Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 37,104
- 55,514
Unajua kabisa hapa duniani tunapita, wengi kufikisha miaka 90 ni bahati nasibu, kwa nini sasa tunaishi kwa kuteseka?
Unaamka asubuhi unawahi kibaruani, mara ufokewe na bosi wako, hayo yote ni ya nini? Kwa nini usiishi kama ndege tu, katika kujipatia mahitaji yako ya kila siku huku ukingojea siku ya mwisho?
Mengi tunayoyafanya hapa duniani ni mbwembwe tu, mwisho wa siku mwili wako tu utavishwa vazi la kawaida na kufukiwa, sasa mbwembwe zote ni za nini?
Unamuajiri mwenzako, unampunja ujira wake kwa kumlipa malipo madogo, yote ni ya nini; tunashindana na nani?
Unaingia kwenye mahusiano, mnaanza kutanguliza hela mbele,wakati kila kitu mmepewa bure kwa muundo unaofanana, hasi na chanya; sasa Unashindana na nani?
Mi naona watu wote duniani waishi kwa uhuru tu, waende popote duniani wanapoweza kwenda bila vikwazo mipakani, pia wale chochote wanachokiona kinafaa kuliwa, wale matunda pori na wanyama pori bila kuwa na kizuizi chochote kile, wawe huru kuongea wayapendayo; huo ndio ubinadamu katika kuishi kwa siku zinazohesabika hapa duniani.
Kwa nini tuwekeane vikwazo, tunashindana na nani?