Kwa nini sikugombea uongozi 2010... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini sikugombea uongozi 2010...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ramos, Jul 29, 2010.

 1. R

  Ramos JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF, lengo la thread hii ni kuonyesha kuwa pamoja na kuwa wengi wetu tunaunga mkono mabadiliko, tena wengi ni watu wenye uzalendo 'kiasi' na kuipenda nchi yetu, bado kuna mambo yanayofanya uwanja wa kudai haki zetu usiwe flat.

  Nimejiuliza pamoja na kuwa ukiongea na wasomi wengi wanakuwa wana-support vyama vya upinzani, lakini ukiangalia mwaka huu ari ya kujitokeza kupitia vyama hivyo kugombea ni ndogo ukilingasha na wanaojitokeza kwenye CCM...

  Nimejaribu kuwaza sababu mbalimbali zinazotufanya 'tuogope' kugombea na vyama vya upinzani, lakini kabla sijamwambia mtu yeyote, nikagundua hata hapa JF waliojitangaza kugombea uongozi ni wachache, wakati naamini hapa kuna vichwa vizuri tu vya kuongoza.

  Hivi kama unadhani kuwa unaweza kuwa kiongozi wa kisiasa, lakini hujagombea, unafikiri nini kimekuzuia kufanya hivyo, na nini iwe suluhisho lake?
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,007
  Trophy Points: 280
  niko ughaibuni kwa hiyo siwezi kutelekeza majukumu ya Ubunge au udiwani nikiwa sipo huko ndo maana nawaunga mkono wagombeaji huko
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sikugombea kwa sababu ninafundisha watoto wadogo shuleni. Iwapo sote tutakuwa wanasiasa, ni nani atafundisha watoto wetu maadili ili waje kuwa viongozi wazuri baadaye? Najua kuna waalimu wenzangu wengi wamekimbilia siasa kwa kufuata masilahi, lakini naamini kuwa maslahi ya wanasiasa yatokanayo na kuwadhulumu wananchi ni laana mbaya sana, heri nibaki na faraja yangu itokanayo na kujua kuwa ninatenda mema
   
Loading...