KWA NINI TUNAACHA MISINGI YA MAHUSIANO

mfwimijr

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
203
152
Ndugu wanajukwaa, Habarini za usiku.

Nyakati za sasa kumekuwa na changamoto kubwa kimahusiano, kwa mtizamo wangu ni kutokana na kuwa na matamanio ya kimahusiano au vitu na kuacha misingi ya asili ya mahusiano, kwa mfano mwanamke anaweza mpenda mwanaume kutokana na kipato chake pasipo kutambua kuwa kipato hakina uwezo wa kuoa au kudumisha mahusiano ijapokuwa kitaleta na kujenga furaha ya muda mfupi na isiyodumu. Kadhalika mwanaume anaweza mpenda mwanamke kutokana na mwonekano wa kimaumbile kama tusemavyo uzuri wa nyumba ni choo (chura) pasipo kutambua kuwa kutokana na mabadiliko ya kibaiolojia na vitu vinginevyo baadaye anaweza badilika na kupoteza mwonekano huo au umependa kabinti modo, je siku umbile la mwili litapobadilika itakuwaje?.

Kuna kila sababu ya kujifunza kupenda kwa asili, kumpenda mtu jinsi alivyo maana katika hali yoyote ile upendo wako kwake hautapungua but ukipenda kwa sababu fulani tambua kuna wakati hiyo sababu yaweza potea kulingana na mazingira au mabadiliko ya ukuaji na kibaiolojia.

Chanzo cha mahusiano kutokudumu ni kutokana na wenzi kupendana kwa sababu, kila mmoja anampenda mwenzi wake kwa sababu fulani ila si pendo litokalo moyoni.

Usiku mwema
 
Mie ndio maana huwaga naamini katika 'Chemistry' Mwanaume una 'click' nae hadi rahaa,ukimkosa dakika tano unakosa furaha,anajua udhaifu wako kabla hata hujamwambia...ni Rafiki kwako kiasi kwamba akikuudhi unaweza kumwambia umeniudhi,sio kuyaweka kifuani,ila saa nyingine kupata mtu wa hivi ni tabu,tunachukua yeyote aliyejionyesha 'interest' kwa sababu ni convenient kwa wakati huo...
 
Mie ndio maana huwaga naamini katika 'Chemistry' Mwanaume una 'click' nae hadi rahaa,ukimkosa dakika tano unakosa furaha,anajua udhaifu wako kabla hata hujamwambia...ni Rafiki kwako kiasi kwamba akikuudhi unaweza kumwambia umeniudhi,sio kuyaweka kifuani,ila saa nyingine kupata mtu wa hivi ni tabu.
Na ukimpata wa hivyo ni raha isokifani.
 
Back
Top Bottom