Huwajui polisi! Mi nilishuhudia RPC mmoja akizungumza na mwenyekiti mmoja wa chama cha upinzani na kila mara alikuwa akimjibu huyo mwenyekiti na kutumia neno 'afande'. Nikashangaa sana, baadae nikamwomba askari mwingine ofisa mdogo anifafanulie kwa nini bosi wake alikuwa anamwita mwanasiasa yule 'afande'. Nikajibiwa kuwa hata wao polisi huwa hawajui baadhi ya wanasiasa wako upande gani, kwa hiyo kujihakikishia uhakika wa ulaji wake, anatoa heshima za jumla kuwa naye ni 'afande'.
Kwa kifupi huyo OCD alimwogopa huyo mgombea. Na si huyo tu anayeogopwa. Kuna wafanyabiashara wanaogopwa sana, wengine majambazi wanajulikana lakini polisi wanawaogopa vibaya!