Ulaya ununuzi wa vitu kuanzia simu ,magari wananunua kwa kulipia kidogo kidogo mpaka MTU wnamaliza na incase likatoka Toleo mfano jipya unafanya top-up je kwa nini kampuni za simu huku bongo haziwezi kufanya mpango huu na wakapata Faida kubwa Tu tatizo ni nini?
Kuna vitu vya msingi ambavyo US na Europe vipo kwa ajili ya kumfuatilia mteja ambavyo Afrika hakuna!! Sio kwamba Ulaya na Marekani watu hawaingii mitini, hell no... wapo wanaoingia mitini; and back in the days miongoni mwa freelancing jobs nilizowahi kufanya ni pamoja na Skip Tracing!!
Skip tracing ni kufuatilia watu walio-default!! Mwingine akiona mambo magumu, anahama hadi state kwahiyo unaanza tracing kufahamu kahamia state ipi, mji upi, na address yake mpya ni ipi!!
Sasa Kibongo bongo, mtu hata credit card hana, physical address hazieleweki, hata utlity bills history huwezi kuzipata! On top of that, sidhani kama tuna mfumo mzuri wa credit bureau!!
Sasa mtu kama huyo akishaingia mitini sijui utamtolea wapi!
Back in the days nilidhani Kibongo bongo ni rahisi kufanya hivyo kwa wafanyakazi, especially wa serikali... and YES, possible lakini sitamsahau mtu mmoja ambae alikuwa mfanyakazi wa serikali kwa jina Mike!
Wakati huo nilikuwa kwenye benki moja, sasa jamaa kaja kuomba mkopo! Mwana alikuwa mshikaji ile mbaya, kwahiyo fasta fasta tukampa mkopo!!
Kilichonishangaza, baadae akatupigia simu mimi na washikaji wengine wawili pale benki, akatuomba tukakutane nae kwenye hotel moja hivi ufukweni!
Nilichukulia kawaida tu lakini kufika kule, kumbe jamaa katuita kula bata!! Pesa iliteketea ile mbaya but I wasn't comfortable at all. Siku mbili tatu baadae tunapata taarifa Richie kahamishiwa mkoa!!
Kumbe wakati anakuja benki alifahamu kwamba anahama jiji! Making things worse, wiki chache baadae tunaletewa taarifa kwamba Mike kafariki! Tukashangaa kulikoni.
Kumbe jamaa alikuwa na ngoma, ndo maana akaomba uhamisho kwenda mkoa wa kwao, na piaalifahamu kwamba hakuwa na muda mrefu duniani though usingeweza kumgundua kwamba anaumwa!!
Sasa hao ndo Waafrika... of course, hata Ulaya na America wapo wa aina hiyo lakini kule ni mifumo mizuri ya kuweza kuwafuatilia!!