Kwa nini deni la Nyanza Lilipwe sasa na kwa hela ya walipa kodi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini deni la Nyanza Lilipwe sasa na kwa hela ya walipa kodi??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kujenda, Aug 25, 2010.

 1. K

  Kujenda New Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi ni mtanzania ambaye nimeona mnisaidie kwa hili, Kwenye kampeni ya CCM mwanza JK aliahidi kulipa madeni yote ya NYANZA... ambayo ni zaidi Tsh billion tano. kati ahadi hiyo alikiri yafuatayo

  Wabadhilifu ndio walioiua NYANZA na hivyo yeye atalipa deni hilo bila kusema kuwa walioiua nyanza atwafany nini, Je hii sio RUSHWA, na kama nakumbuka aliseme hilo halipo kwenye ilani ila atalibeba yeye.

  Sasa mimi nauliza hizo hela atazitoa wapi? je ni halili kulipa deni bila kuwatask wahalifu kwanza au ndo uwajibikaji huo?

  Inaniuma kwa sababu kuna watoto wanakaa chini, walimu hawana nyumba kwani japo asiwakumbuke hao lakini anataka kuwalinda wwezi,

  jamani mi naomba msaada wenu kwa hili, hivi hatuwezi kumshtaki na kuliwekwe kwenye agenda za kampeni watu makini walisimamie. kwa hili sina ugomvi na wakuli wa kanda ya ziwa, lakini hii sio Rushwa kweli?
   
 2. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 889
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hiyo moja kwa moja ni rushwa. Sijui akiambiwa KNCU, KCU, SHIRECU,....nk nao wanadaiwa, atawalipia?
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hizi ndizo siasa za kishenzi za CCM, siasa za kulinda wahalifu. Watu ambao wameingia mikataba ya kinyonyaji kwa kutumia NCU (1984) wapo na wanamali ambazo zingetumika kulipia fidia ya kufilisika kwa NCU (1984).
  Je wamechukuliwa hatua gani?? Na kwa nini jasho la masikini litumike kusafisha kinyesi cha walafi ambao sasa wapo kwenye siasa?????

  Naendelea kukasirika bora nisiendelee kuandika wasije waka deal na mimi
   
 4. b

  buckreef JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alichosema Kikwete ni hiki hapa chini, ni wazi mwanzilishi wa hii thread hujaandika ukweli:
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Je ni nani anawajibu wa kuhakikisha kuwa hawa wezi ambao wameifikisha hapo Nyanza ni nani? Je kama walioiba hawakuwajibishwa watakaokuja hawatafuata nyayo za watangulizi wao?
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yes -- ni kulinda mafisadi tu. Kwani tumesahau hiki ni Chama cha Mafisadi (CCM)?
   
 7. I

  Igembe Nsabo Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kila mtu anafahamu kuwa Mhe. na watu wake wametufanya sie wananchi kama tu Mapuguwani na hatuna akiri, Jana hata mie nimesikia akisema watu wa BUKOBA wakimchagua atawanunulia Meli Kubwa kuliko hata MV BUKOBA au sawa na MV BUKUBA, Pia wasukuma atawanunulia KIVUKO KIKUBWA pale KIGONGO - BUSISI, atawaletea UMEME, atawajengea Barabara!!!!! na mambo kibao!!!!. Mimi nasema zile Bara bara za Singida - Manyoni, Mtwara - Lindi ( Nangurukuru) ambazo ziliachwa na Mhe Ben Mkapa vikiwa ni vipande vya Kilomita kama 60 hivi vimechukua miaka yote ya utawala wake!!!!!.Mimi nafikiri asitutukane kwa kutudanganya na ahadi za kipuuziii, angekuwa anasema nini atafanya tuondokane na utengemezi wa kusubiri Budget support kutoka kwa WAHISANI, ataongezaje mapato, Suala la UFISADI atapambana nalo vipi???, Atapuguzaje matumizi ya Serikali yake yale ambayo hayana TIJA kwa kuangalia ukubwa wa Serikali, uedeshaji wa Mashangingi, Safari zake za nje ya nchi zisizo na tija na .......! Haya ndio mambo aliyotakiwa kutuambia lakini sio kutupa ahadi za kipuuziii ambazo hazitekelezeki...utanunua meli kwa pesa zipi kama hukusanyi kodi??? utajengaje barabara kama matumizi ya Serikali yake ni makubwa kuliko makusanyo ya kodi???.Jamani nchi hii tunahitaji mabadiliko ya kweli, tunahitaji watu wenye udhubutu wa kutenda ili tuwe nchi ya mfano, na wakati ni huu.Kuna email imekuwa ikisambazwa naombeni iwafikie wanachi wote mie imegoma tu ningewawekea hapa hizo slide zake! mkaona wenyewe ( kwa kifupi kuna fundi viatu yupo amelala chini ya mti na Bango la &quot;Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya&quot;, ingine kuna watoto wa shule moja huko vijijini wamekaa juu ya mawe na shule yao ni ya majani iko wazi sehemu zote, ingine imeonyesha jengo la BUNGE DODOMA na mwisho imeonyesha Gazeti la RAI likiwa na zile POSHO ZA WAHESHIMIWA ukianzia na Mafuta lita 1,000 @ 2,500/=, kikao kwa siku Tsh. 100,000/=, Dereva Tsh. 400,000/= @ mwezi, Jimbo Tsh. 450,000/=@mwezi, Ukarabati wa gari Tsh. 1,000,000@mwezi na......inakadiriwa kufikia Tsh. 6.9milioni@mwezi.). Haya ndo tulitakiwa kuwaambia wananchi, nani anayetaka kwenda kuwa Daktari Mwananyamala kusaidia akina mama wanaojifungua na ambao wanalala kitanda kimoja watu watatu na watoto wao - wagonjwa!!!! nani anataka kwenda OCEAN ROAD Hospital kutibu wagonjwa wa Cancer??? si ni bora nikawa Mbunge ili nami nipate allowance kama hizo na kuwa waziri wa Serikali ya JK!!! na hapo sasa nchi hakuna Mchumi wala Engineer anayeweza kufanya kazi kwa moyo wote isipokuwa ubabaishaji tu!!!!. Nani akae kwa TGS.... na kama sio kusubiri kuwa na vikao hewa au safari hewa???</p>
   
 8. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,265
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Uongo mwingine wa CCM meli sijui kivuko tangu mv bkb ilipozama mpaka leo ilitakiwa wawe washanunua nyingine pamoja na vivuko sasa kama muda wote wameshindwa wataweza sasa?bara bara karibu zote zilizojengwa ni miradi ya mkapa au mwinyi yeye miaka mitano iliyopita kafanya nini?
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,770
  Likes Received: 915
  Trophy Points: 280
  Wacha kutusanifu wewe, fweza alizojichotea kwenye share zake za Barrick ni wizi ndio sababu haya makampuni ya uchimbaji yanafanya yanavyotaka hakuna rais aliyekubuhu Ufisadi kama huyu na siku yake inakuja.
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,969
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Vyama vyote vilivyo katika matatizo nchi nzima atalipa madeni yao na kuwapa mtaji wa kuanza upya.
   
 11. A

  August JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,175
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Sio kwamba atawalipia ni si ndio tutalipa kwa kutuzidishia kodi au kutunyima huduma flani, kwa hiyo kwa maneno mengine anataka kuchukua hela yetu bila ridha yetu ili afanye yeye anachokiona kinafaa kwetu.
  kwa hiyo ni juu yetu kukubali au kukataa hela yetu isitumike namna hiyo kwa kutoipigia kula ccm
   
 12. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naomba watanzania wengi iwezekanavyo wapata kuuliza maswali haya ya msingi, tusikubali kudanganywa kama majuha!!! Nitafanya hivi mie, nitaweka hiki mie, nitawapatia hiki mie, wasanii wa Tanzania watakuwa kama Beyonce.... real? How? Mbona hata dalili hatujaziona katika miaka mitano unayomaliza??
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,622
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Hapa ni JK muasisi wa rushwa akitoa rushwa.

  Tena anatoa rushwa kwa pesa waliokwiba wao.
   
Loading...