Kwa nini ni ulaya Tu na sio bongo

Kwa nini ni ulaya Tu na sio bongo

Mbona bongo ipo hiyo huduma mfano mdogo hata mm nafanya hiyo kulipia kidogo kidogo ila sema kumuachia mtu aende na mali hapo ni utata kwa maana wezetu wanasystem nzuri ya kufatilia watu mfano mtu akienda labla na passport yake akachukua bidhaa kwako kitendo cha mshahara wake kutoka tu ww unapewa kiasi mlichokubaliana kabla hela yajaenda kwa muhusika mfano mlikubaliana kila mwezi mlipane 50K mshahara ukitoka tu wanakata juu kwa juu unapewa chako ila bongo hiyo system hakuna labla miaka ya mbele huko
 
Ulaya ununuzi wa vitu kuanzia simu ,magari wananunua kwa kulipia kidogo kidogo mpaka MTU wnamaliza na incase likatoka Toleo mfano jipya unafanya top-up je kwa nini kampuni za simu huku bongo haziwezi kufanya mpango huu na wakapata Faida kubwa Tu tatizo ni nini?
Bongo tayari wanafanya muda tu ( nadhani hakufuatilia au hauna taarifa ) hasa kwenye simu
Mitandao ya simu hufanya hvyo

Mfano
Kwa Sasa Airtel wanatoa hiyo hudama na ( hapo nyuma tigo pia walikuwa wanafanya )

Tatizo kwenye Airtel simu ya laki mbili ( 200k )dukani wao wanauza Kwa mfumo huo huo mpaka ukimaliza malipo inafika laki saba ( 700)

Iko hivi..

Kuna simu wanauza nadhani no infinix au tecno yenye ram 2 na rom 32, Kwa kuanzia unapeleka elfu 70, halafu unakuwa unafanya malipo ya shilingi 1750 Kwa siku mpaka siku 365/364 au ( 12,2500 ) Kwa wiki mpaka wiki 54 (12250×54=661,500 )


Hivyo bhas
Kwa upande was Airtel , simu ya laki mbili ( 200k ) wao Kwa mfumo was kudunduliza wanakuuzia Kwa approximately laki sita ( 600k )




KWA KUMALIZIA
IDEA YA AIRTEL NI NZURI ILA JINSI INAVYOFANYIKA NDIO IMEKAA VIBAYA KIDOGO


MAANA HAIWEZEKANI KITU CHA LAKI MBILI ( 200K ) WEWE UTAKE FAIDA YA LAKI NNE (400K )

HAIWEZEKANI
 
Back
Top Bottom