Mtu ninakuwa nawe kimapenzi kwa muda mrefu tena tukipeana mapenzi na ahadi motomoto!
Tunafanya mengi katika sehemu mbalimbali, nikiwa na matumaini mwisho wa yote tutakuwa pamoja katika ndoa!
Lakini siku unakuja kuniambia "eti hatuendani kiumri!"
Hivi Una akili sawasawa wewe?
Ina maana hukuliona hilo, toka enzi zile nafanya michakato ya kukupata?
Utawezaje kulipa upotevu wa mda na gharama zangu kwako enzi zile nalala usiku wa manane kisa tu, nikutumia msg ya mahaba?
Inauma sana Jamani, yaani mda wote ule, leo tuko katika hatua za mwisho ndio uone umri Ni tatizo?
Sio siri...Town naiona nuksi!