Elections 2010 Kwa nini CUF wanaukimbia uwanja wa Jangwani?

Kitu cha msingi ni kuleta ushindani mkubwa kwa chama cha ccm na kukiondoa madarakani bila kujali itikadi ya vyama.
Kama unadhani cuf wanafaa basi piga kura ya NDIYO kwa CUF.Kama unaona CHADEMA inafaa basi piga kura ya NDIYO.
Hii ndiyo Demokrasia tunayoipigia makelele na elimu ya uraia ambayo ni haba sana kwa watanzania walio wengi.
MYTAKE:

  • Tuwashauri ndugu zetu kujua haki na wajibu wa kupiga kura kuchagua viongozi,na sio kuishia kulalamika kila kukicha.
  • Tuwafundishe watoto wetu kwenye vyuo vya uandishi wa habari waache kulalamika kila kukicha kuwa wanaonewa na hawapewi haki ya kupata habari.
  • Tuwaeleze ndugu zetu athari za kupewa rushwa ya uchaguzi 2000 na baada ya uchaguzi unairudisha bila wewe kujua.
  • Mbona Tanzania kuna wasomi vijana wengi tuu wanatoka vijijini?hawaoni hili?viongozi wote wanaoshabikia ccm leo walisoma bure,iweje leo watuambie tulipie pesa nyingi hivyo?AMUA SASA.
I like your comments
 


Hii pia inaongeza ile hoja kwamba CUF ni chama cha Kiisilamu. Halafu kama ulichunguza sana picha za magazeti zilizoonyesha mkutano huo na ule wa Chadema kule jangwani siku ya pili yake – utaona ule wa CUF wahudhriaji weni walikuwa wamevalia baraghashia kuliko ule wa Chadema. Ziangalieni hizo picha tena.



Mimi sasa nimeshindwa uvumilivu wa hili ni bora basi muwaeleze waislamu hawatakiwi kushiriki siasa kwenye nchi hii. Kumbuka hata hao walioleta uhuru wa nchi hii ni waislam angalieni hoja kama udhaifu wa viongozi na sera zao suala la wanachama wa chama fulani ni wachagga, wasukuma au wakristo hailitasaidia kitu mimi mbona nashabikia Chadema na mie sio mkristo wala mchagga? acheni kuwa na akili finyu mie nadhani Makamba alikusudia watu kama nyie ndio wenye akili ndongo sio kina marando...... Tafakari
 
Hili Rev. Masanilo ni chakula cha mapadri kwa muda mrefu tu ndiyo maana lina-act namna hiyo.

Wavaa vibarakashia wanahudhuria mikutano ya kisiasa tokea enzi za TANU wakati huo hata Mbezi na Kimara ni pori tu. Nenda kapekua picha za enzi hizo na mtuwekee hapa.


Madrasa al sul
 
CUF ni chama cha wapemba ndiyo maana huku bara watu wenye akili nzuri kama Lwakatare walishastuka wakakikimbia siku nyingi.CUF kinahusishwa na uislam kwasababu wapemba wengi ni waislam hakuna wakristo kule

Here you are again...nani amekuambia kuwa Pemba hakuna wakristo? Wapo tena ni wazawa wa huko na wenye vizazi kadhaa....
 
Hapa ni siku Mwalimu anapewa kuwa Mkuu wa TANU

112007-10-13_221732.jpg
Hapa ni siku Mwalimu anapewa kuwa Mkuu wa TANU


Kwa picha yako nashawishika Nyerere alikuwa CUF
 
Je hautaki CUF kusimamisha mgombea wao Kigoma kasikazini?

Ni ujinga kwa CUF kushindana na Zitto Kigoma.....Kama ilivyo kwa Mtatiro kuibuka alipokuwa kushindana na Mnyika Ubungo....inaelekea CUF na CHADEMA wameamua kushindana nani anaharibu kuliko mwenziye....
 
Ya Kile chama kilichozindua kampeni siku ya IJUMAA!

What if wakisema kile chama kilichozindua kampeni wakati wa Futari??? Wenzenu CCM kwa kuwa mbele zaidi yenu nyote CUF and CHADEMA wakabadili ratiba mara walipogundua kuwa programe ingewazuia waislam kutopata muda wa kufuturu. That is called SENSITIVITY Vs INSENSITIVENESS.

Hivi Masanilo umesahau kuwa katika mkutano mkuu wa CHADEMA mwaka jana walisahau hata kuandaa futari kwa wanachama wao waliofunga ramadhani wakati huo hadi siku ya pili ilipoandaliwa tambi kavu na ujji wa sembe???

Hili tatazo mnalo wote na litaendelea kuwagharimu lakini zaidi kugharimu maendeleo ya demokrasia katika Tanzania yetu....

omarilyas
 
Nakumbuka kabla ya CUF kwenda Kidongo Chekundu waligombania uwanja wa Jangwani na Chadema hadi ikabidi waitwe kwa Tume ya Uchaguzi kusuluhishwa ndipo CUF walipoamua kurudisha ratiba yao nyuma na kufanyia eneo tofauti.
 
Ni ujinga kwa CUF kushindana na Zitto Kigoma.....Kama ilivyo kwa Mtatiro kuibuka alipokuwa kushindana na Mnyika Ubungo....inaelekea CUF na CHADEMA wameamua kushindana nani anaharibu kuliko mwenziye....

Hata mimi nashindwa kuelewa kulikoni hapa?
 
hao wanaume waliokaa katikati ya wakinamama ndio walewale wasiojua somo.
 
Ni ujinga kwa CUF kushindana na Zitto Kigoma.....Kama ilivyo kwa Mtatiro kuibuka alipokuwa kushindana na Mnyika Ubungo....inaelekea CUF na CHADEMA wameamua kushindana nani anaharibu kuliko mwenziye....

Tatizo mnasahau historia,nyinyi mnaangalia pale ambapo chadema tu wanapoekewa upinzani,hamuangalii chanzo chake nini, halafu hata mkiambiwa ukweli hamkubali,kwa sababu mtu ukipenda hata kama ni chongo utasema kengeza,lkn ingekuwa mnakubali kasoro zenu basi nina hakika upinzani ungekuwa una nguvu sana.. Nyinyi mumesahau mlivowafanyia Cuf kwa mara ya kwanza,ndipo ulipoanza uhusiano kuvurigika,mnakumbuka Pale mliposema hadharani kuwa Upepo sasa umebadilika, halafu mkenda kuwafanyia fitna TLP mpaka viongozi wao wakaja juu kuwalaani chadema,na wakatamka hadharani kuwa chadema kazi yake ni kuua upinzani,then mumesa mpaka NCCR waliwabwatukia viongozi wa chadema,mumesahau mpaka hayati chacha wangwe,mlitaka kumfanyia fitna akose jimbo, halafu angalia Hivi sasa mbeya wapinzani wote mpaka Cuf wameshirikiana kuwa kitu kimoja na wana umoja wao,isipokuwa chadema tu haimo... yapo mengi sana,na ndio maana baadhi ya wachambuzi wanasema chadema imeletwa kwa ajili ya kuua upinzani.. lkn bado mimi naifanyia utafiti kauli hii
 
Tatizo la wabongo tumejaa unafiki hata kwa kitu kinachojieleza wazi.Kwani ni siri kuwa CUF ni chama cha waislamu?na KUMBUKA KUWA UISLAMU SIO KUJIITA MUHAMAD,ni matendo yako........

Je CHADEMA ni chama cha wakristo????????????? mie kuanzia sasa bora niende kwenye chama cha waislam wenzangu maana naoha hoja humu ndani imekuwa hiki cha waislamu kile cha kikristooo mara kile cha wachagga sasa mawili na nadhani kubwa kuliko najitoa rasmi either nibaki na dimi yangu au nijiunge CCM maana si CUF wala Chadema watakao chukua nchi. Hii nchi ina wenyewe kama hamuamini muulizeni bashe.

If you can't fight them....................................... I am IN now !!!!!!
 
Back
Top Bottom