kwa nini hawa wazee wasipimwe akili???...

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
Zitto awagonganisha wazee Kigoma, Geita




Na Renatus Masuguliko



19th April 2010








headline_bullet.jpg
Wavutana kwa zaidi ya saa saa saba
headline_bullet.jpg
Kigoma wawataka Geita wasubiri miaka mitano
headline_bullet.jpg
Wamfananisha Zitto na dume la mbegu



Zitto%20K(4).jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.



[FONT=Helvetica, sans-serif]Kauli ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, juu ya jimbo atakalogombea ubunge ndiyo itakayotegua kitendawili hicho baada ya wazee wa Kigoma na Geita kuvutana kwa zaidi ya saa saba katika kikao kilichomalizika bila kufikia mwafaka.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jumamosi, wazee wa Kigoma waliutaka ujumbe kutoka Geita kuwa na subira kwa kuwa bado wanamuhitaji mbunge huyo kijana kuendelea kuwatumikia. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Kikao hicho kilifanyika katika kijiji cha Mwandiga nyumbani kwa Zitto, takribani kilomita 20 kutoka Kigoma mjini. Ujumbe wa wazee wa Kigoma uliongozwa na Mwenyekiti Baraza la wazee wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kigoma, Ramadhani Mengi. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Wawakilishi wa familia ya Zitto pia walihudhuria mkutano huo, ingawa Zitto mwenyewe hakuwapo.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Kikao hicho kilichotawaliwa na mvutano wa hoja kali na nzito kutoka kila upande, kilianza kwa hoja iliyowasilishwa na kiongozi wa ujumbe wa kutoka Geita, Mabula Kachoji, aliyeanza kwa kujitambulisha na kisha kuweka wazi kuwa ujio wao ulikuwa na lengo la kuomba Zitto akagombee ubunge katika jimbo lao katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Baadhi ya hoja zilizowasilishwa na ujumbe kutoka Geita ni kwamba kwa mujibu wa mila na desturi za Kisukuma, sio kosa wala aibu kuazima dume kutoka kwa jirani ikibainika kuwa linafaa na ndicho kinachofanyika sasa kwa Zitto kuombwa kwenda kugombea Geita.[/FONT]
“[FONT=Helvetica, sans-serif]Sisi tupo hapa kwa maslahi ya wana- Geita na siyo kwa maslahi ya kisiasa kwa sababu Geita tunahitaji mwakilishi mwenye nguvu, ujasiri, mchapakazi, anayeheshimu wapiga kura wake, msikivu, mtiifu na [/FONT][FONT=Helvetica, sans-serif]anayewashirikisha wapigakura kujiletea maendeleo na kutaua kero zao; kwetu Geita kwa miaka zaidi ya kumi hilo halipo,” alisema Kachoji. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Kiongozi huyo wa ujumbe kutoka Geita, alisema kutokana na baadhi ya sifa zilizotajwa ndiyo sababu walifikia uamuzi wa kwenda kumuomba Zitto aende kuwatumikia Geita na kwamba hatua hiyo inatokana na kauli yake ya Machi 28 alipokuwa Geita kuweka wazi kuwa yuko tayari kugombea katika jimbo hilo ikiwa wazee wake watamruhusu.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Mara baada ya utangulizi huo, ilifuata ibada maalum kuombea mazungumzo hayo ambayo iliongozwa na Mchungaji Eliasi Kazimili wa Kanisa la African Brotherhood Church (ABC) aliyekuwa miongoni mwa wajumbe saba kutoka Geita.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Mchungaji Kazimili anatoka katika tarafa anayotoka mbunge wa sasa wa Geita, Ernest Mabina. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Katika maombi yake Mchungaji huyo alimfananisha Zitto Kabwe na mkombozi aliyetumwa kuwaokoa wana wa Israel waliokuwa wanateseka utumwani katika nchi ya Misri.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Alisema anamuona Zitto kama hastahili kuwepo Kigoma tu isipokuwa katika sehemu yoyote kunakohitajika ukombozi. [/FONT]
“[FONT=Helvetica, sans-serif]Ndugu zanguni najua baadhi mtashangaa kuwa imekuwaje kwa kiongozi wa dini kama mimi kuwa katika ujumbe huu, napenda kuwathibitishia kuwa hii ni ishara ya matumaini kuwa kijana wenu anahitajika Geita na mimi ni mchungaji wa kondoo ambao ni wanadamu na siyo wa miti,” alisema Mchungaji Kazimili katika maombi yake. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Baada ta hapo, hoja zilianza kutolewa na kisha kujibiwa na upande wa pili kwa nyakati tofauti.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Mjadala huo ulitawaliwa na jazba kila upande ukitetea hoja kuhusu uhalali na haki ya kumsimamisha Zitto katika uchaguzi wa Oktoba. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Hata hivyo, baada ya mvutano mrefu na mkali, Mwenyekiti ujumbe wa Kigoma, Mengi alisimama na kuhitimisha mjadala huo kwa kusema kuwa kwao hawako tayari kumwachia Zitto kwenda Kugombea Geita.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Hata hivyo Mengi alisema kitakachosubiriwa ni kauli ya mwisho ya Zitto baada ya kurejea kutoka katika mkutano wa 19 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.[/FONT]
“[FONT=Helvetica, sans-serif]Kwa msimamo wetu sisi wazee wa Kigoma jimbo la Kaskazini, tunawaomba watu wa Geita kuwa na subira walau ya miaka mitano ili walau amalizie kazi iliyobakia kwa miaka mitano. Tumeshuhudia mabadiliko makubwa Kigoma, tumepata lami, huduma za nishati na umeme vimeboreka, maji na nyinginezo sasa akitutoka tena tutakuwa watu wa nani,” alihoji mzee Mengi.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Hata hivyo, alisisitiza kuwa hatima ya wapi atagombea itatokana na kauli itakayotolewa na Zitto mwenyewe.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Wazee wa Geita waliondoka Kigoma jana asubuhi kurejea kwao na kusubiri tamko ambalo litatolewa na Zitto kutokea kijijini kwake Mwandiga.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Nipashe jana ilizungumza na Zitto jana mjini Dodoma anakohudhuria mkutano wa Bunge ili kupata kauli yake juu ya mkutano wa wazee wa Kigoma Kaskazini na Geita, lakini alisema hajapata taarifa rasmi za kilichoamuliwa katika mkutano wa wazee hao.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Kwa matokeo ya mkutano wa wazee hao, sasa Zitto atawajibika kutii kauli ya wazee wa Kigoma Kaskazini kama alivyosema mwenyewe kwenye mkutano wa hadhara Geita kwamba alikuwa akisubiri kauli yao.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Zitto amepata umarufu mkubwa nchini kutokana na kuendesha harakati za kutetea haki ya wananchi kunufaika na rasilimali ya madini. [/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Ni kutokana na harakati hizo, Zitto alisimamisha ubunge kwa miezi kadhaa kutokana na kuwasilisha bungeni hoja binafsi juu ya kusainiwa ughaibuni mkataba wa mgodi wa Buzwagi baina ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na kampuni ya madini ya Barrick.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Mkataba huo wa kuchimba dhahabu ulisababisha Zitto na chama chake kuanzisha harakati za kisiasa walizozipachina jina la ‘operesheni sangara’ kuhamasisha wananchi kudai kunufaika na rasilimali za taifa.[/FONT]
[FONT=Helvetica, sans-serif]Geita ni miongoni mwa maeneo ambayo dhahabu inachimbwa kwa wingi nchini. [/FONT]




CHANZO: NIPASHE
 
bongo zao ziko vichwani kweli? mtu atoke kigoma aende Geita. Hawa wasukuma vipi?
 
Kwani Geita si Tanzanzania au mbona Kenja ni mbunge wa kinondoni je yeye ni mzaramo au,pamoja na kupiga kelele za ukabila bado watu wanauendeleza kwa kuleta hoja mbofumbofu,je kuna sheria inayosema kuwa ukitaka kugombea ubunge jimbo la kwa mfano Kyela lazima uwe mzaliwa wa kyela na uwe mwakyusa acheni hizo,mwache Zito akagombee ubunge Geita,kama atashinda au atashindwa yote ni matokeo
 
Kinachonifurahisha ni kwamba Tz ni nchi nzuri sana. Mtu anajisikia nyumbani mahali popote na kwamba anaweza kupata uongozi mahali popote. Kweli tuna sababu za kujivuna kwa hilo; kitu ambacho si rahisi popote Africa. Mungu ibariki Tanzania yetu.
 
hoja hapa si ukabila wala nyumbani ni nyumbani............... wangesema wameketisha zito kitako kumpa nasaha, kidogo ningeelewa.................. zito akiamua kwenda geita kugombea, kigoma watamtazama kwa jicho gani??................
 
hoja hapa si ukabila wala nyumbani ni nyumbani............... wangesema wameketisha zito kitako kumpa nasaha, kidogo ningeelewa.................. zito akiamua kwenda geita kugombea, kigoma watamtazama kwa jicho gani??................
Agombee Geita basi ashinde huko, akishindwa..........
 
Kama mmbunge wa Geita kwa sasa ni wa CCM na mimi nina political ambitions, ningeachana na majimbo ambayo yanahitaji fedha nyingi kugombea, nika kimbilia huku clearly mmbunge wao hawamtaki baadhi ya watu yaani its an open invitation.

You only need huyu Zitto endorsment ya kuwa huyu ni kama mimi mkimpa nafasi yaani inaonekana huko ana abudiwa kama kiongozi imara na amna better endorsment kama ya mtu waliempa trust. Nafunga mizigo yangu napeleka majeshi huko wana-chadema vijana opportunity goes to those who seek for it, and they dont present themselves openly like this one politically.

Hivi kwanini tunazani ni muhimu viongozi wa wenzetu coming election time wanatumia popular political figures in their campaigns Zitto si lazima aenda Geita lakini Chadema lazima waende na mgongo wa Zitto huko.
 
Back
Top Bottom