Kwa nini katiba Tanzania ya 1984 haifai? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini katiba Tanzania ya 1984 haifai?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Shadow, Mar 2, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ndugu wanabaraza,

  Kumekuwa na michango mbali mbali kuhusiana na hili suala la katiba ya Tanzania ya Mwaka 1984 kuwa na mapungufu makubwa. Kulingana hayo na ukiangalia watanzania toka uhuru hawajawahi kutengeneza katiba yao. Napenda kuwakaribisha katika mtiririko huu wa mawazo(thread) hili tuweze kuchanganua katiba yetu ni kwa nini haifai na vigezo vipi vinatufanya tuione haifai. Katika kuichambua naomba tutumie mifano hai na si hadithi za kufikirika. Mwisho kama tutaweza kupata hitimisho la nini kifanyike baada ya huu mchanganue.

  Kumbuka katiba ndio sheria mama ya nchi yetu. Sheria zote zinatakiwa kuahakisi sheria hii mama( kind of mirror image reflection).

  Karibuni.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Acha porojo, hakuna Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1984. Kafanye homework yako vizuri ujue kwanza Katiba ilitungwa lini na kama kuna mapungufu uyataje ni yapi ili tuyajadili. Acha hearsay kutoka kwa wanasiasa ambao wanapenda kuwatapeli wananchi. Na kama watanzania hawajawahi kutengeneza Katiba yao ilitengenezwa na nani? Kwani utaratibu wa kutengeneza Katiba ukoje kwa mawazo yako? Kuwa specific ili mjadala nao uwe specific.
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hii haijakaa vizuri kabisa Hiyo bold inaonesha kuwa uliyoandika sio sahihi in material aspects.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi naona labda alikuwa anazungumzia
  KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
  TANZANIA YA MWAKA 1977.
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hamna katiba ya Mwaka 1984.Namuunga mkono mchangia mada wa kwanza katika hii thread.
  Mwaka 1984,kilichotokea ni badiliko muhimu sana katika historia ya katiba yetu ambayo ni inclusion of the Bill of Rights in our Constitution since its rejecton from the Indepence Constitution.
  Na siyo kweli kwamba Watanzania hawajawahi kutengeneza Katiba yao,tumetengeneza Katiba zetu kuanzia ile ya Uhuru iliyokuwa ya Kikoloni zaidi,The Republican Constitution ya 1962,ya Interim ya Mwaka 1965 na ile ya 1977
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Sep 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama alikuwa anamaanisha hivyo aseme na kama alikuwa anamaanisha Katiba ya Zanzibar, 1984, nako aseme, pia atoe mapungufu anayodai yapo ili tuyajadili!
   
  Last edited: Sep 22, 2009
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .

  Acha ujinga huo. Zanzibar imetokea wapi hapa.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sio ujinga Katiba ya Zanzibar ndiyo ya mwaka 1984 na sio ya Tanzania ambayo ni ya mwaka 1977. Sio ustaarabu kutumia lugha chafu wakati tunajadili, mambo hayo hayana nafasi hapa JF!
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kevo unauhakika na hiyo maneno yako niliyo red.

  Je unafahamu procedure za kuandika katiba mpya? Je unafahamu kuwa lazima kue kushirikisha wananchi, wanataaluma, NGO's, mashirika ya dini katika mchakato mzima.

  Hakika Tz toli copy na paste kutoka katiba ya wakoloni. Ndio maana kuna sheria nyingine unaona wazi zimepitwa kabisa na wakati .
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Sep 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo mapungufu ni yapi kama yapo tuyajadili? Ni hilo tu la copy and paste kama unavyodai? Ningependa kama mtu ataonyesha mapungufu katika Ibara fulani au Sura fulani, mjadala ungekuwa mzuri kwa sababu kama Ibara fulani imekuwa copied and pasted lakini ikawa haina mapungufu sioni kama ni tatizo. Vilevile vitu vingine kama Bill of Rights ni rahisi kuwa copied and pasted kwa sababu ni suala la kimataifa hasa kutokana na Tangazo la Haki za Binadamu la UN, 1948 ambapo hiyo Bill of Rights ilikuja kuingizwa kwenye katiba yetu mwaka 1984! All in all nakubaliana na wewe kwamba ni jambo jema kuwa na referendum (ili kupata maoni ya wananchi) ili kuandika Katiba mpya!
   
 12. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nazifahamu na kuna moja ya threads nimeshawahi kuzi-outline!

  Sasa,suala linapokuja hata kama hao stakeholders hawajashirikishwa,kwani watu 20 au 200 walikuwa ni wakoloni ama watanzania?????????

  Katiba ya 1977,proposals zilijadiliwa na a constitutional committee ya watu 20 chini ya Uenyekiti wa Thabit kombo na Secretary wake Pius Msekwa,hawa walikuwa wakoloni???????????

  Ilipitishwa na constituents assembly ya zaidi ya watu 150,hawa walikuwa wakoloni???????????

  Akina Nyerere wakati wana-adopt katiba ya Uhuru pale karimjee hadi kukataa kuweka bill of rights kwenye katiba,hawa walikuwa wakoloni?????????

  Naomba unipe list ya hizo sheria za wakolon tulizo copy na ku paste kutoka kwa wakoloni zinazo-exist mpaka leo!
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Labda nianze kuzibainisha baadhi tu.

  1.Sheria ya ndoa ya 1972.
  2.Sheria ya Sifa za Rais No 4 ya mwaka 1992, No 13 na 16 ya mwaka 1994 na ile No ib 7 ya mwaka 2000.
  3.Sifa za mtu kuwa Mbunge Sheria ya 1984 Na.15 ib.13
  Sheria ya 1992 Na.4 ib.19
  Sheria ya 1994 Na.34 ib.13
  4. Utaratibu wa uchaguzi wa wabunge wa majimbo ya uchaguzi
  Sheria ya 1992 Na.4 ib. 25

  Sheria ya 1995 Na.12 ib.10
  Sheria ya 2000 Na.3 ib.12​
  5. Sheria za uanzishwaji a Serikali za mitaa na chaguzi zake.

  Zipo nyingi nyingi labda nitulie kidogo naweza kuziweka hadharani.

  Nasriyah Saleh Al-Nahdi.
  Doha
   
 14. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuziainisha haitoshi tuu tuonyeshe na kasoro zake!
  Na hizi sheria zina uhusiano gani na katiba unayodai tuli-kopi and paste?
  katiba ni tofauti kabisa na hizi sheria.Na mjdala uliopo hapa ni wa Katiba inayodaiwa ni ya mwaka '1984'
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pole sana. Kwa heri.
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Oct 6, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Barux2 kusema sheria fulani ina mapungufu (of course hapa tunataka Ibara pekee za Katiba inayodaiwa ya mwaka 1984! au constitutional Acts zilizo-enact Ibara hizo) bila kuyataja mapungufu hayo uko serious kweli na mjadala huu? Kaaazi kweli kweli!
   
Loading...