Nimebarikiwa sana na ujumbe huu kwa kuanza nao kazi siku ya leo... Nashukuru sana.
Ukisamehe, unajiweka huru.... Hivi kweli ni nani kati yetu hajawahi kumkosea mwenzie au kumkosea Mungu? Iweje Mungu aliyekuumba anakusamehe unapomkosea, wewe ushindwe kumsamehe mwenzio? Mungu awabariki sana mtakaosoma thread hii.
"Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11:25,26)