Kwa nini tovuti yangu haipati watembeleaji?

sele255

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
205
262
Habari wana jamii forums,
Hilo ni swali gumu kwa bloggers ambao ndio wanaanza.Unaweza kuuliza na kupata ushauri kwa watu lakini ushauri huo usikusaidie.Leo tuchambue jambo moja tu ,,,kuhusu hadhira unayoiandikia maudhui.,,,,

1.Lugha unayotumia
Je unatumia lugha ipi kufikiasha ujumbe kwa watembeleaji wako.Kama unatumia lugha ya kiingereza na unataka kupata watembeleaji wa tanzania tu ni jambo gumu.Sijamaanisha kwa watu wote wanaotumia lugha ya kiingereza tanzania hawapati watembeleaji .Unaweza kutumia lugha ya kiingereza na ukapta watembeleaji.Suala je ni watu wa aina gani unawalenga.Unaandika lugha ya kiingereza na ujumbe unataka uwafikie watu wasiojua kiingereza hapo hautoweza kupata watembeleaji.Andika mada za kiingereza kuwafikia watu wanaojua lugha hiyo.Vile vile unaweza kuandika lugha ya kiswahili ukakosa watembeleaji vile vile.Hapa inatokana kwamba mada inayoandikwa haiwasu walengwa.Andika mada husika iwafikie watu ambao ni walengwa.

2.Hadhira yako
Huwezi kuandika mada zinazohusu mambo ya vijana ukiwa na maana hiyo mada iwafikie watu wazima.Hapa utakuwa unaandika mada ambazo haziwahusu hadhira yako.Kama walengwa wa blog yako ni watu wazima andika mada zinazohusu watu wazima.Ukiwa na hadhira ya aina moja itakusaidia kupata watembeleaji ambao watakuwa hawapungui mara kwa mara.Vile vile itakusaidia kukuza idadi ya watembeleaji wako mara kwa mara.

3.Habari unayoandika.
Epuka ku-copy na ku-paste taarifa kutoka blog nyingine kwenda blog yako.Andika mada nzuri na bora ambayo haitopatikana katika blog yoyote ile.Hii itakuwezesha kukuza ubora wa blog yako kwa muda mfupi.

4.Andika mara kwa mara.
Ndio kabisa kuandika mara kwa mara kutakuwezesha kuongeza idadi ya keywords katika tovuti yako.Hii ndio siri bloggers wengi hawajui.Kwa hiyo.Utapokuwa unaandika mara kwa mara unaongeza maneno ambayo yatakusaidia kupatikana katika search results.Kinachofuata baada ya hapo ni kuongezeka kwa watembeleaji siku hadi siku.

5.Sehemu za kuandika comments
Ndio kabisa, unaweza kufikiaria ni utani kuhusu hili suala.Site yako ikiwa na comments za kutosha ambazo ni nzuri pamoja na reply kutoka kwako kwa kila comment inasaidia sana kukuza page rank ya tovuti yako na kukuwezesha kuongeza watembeleaji kwenye tovuti yako.



Kwa maswali na ushauri nakaribisaha........

From SEO service consultant
 
Back
Top Bottom