lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,484
Wataalam na wajuzi wa mambo nijuzeni,ni kwa sababu gani serikali ya Tanganyika inaogopwa,hususani na watawala waliopo madarakani?
Kwa kifupi Tume ya Jaji Francis Nyalali ilipendekeza serikali 3,tume ya Jaji Kisanga ilipendekeza serikali3,tume ya Jaji Warioba imependekeza serikali 3.
Zote hizi mapendekezo yake yalikataliwa na watawala tena kwa kashfa na kejeli.mfano,Jaji Kisanga alishutumiwa na Mkapa sana kuhusu mapendekezo yake ya serikali tatu.
Kwa mtindo uleule naye Kikwete kamshutumu Jaji Warioba na kumzodoa kwa ujanja wa panya wa kuuma na kupuliza.Nashangaa sana licha ya tume hizi kukusanya maoni ya wananchi na sio maoni ya wakuu wa tume hizo.
Isitoshe iweje maoni yote ya tume yafanane tene kwa nyakati tofauti lakini wakuu bado hawakubali maoni ya wananchi.
Hii tume ya warioba iliundwa na makada madhubuti wa ccm.mfano mkubwa ni Warioba mwenyewe na Salim Ahmed salim,lakini bado CCM wa leo hawakuridhika.
Wajumbe hao wawili niliowataja warioba na salim wangekua hawajulikani imani zao ingesemwa wametumwa na wapinzani.Hayo ni machache kati ya mengi yanayonishangaza.kuna nini kati ya watawala na uwepo wa Tanganyika?