Kwa nini ccm isiwe na katibu mkuu mwanamke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ccm isiwe na katibu mkuu mwanamke?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mlimbwa1977, Apr 25, 2011.

 1. m

  mlimbwa1977 Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa uteuzi wa mgombea kiti cha uspika ndani ya CCM mbiu ilikuwa ni wakati mwafaka kwa mwanamke kushika moja ya mihimili ya dola,ndipo tuliposhuhudia Ndugu Samwel Sita akienguliwa.

  Ukiangalia safu ya uongozi mkuu wa chama hiki ukianzia mwenyekiti,m/mwenyekiti,Katibu mkuu,na wasaidizi wake wote ni wanaume.Je mbiu iliyokuwa ikiimbwa ya kuwapa wanawake madaraka makubwa ilikuwa hadaa kwa watanzania au ilikuwa ni chuki binafsi dhidi ya spika sita?

  Kwa hakika sifurahii kabisa sera ya kupeana madaraka kama chakula,eti wabunge viti maalum!! mfumo huu unawadumaza wanawake na kujiona wao ni watu wa kupewa tu bila kuvuja jasho.Kadri watakavyojitokeza kwa wingi majimboni jamii itawakubali na hatimaye kuongezeka bungeni wakiwa na ajenda mahsusi zinazowapeleka kwa lengo la kuwakilisha jamii wanakotoka badala ya sasa.

  Naomba tuchangie kwa masuala yote haya mawili.karibuni.ELEWA KADRI UNAVYOTOA MAWAZO YAKO CHANYA YANAWEZA KUSAIDIA KUIJENGA INCHI YETU.
   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  itaongeza nini?na kwanini umefikiria hivyo?
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  CCM ni mhimili wa ngapi wa dola?
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Kama ccm wanataka kuweka mwanamke nafasi hiyo wasisite kumpa Sophiiiiiiiiii maana nae ana pumba sana kaama kaka yake alietoka!midomo mali yao wote hao akili na fikra hakuna
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mipasho ya bungeni haijakuchosha?

  Wanajiandaa kwa vita ya 2015....na wakati huo ni vita....na kina mama wetu wa TZ bado hawajaonesha kama wanaweza kuchuna uso na kudanganya bila kusikia aibu katika medani ya siasa.
   
 6. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sichangii plz!!!!!!!
   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Ndg c umesema atapewa moja ya mhimili wa dola,sasa c kashapewa Bunge! ccm sio mhimili wa dola ni chama tawala.
   
 8. m

  mlimbwa1977 Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maana yangu ni kwamba kama lengo ni kuwapa wanawake nafasi za juu katika uongozi,CCM kama chama kilichoonyesha nia hiyo kwa nafasi ya uspika nia hiyo ingeendelea hata ndani ya chama.
   
 9. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  dah maamuz ya mwanamke ndan ya chama italeta pumba kibao kama bungen
   
Loading...