Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
WanaJF,
Sasa tuache lawama, ushabiki, matusi, shutuma, umbea, uongo, uzandiki, ukada, udini, ukabila, uonevu na uchochezi. Tuache yote na tujenge nchi yetu. Kama ni lawama, matusi, shutuma, udhaifu, mapungufu nk tumeshayataja! Sasa tuseme tunaenda wapi.
Kwa niaba ya Raisi nachukua maamuzi yafuatayo;
1.Najiuzulu wadhifa wangu wa u-Raisi, ukuu wa majeshi na uenyekiti wa chama!
2.WanaJF waunde serikali kutoka miongoni mwao wanayoiona ina uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi. Mawaziri hao watoe mipango kazi yao ya nini kifanyike na kifanyike vipi ili kuokoa taifa.
Mpaka sasa najua matatizo ambayo WanaJF wanayaona na kuyasema sana dhidi ya Serikali yangu, Ufisadi, Rushwa, Elimu, Ajira, Afya, Matumizi mabaya ya ofisi, Umeme, Miundombinu, Mfumuko wa bei, Ujambazi, Unyanyasaji wa kijinsia, Mauaji ya Albino, Mauaji ya Wazee, Malipo ya Wazee wa East Africa, Malipo ya Dowans, Migomo, Matatizo ya Walimu, Madaktari na Wafanyakazi wengine nk! Kwa kweli nakubali ni mengi!
Ni matumaini yangu viongozi wazuri watapatikana kwa mfano, Mzee Mwanakijiji, Waberoya, Mohamed Shossi, Michelle, Birigita, Denyo, Rev Masanilo, Voiceof Reason na wengineo wengi! Kila anayeonekana anafaa atoe mapendekezo ya kina kuhusu wizara yake!
Kelele za kupanda bei ya nishati zibadilike kuwa mapendekezo kuhusu nini kifanyike! Mikataba mibovu yatolewe mapendekezo mikataba hiyo ifanyweje!
WanaJF, forum yenu iwe chimbuko la suluhisho na sio mfereji wa lawama. Sio kwamba msilaumu au msifichue ufisadi bali kama viongozi sasa mtoe solutions kulingana na hali halisi.
Shutuma na lawama zenu zimenisababisha niwarudie niwaombe mnisaidie kuongoza kwani mnaonekana mnao uwezo mkubwa. Nadhani hilo mtaliweza. Semeni bila kuficha nini kifanyike kutatua matatizo hayo mnayoyapigia kelele kila kukicha. Imefika mahali kelele za mlango zinamzuia mwenye nyumba kulala! Sipati usingizi!