Kwa nini TRA na PCCB wanafanya Siasa?

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Nashangaa kuona hizi taasisi mbili za serikali zinafanya siasa badala ya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Mfano ni mara kwa mara tumeona TRA na PCCB wamekuwa wakijitokeza kujibu tuhuma ambazo zinawakabili kisiasa badala ya kuleta ushahidi, ni jambo la kushangaza kuona TRA wana under estimate mapato ili waweze kufanya kazi ndogo na hatimaye kupongezwa.

Mfano ni katika kukusanya kodi mara nyingi TRA wamekuwa wakitoa makadirio ya chini ili waweze kuyafikia na kupongzwa wakati kimsingi unakuta muda mwingi wanafanya propaganda. Kwa mfano
mtu anayepokea 1,000,000/= kodi ni laki 196,500/= (PAYEE) katika hali ya kawaida huu ni mshahara wa Mwalimu/Nesi lakini makampuni makubwa kama ya mawasiliano/Kuchimba madini/Kuchimba mafuta na gesi etc. yanapewa muda wa kutolipa kodi kabisa na baada ya muda huo kuisha kampuni husika inauzwa kwa mkoloni mwingine ambao kwa sasa tunawaita wawekezaji. Mfano ni majuzi tu Zain na Vodacom ziliuzwa TRA hawajatuambia TZ ilifaidi nini, na hawakotayari kuizungumzia hilo.
Katika maswala ya msingi kama haya TRA wako kimya, wana kigugumizi na jibu liko wazi ni ufisadi.

Leo hii utakuta kampuni kubwa ya madini au mawasiliano inapata faida kubwa lakini kodi inatoa kiduchu hatujui ni kwa nini.Lakini wanahangaika na mshahara kwa katibu mkuu wa CDM kwa nini?, mbona hawasemi wabunge walipe kodi kama njia ya kuongeza mapato? au wanasubiri CDM iwe na wabunge wengi ndio waje na hiyo hoja? Watanzania muda umefika wa kutumia nguvu ya umma katika kupinga hizi tasisi feki na viongozi wake.

Ukija kwenye PCCB, wako wepesi sana katika kubambikia watu kesi za rushwa hasa wale waliokuwa wanatofautiana na rais wa sasa, mfano ni Prof Mahalu, huyu bwana anaandamwa na mkuu wa kaya kwa chuki binafsi, kwani katika kutekeleza ununuzi wa ile nyumba JK alikuwepo from A to Z, hata bungeni alitetea taratibu zote zilifuatwa, sasa baada ya kuwa rais anamwandama ya nini kama si chuki binafsi?

Miaka miwili iliyopita serikali ya uingereza ili anza kufuatilia kshfa ya Rada, ambayo kampuni ya BAE iliiuzia TZ rada na watu wakapiga hela akiwemo Andrew Chenge. Idris Rashid na wengine, Serikali ya uingereza ikataka waTZ hao wachunguzwe ile hali na yenyewe iichunguze watu waliohusika kule kwao, huku kwetu zikaanza blaa blaa za kuwatetea hawa jamaa waliohusika na hata baada ya chenge kukutwa na karibi dola 1mil. huko nje bado kwa PCCB walikuwa hawaamini. Mpaka inafika mahali wanamsafisha huyu bwana mkubwa hadi sasa wanakataa kabisa kumchuguza huyu jamaa wakiwa hawaamini kama alihusika. Lakini lo wanakiri eti BAE iliibia serikali ila hawataki kuwachunguza wahusika.

Leo serikali ya uingereza imebaini kulikuwa na ufisadi na inataka kuleta fidia kwa watanzania eti anakuja mwendawazimu fulani, eti pesa hizo wapewe wao kwa sababu gani? Je wanakubali kwamba kuna ufisadi ulifanyika? na walichukua hatua gani?

Kama inawezekana pesa hizo zije zijenge hospitali moja kubwa hapa TZ na ujenzi huo usimamiwa na wananchi pamoja na serikali ya uingereza, kwani sisi hatuna serikali ila genge la wahuni/ mafisadi likiongozwa na fisadi namba moja.

Nakumbuka katika hili PCCB waliwasafisha watuhumiwa mara mbili au zaidi.


Watanzania tunaiunga mkono serikali ya Uingereza kuleta pesa hizo kwa njia nyingine na si kuwapa hili genge la mafisadi. Tunajua pesa za EPA zilirudishwa sasa ziko wapi? walio mjini wanasema zimepelekwa kijijini kwa wakulima na wakulima wanasema ziko mjini. ukweli kwama wajanja wamezilamba.
 
Umesema vema, Mkuu.

Tatizo vyombo vyetu hivi vina kashfa nyingi mno za kifisadi, takriban sawa tu na viongozi wa kisiasa hapa nchini. Ndiyo maana na wao wameamua kuwa politicians. Watu tunalalamika sana lakini wapi! Si JK wala mafisadi wenzake wanaoamini kwamba tumechoka kuibiwa kipumbavu kila siku tena na wezi waalewale na kwamba tunataka waache. Hawa "wakosa haya" wapo tayari kuliingiza taifa zima motoni lakini wao waendelee kula.

Wakati mwingine natamani kungekuwa na kitu mfano wa Al Qaeda kwa ajili ya kuwabana mafisadi tu, lakini unajua tatizo nini?.......Fedha!..fedha ngumu! Osama alifanikiwa kwa kuwa alikuwa nazo nyingi na walioamini katika falsafa yake walikuwa wanamchangia. Huwezi kuamini hapa kwetu watu wataniona mwehu hata kule kuwaza tu jambo hili lakini kila siku unakuta wanalalamikia ufisadi na wanaamini rais na matajiri waliomwajiri hawapo tayari kuacha wizi.

Mungu anisamehe. Ninavyokerwa na huu wizi, sihitaji hata kuaminishwa kwamba nikijitoa muhanga nitaenda peponi. Mie hata kama ni motoni potelea mbali ilimradi tu mafisadi waogope na kuacha ushenzi wao mara moja maana, hata tukijifanya kutochukua hatua bado tutateketea katika moto wa umasikini.
 
Back
Top Bottom