wakaitumia KGB kumwangamiza kwa poisoning.

Walitumia mbinu kama za MOSSAD walizotumia kipindi cha tension middle East na viongozi wa PLO na Makundi mengine
 
Ile ilitisha, walimuekea sumu kwenye chai bwana ikammaliza taratibu. Ninaomba ile Technic isifike huki kwetu, kwa siasa hizi tutazika viongozi wa upinzani mmoja baada ya mwingine mradi tu ufungue mdomo.
 
Na kifo cha Alexandr Litvnenko kiliongeza tension pale Putin alipokataa kupeleka watuhumiwa kukabiliana na mashtaka.
Nakumbuka vizuri sana lile sakata! ila Putin mtata sana! Litvnenko alipo amua kumtimkia UK baada ya kuharibu akamfuata huko huko! unaifahamu historia ya Alex!
 
Hawa jamaa walikua allies for centuries since vita na Napoleon hata katika vita ya kwanza ya duania. Mapinduzi ya Urusi mwaka 1917 yalileta mvutano kiaina lakini katika vita ya pili ya dunia walikua allies tena.

Katika vita baridi mwaka 1947-91 kulikua na tensions kibao zilizopelekea mavutano mengi na matishio ya kuingia viwanja vya vita.

Mwaka 2014 mahusiano kati yao yalifikia pabaya. Serikali ya UK wakishirikiana na France na Germany, waliiwekea vikwazo vya kuiadhibu Russia katika European Union kwa kile waziri mkuu wa Uingereza (wakati huo) David Cameron alichosema ni kutokana na Urusi kuichukua rasmi Crimea na kwa serikali ya Urusi kusapoti sera ya utengano huko Ukraine.
Mkuu inaonekana hayo mambo ya propaganda za waingereza dhidi ya warusi yameanza kitambo source nyingine zinaonyesha tangu miaka 460 iliyopita, pia hata hiyo Crimea sio juzi tu tangu Crimea war 1853-56, ni hawa hawa waingereza waliofanya propaganda ili vita vianze. Hii dunia fitna inaonekana ni kila mahali
 
Sababu ni kwamba mafahari wawili huwa hawakai zizi moja na kila taifa hupenda kuwa juu kuliko mengine katika nguvu za kijeshi katika context hii UK na Russia wote ni world superpowers haiji tokea wakapendana
 
Nafikiri kiongozi wa warusi na ubabe wake, inasababisha chuki kwa raia na mali zao. Na hasa anavyoingilia mpaka mambo ya ndani ya nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom