....Mkuu hili bado lina utata mkubwa sana hasa katika bulungutu la shilingi bilioni 95 ambayo Dowans inastahili kulipwa na TANESCO. Pesa hii ilitakiwa kulipwa tangu December, 2010 na ilishafagiliwa kwamba ilipwe na akina Msanii Kikwete, Pinda, Ngeleja, Mwanaheria Mkuu wa Serikali na inasemekana hata magamba walifanya kikao na kuridhia kwamba Dowans/Richmond wanastahili kulipwa bulungutu lao la shilingi 95 billioni plus accumulated interest.
Watanzania tukaja juu na kupinga kwa kila hali kulipwa malipo hayo ya kifisadi kwa kuwa hakukuwepo na mantiki yoyote ile ya kulipwa hasa ukitilia maanani kwamba Dowans ni kampuni ya kitapeli ambayo haikuwa na HQ Texas kama ilivyodaiwa na fisadi Rostam ilishindwa kutumiza masharti ya mkataba wake wa kufua umeme wakati nchi ilipokuwa gizani. Kesi bado iko mahakamani na natumai kwamba shinikizo la Wabongo ndani na nje ya nchi litahakikisha mafisadi wa Dowans/Richmond hawalipwi hata senti moja ya mradi wa kifisadi ambao ulibarikiwa na msanii Kikwete na rafiki yake EL. Kwa maoni yangu ni ushindi wa aina yake kwa Watanzania kuweza kusimamisha malipo ambayo yalitakiwa yafanyike zaidi ya mwaka mmoja uliopita (December 2010).