Uchaguzi 2020 Kwanini tusiichague tena CCM?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,885
KWANINI NISIICHAGUE TENA CCM?

Na, Robert Heriel

Ni lazima tuIchague tena CCM kwa kura nyingi za kishindo. Sisi wanaume, wake zetu, vijana wetu wote tutamchagua. Hatuwezi kuchagua vyama vingine kwa sababu haviwezi kufanya kama CCM ilivyofanya;

ZIFUATAZO NI SABABU KUNTU ZA KUICHAGUA TENA CCM

1. UHAKIKA WA FUTURE YETU NA KIZAZI CHETU.
Mpaka sasa kila mmoja anauhakika wa maisha yake ya baadaye, uhakika wa maisha ya uzee kila mmoja anayo.
Kwa walioajiriwa wanauhakika wa kupokea pensheni zitakazowafanya wale uzee mwema. Hata sisi tusioajiriwa mimi na wewe tunaouhakika kuwa tukizeeka tutapewa pensheni kwani nasi tulikuwa tukilipa kodi. Hakuna haja ya kuwategemea watoto na wajukuu zetu. Tutapewa posho za uzee kwa kulitumikia taifa enzi za ujana wetu.

Sisi wazazi wenye watoto tunauhakika wa Future ya watoto wetu iliyowekwa na CCM. Watoto wetu hawatapata shida. Waliomaliza shule elimu ya juu na elimu ya kawaida. Tuna uhakika wa maisha yao kutokana na mfumo uliowekwa na CCM.

Watoto wetu wa kike tuliowazaa wanauhakika wa kuishi bila kutegemea wanaume watakaowaoa kutokana na mfumo mzuri uliowekwa na CCM. Vijana wetu wa kiume wameandaliwa mazingira mazuri, yaani kijana akifika miaka 25 anauwezo wa kujitegemea bila ugali wa shikamoo na Mboga za Marhaba.

Sisi watoto nasi tunafurahi kwa sababu tunauwezo wa kuwatumia wazazi wetu kila mwezi pesa za kujikimu kwa sababu mfumo uliokuwepo ni mzuri.

Hata sisi wazazi CCM imetuwekea mfumo mzuri wa kuwasomesha watoto wetu shule nzuri kabisa bila shida yoyote. Watoto wetu wanaendelea na masomo vyema kabisa, tunauhakika familia zetu zitakuwa za kisomi kutokana na kuweza kugharamia gharama za shule na chuo.

Kina Baba nasi, tunaishukuru CCM kwa sababu tunapata pesa ya uhakika ya kuwahudumia wake zetu, wanavaa wanapendeza, hawavai nguo moja kama sanda kwa maiti. Wananukia vizuri kwa sababu tunawanunulia mafuta mazuri na sio kunukia beberu kwa kushindwa kupaka mafuta kwa umasikini. Kwa nini tusiichague tena CCM ikiwa tunauhakika wa maisha?

Watoto wetu wanakula vizuri chakula chenye lishe, wanalala mahali pazuri, vyumba vyao vinanafasi inayoingiza hewa ya kutosha, wanatumia maji masafi na salama, kwa nini tusiichague CCM tena?

Vijana wote waliochuoni na mtaani wanauhakika wa kujiajiri au kuajiriwa. kazi zipo, wote tuna kipato kizuri cha kutufanya tuyafurahie maisha. Hakuna kijana asiye na kazi ya uhakika. Hata wanaobet wanafanya hivyo kwa burudani tuu na sio kwa shida. Kwa nini tusiichague tena CCM?

2. UHAKIKA WA MAKAZI
Tunashukuru mungu kwa Kutupa CCM. Watu wazima wote wenye umri wa kuanzia miaka 40 wote tunasehemu zetu za kuishi. Tuna nyumba nzuri tunazoishi na watoto wetu. Nyumba zetu zinaumeme na maji. Hakika maisha yetu ni mazuri chini ya CCM kuliko chama chochote kile.

Hata sisi vijana wenye umri wa miaka 23 - 39 mambo sio mabaya, tumepanga nyumba na kodi hazitushindi, pia wengi wetu tumeshanunua viwanja, tunahangaika kujenga, na hivi karibuni tutahamia makwetu. Sasa kwa nini tusiichague CCM ikiwa inatupa nafasi ya kufanya haya? Ingekuwa CCM haijaweka misingi ya sisi kuwa na uhakika wa makazi tusingeichagua lakini imeweka na wote tunauhakika wa kuishi sehemu nzuri. Hata wewe unayesoma ninauhakika utakuwa shahidi kuwa unamakazi yako mwenyewe kama upo juu ya miaka 40 na kama upo chini basi unamalizia kujenga.

3. MISHAHARA MINONO
I love You CCM, I need You CCM. Mwaah! Hakuna asiyepata mshahara mkubwa nchini kwetu. Kima cha chini cha mshahara kinakidhi mahitaji yetu. Watumishi wa serikali wanalipwa vizuri, hawalalamiki. Waalimu wanafundisha vizuri ndio maana elimu ipo juu ya nchi yetu kwa sababu walimu wetu wanalipwa mishahara minono. Mapolisi wetu nao Alhamdululah! Wanalipwa vyema ndio maana wanatulinda na mali zetu huku nyuso zao zikitabasamu.

Huko sekta binafsi nako watu wanalamba mishahara minono. Viwandani vijana wanachekelea mishahara minono inayowatosheleza kabisa wao na familia zao na kuweka akiba. Kwa nini tusipende CCM. Tunasema; CCM WE LOVE YOU! Mwaaah!
Tena tunafanya kazi masaa nane tuu yakizidi sana tisa. Kwa nini tusiichague tena ikiwa imeweza hayo?

4. UHAKIKA WA MAVAZI BORA
Kutokana na uchumi wetu kuwa mkubwa. Kwani tunalipwa vizuri, biashara zinaenda vyema. Tunauhakika wa kuvaa nguo mpya kabisa kutoka kiwandani, nguo OG sio nguo za mitumba ambazo zimevaliwa na watu wa mataifa mengine. Nani avae nguo zilizokojolewa na mtu mwingine, nani avae nguo zilzonajisiwa na uchafu wa mwingine, sisi sio masikini kwa kiwango hicho. Hata kama nguo hizo zifuliwe na kemikali bado ni Mtumba tuu. Hatuvaagi nguo za mitumba, bado hatujafikia umasikini huo. CCM imetusaidia na kutupa uwezo wa kununua nguo mpya kwa kadiri ya mahitaji yetu. Sasa kwa nini tusiichague CCM?

5. UHAKIKA WA HUDUMA ZA AFYA
CCM RAHA! CCM UTAMU KUNOGA! kwa nini nisiichague ikiwa watu wote tuna bima ya Afya. Hata ukiumwa sasa hivi unauhakika wa kutibiwa ukienda hospitali. Kwanza ukifika hospitali utakutana na Madakatari na wauguzi wanaopenda kazi yao kutokana na mishahara minono. Pili, madawa na vifaa vya tiba vipo. Yaani ni huduma tuu. Ukifa basi ni mapenzi ya Mungu na wala sio uzembe au kutokuwa na madawa. Wake zetu wawapo na ujauzito mambo bwereree! Huduma zao zipo. Wazee wetu wanatibiwa bure. Sasa kwa nini tusiichague CCM?

6. UHAKIKA WA UHURU
Uhuru unajengwa na Elimu, Ukweli, Na haki. Huwezi kuwa huru kama huna elimu, kwani usipokuwa na elimu huwezi kuujua ukweli, na usipojua ukweli huwezi kupata haki. Na kama hakuna haki basi hakuna uhuru. Watanzania wote wanauhuru na nchi yao. Wanawezo wa kusema ukweli wowote ule na wakawa na amani. Tunauwezo wa kumchagua tutamtakaye, tunauwezo wa kumuwajibisha yeyote akoseaye bila kujali cheo chake. Tupo Huru. CCM imetupa uhuru kamili. Piga kelele kwa CCM yakee!

7. UHAKIKA WA KUACHA URITHI
Dini inasema; Mzazi mwema huacha urithi kwa watoto mpaka wajukuu wake. Kinyume chake ni kuwa Mzazi asiyemwema haachi urithi.
Kutokana na mifumo tuliyowekewa na CCM kila mmoja wetu tunauhakika wa kuacha urithi kwa watoto wetu. Tunauwezo wa kuwaachia mashamba, viwanja, miradi, nyumba, mifugo na mali yoyote ile. Sisi sio wale raia wa nchi zingine wanaosema elimu pekeake ndio urithi jambo ambalo sio kweli. Elimu ni kitu kingine na Urithi ni kitu kingine japo vyote vinategemeana. Tunawapa watoto wetu elimu ili waweze kuvitumia vizuri vile vitu tutakavyowapa wavirithi hapo baadaye. Kwa mfanoi. mzazi anaowajibu wa kumpa mtoto elimu ya biashara ikiwa anamiradi atakayomrithisha mtoto, au elimu ya kilimo na ufugaji ikiwa atamrithisha mifugo au mashamba.
Wazazi wote chini ya CCM tunamali za kuwarithisha watoto wetu ili litimie lile andiko kuwa mzazo mwema huwarithisha watoto na wajukuu. Kwa nini Tusiichague CCM ikiwa wote tuna uhakika wa kurithisha watoto mali zetu.

Wajinga wa nchi nyingine hudanganywa na kujikuta wakisema sio lazima urithishe watoto mali, elimu inatosha, wakati huo huo viongozi wao wa nchi huwekeza na kununua mashamba maelfu ya heka, huanzisha miradi mikubwa ambayo kabla hawajafa huwarithisha watoto wao. Watoto wa masikini wakimaliza shule huhangaika kutafuta ajira wakati watoto wa viongozi wakimaliza shule huenda katika urithi walioandaliwa na Wazazi wao wenye hekima.

8. UHAKIKA WA KUTEMBEA DUNIANI
CCM inatupenda hakika. Watu wote tunauhakika wa kutembea duniani tukitaka. Mchakato wa kupata Hati ya kusafiria(Passport) ni bei nafuu kwa kila mmoja wetu. Pia inatolewa bila masharti magumu. Nafikiri kila kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 25 ana hiyo Passport. Kutokana na dunia ya sasa kutoka nchi za nje ni muhimu sana hasa kwa vijana wachangamfu na wachakarikaji. CCM imetusaidia sana kwa hilo. Kwa nini tusiichague tena?

Kwa nini nisiichague CCM ndugu zangu?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Ndugu Watanzania wenzangu, mtu yeyote kati yenu asifanye kosa la kuirudisha ccm madarakani, mtajuta kwa miaka mingi ijayo wakati wa mabadiliko ni huu.
 
Yahani hapo(nje ya fasihi) 1. Ndugu@Robert umekuwa msahaulifu haraka namna hii kweli?
- Ni Magufuli na CCM yake ndo walio badili sheria ya mifuko ya hifadhi za jamii
- Wameweka kikokotoo kinacho punja mstaafu kwa kuondoa kinacho MPA maslahi makubwa.
- Wameondoa fao la kujitoa na kulazimisha mtu kuchukua mafao yake akifikisha 50+yes! , hata kama una 20yrs sasa hivi, wakati huo wao mafao yao yote yaliyo nona huyachukuwa kila baada ya miaka 5
KUMCHAGUWA MAGUFULI NI HATARI KWA USTAWI WETU.
MSIWE NA MAHABA NA MWANA SIASA/CHAMA CHA SIASA KUWENI NA MAHABA NA USTAWI WENU NA VIZAZI VYENU!.
 
Hizo ahadi za kufikirika wakae nazo kwenye makaburasha ,mwaka huu wananchi hawataki kusikia mikakati ya wala sera lengo ni moja tu kumtoa nduli ndani ya mipaka yetu.
CCM ndie nduli alieivamia Tanzania ukipima sasa nduli huyu amevuka mipaka baada ya maisha kusonga mbele WaTanzania wanarudi kule kupigia magoti watawala.

Asie jitambua utu wake ndio ataipa CCM kura yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom