Kwa nini magari mengi yana rangi ya silver?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,410
Reaction score
14,119
Nimefanya uchunguzi wa rangi za magari mengi yanayotembea barabarani.
Mengi ya magari hayo ya aina yote , karibu 40-60% ni rangi ya silver.
Nimejiuliza ni kwa nini?.
Wakuu mwenye jibu tafadhali.
 
Kama IST nadhani 90% ni rangi ya silver
 
Nimefanya uchunguzi wa rangi za magari mengi yanayotembea barabarani.
Mengi ya magari hayo ya aina yote , karibu 40-60% ni rangi ya silver.
Nimejiuliza ni kwa nini?.
Wakuu mwenye jibu tafadhali.

Kwani Mkuu labda ulitaka yawe na rangi gani?
 
Mkuu kaa barabarani muda wowote na yachunguze magari 100 yanayopita muda wowote.
We kwa muda gani na mikoa mingapi ulikaa barabarani na kutoa tathmini hiyo?
Au ulikaa barabara ya Msata-bagamoyo ile ambayo uliripoti hapa kuwa imepata nyufa kibao kabla ya uzinduzi?
 
mimi utafiti wangu umegundua matairi yote ni meusi.

1410115913969.jpg
 
Mi utafiti wangu nimegundua hauwezi kula karanga huku ukila mua!
 
1. Magari meusi si salama sana maana hayaonekani barabarani yanafanana na lami. (Yanavutia kwa mtazamo lakini sio salama)

2. Magari mekundu yanamtazamo wa kinadharia kwamba nyekundu ni rangi ya hatari, yaani inatisha kwa waliowengi.

3. Magari ya blue, kiasi yanavutia lakini kwa rangi ilopakwa kwa ustadi mkuu

4. Magari meupe yanavutia na kiusalama nimazuri sana, lakini dosari kidogo ya rangi inachafua taswira na muonekano wa gari

5. Magari ya rangi ya silver

-Kiusalama, yanaonekana vema barabarani, inakaribiana na nyeupe.

-Haichomi macho, wala kutisha kama ilivyo red

-Gari ikisafiri hata barabara ya vumbi bado itaonekana vizuri kuliko nyeupe yaani inaficha uchakavu hata uchafu.

Rangi zingine bado kushindana na silver nivigumu sana, maana silver inabeba hata wapenzi wa gari nyeupe, samawati na pink.
 
Naona the most comprehensive anwer so far!
 
mimi ni megundua rim nyingi ni za silver
 
Nimebaini gari nyingi sasa hivi ni automatic sio manual.
 
Mimi nimegungua Mara nyingi magari huenda mbele na Mara cha he nyum

Nimegundua kuwa magari mabovu hupelekwa kwenye karakana

Nimedundua pia matairi yake huzunguka.

Nimegungua uskani wa gari upo mbele

Nimegungua mbele lazima kuwa na matairi mawili

Nimegundua kuwa magari mengi hutumia mafuta
 
Back
Top Bottom