Kwa nini IGP hasemi lolote juu ya kipigo cha OCD Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini IGP hasemi lolote juu ya kipigo cha OCD Nzega

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Oct 29, 2010.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Tukio hili nalilinganisha na jinsi mkuu wa Wilaya alivyo wachapa viboko waalimu huko Bukoba. Tofauti ni kwamba waalimu walichapwa kwa usimamizi wa askari. Huyu OCD ni kwa upuuzi wake tu maana kila mtu pale kituoni alikuwa chini ya amri yake. Alishindwa kutumia amri yake.

  Najua ni matokeo ya kudhani wateule wote wako chini ya chama na siyo serikali. Lakini lazima IGP alinde heshima ya Jeshi kama Chama kilivyolinda heshima ya waalimu.

  IGP yuko wapi au ndo ushemeji wa kipuuzi na kutojua thamani ya jeshi.
   
 2. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nzega au Maswa? Sisi tunajua wa Maswa
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chama ndicho kilimpa ajira mkuu umesahau?
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  IGP ni mteule mwaminifu wa rais aliyeko madarakani na si kwa ajili ya katiba
  wanajisahau sana hawa miamba wa majeshi yetu
   
 5. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Acha wapigwe maana ndio wanalinda mfumo uliopo. Safi sana!
   
 6. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Huwajui polisi! Mi nilishuhudia RPC mmoja akizungumza na mwenyekiti mmoja wa chama cha upinzani na kila mara alikuwa akimjibu huyo mwenyekiti na kutumia neno 'afande'. Nikashangaa sana, baadae nikamwomba askari mwingine ofisa mdogo anifafanulie kwa nini bosi wake alikuwa anamwita mwanasiasa yule 'afande'. Nikajibiwa kuwa hata wao polisi huwa hawajui baadhi ya wanasiasa wako upande gani, kwa hiyo kujihakikishia uhakika wa ulaji wake, anatoa heshima za jumla kuwa naye ni 'afande'.

  Kwa kifupi huyo OCD alimwogopa huyo mgombea. Na si huyo tu anayeogopwa. Kuna wafanyabiashara wanaogopwa sana, wengine majambazi wanajulikana lakini polisi wanawaogopa vibaya!
   
Loading...