Kwa nini kusamehe ni muhimu?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,133
Kwa nini kusamehe ni muhimu?

Kusaheme ni vizuri sana kwa moyon wako.
Kusaheme kuna uhusiano mkubwa na Blood pressure (BP) pamoja na kupunguza Stress hivyo kusamahe huweza kukupa faida kubwa sana kwa afya yako ya moyo.

Pia kusaheme kuna matokeo postitive na dalili za kimwili kiafya, dawa unazotumia (medication), kiwango cha usingizi, kuchoka na kulalamika.

Hii ina maana kwamba mtu asiyesamahe hupata matokeo negative kwa yaliyotajwa hapo juu.
Kusamahe huimarisha mahusiano na urafiki.

Kusamahe huimarisha roho ya kujitolea (volunteerism) na kuwa watoaji katika jamii.
Kusahamehe hupunguza uadui.
Kusamahe ni njia nzuri ya kujilinda na hasira.
Kusamehe hukuongezea kiroho chako na kujisikia vizuri mbele za Mungu
Kusamahe huimarisha saikolojia yako
Kusamehe hupunguza maumivu sugu
Kusamehe ni kukaribisha uponyaji wa mwili na roho

Forgiveness is choosing to love. It is the first skill of self-giving love.

Kusaheme ni kitu kizuri sana kwa mwili wako, mahusiano yako na mahali ulipo duniani hivyo achana na hasira za kutosamehe na badala yake samahe ili ufanye dunia mahali bora kuishi.

Wapo watu ambao husema anasamehe lakini hasahau, ukweli hasara ya kutosamehe ni kubwa sana kwa anayetakiwa kusamehe kuliko anayesamehewa.

In the Bible it says they asked Jesus how many times you should forgive, and he said 70 times 7.
Well, I want you all to know that I'm keeping a chart.
(Hillary Rodham Clinton)
 
Nimebarikiwa sana na ujumbe huu kwa kuanza nao kazi siku ya leo... Nashukuru sana.
Ukisamehe, unajiweka huru.... Hivi kweli ni nani kati yetu hajawahi kumkosea mwenzie au kumkosea Mungu? Iweje Mungu aliyekuumba anakusamehe unapomkosea, wewe ushindwe kumsamehe mwenzio? Mungu awabariki sana mtakaosoma thread hii.

"Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Marko 11:25,26)
 
Kwa nini kusamehe ni muhimu?


Wapo watu ambao husema anasamehe lakini hasahau, ukweli hasara ya kutosamehe ni kubwa sana kwa anayetakiwa kusamehe kuliko anayesamehewa.


Asante kwa somo zuri, ubarikiwe
Ni kweli kabisa yaani, unaposhikilia kutokusamehe unaumia wewe badala ya wenzio:
Mungu hakusamehi dhambi zako
Unajenga chuki, hasira na visasi kwa mtendaji ambavyo vitakuletea msongo wa mawazo
Unapata huzuni kila unapokumbuka hicho usichosamehe...nk
Kweli tuache kujihesabia haki, hakuna mwema ila Mungu pekee.
 
Hakika somo ni zuri ajabu, ila wakuu kuna kipindi mambo yanakuwa magumu sana, unasamehe na jamaa anarudia ishu ile ile kesho yake!
 
Hakika somo ni zuri ajabu, ila wakuu kuna kipindi mambo yanakuwa magumu sana, unasamehe na jamaa anarudia ishu ile ile kesho yake!

Sokwe wa town,
Kumbuka Yesu alisema samehe hata 7x70. just imagine, unatakiwa kusamehe hata kama mtu amekukosea mara 490!! What a wonderful message from Jesus!!
 
Naipenda hii quote kutoka kwa Buswelu:
"The happiness you get from being able to forgive someone is beyond any apology"
 
Kusamehe kunakufanya uwe na mwelekeo mzuri na mipangilio mizuri katika maisha yako
Kusamehe kunaongeza siku za kuishi
Kusamehe kunafanya chachu za mwili zitengame kwa hivyo kupunguza maradhi(Hormones)
Kusamehe kunakufariji mwenyewe kwani kunakufanya ujione mtu mwenye maamuzi
kusamehe kunadumisha heshima
kusamehe ni njia nzuri ya kujua kinachofuatia
kusamehe ni uwanja mpana ni pamoja na kujisamehe mwenyewe katika mambo uiyowahi kuyafanya ya kakudharilisha katika jamii lakini baada ya kujisamehe ukabadili tabia na kuanza upya
 
Kusamehe ni muhimu sana katika maisha ya kila siku,na siku zote ni muhimu kujifunza kusamehe na kusahau kabisa.
 
Asanteni wanajamvi kwa ujumla ,HAYA yoote siyo mara ya kwanza kuyasikia au kuyasoma
ila moyo wa binanamu huwa unapata kutu usipopata mawaidha mazuri kama haya hivyo likikupata la kukupata unachowaza ni kulipa kisasi ,ninashukuru kwa kukumbushwa umuhimu wa kusamehe zaidi na zaidi na kweli hii ni dawa kwani baada tu ya kuusoma ujumbe na kutafakari na kuamua kusamehe na kumuomba mungu anisamehe na mimi nasikia mwili kuwa mwepesi na kwamba kuna mzigo usioonekana unaushusha immediately unapoamua kwa dhati kusamehe.
IT IS EXPERIENCED THAT PEOPLE PERISH BY THE VERY MEANS THEY USE TO DESTROY OTHERS
 
kweli hii ni dawa kwani baada tu ya kuusoma ujumbe na kutafakari na kuamua kusamehe na kumuomba mungu anisamehe

NA IWE HIVYO MILLELE IN JESUS NAME
 
Back
Top Bottom