Wanajf wa CHADEMA, juzi niliona waraka wa katibu mkuu wa BAVICHA kamanda, Deogratias Munishi unaoelekeza muundo mpya wa CHASO ngazi ya mkoa . Huu waraka unaelekeza kuwa CHASO mkoa utaongozwa na viongozi watatu ambao ni:
(a) Mratibu wa CHASO Mkoa
(b) Mratibu Msaidizi wa CHASO Mkoa
(C) Mratibu wa uhamasishaji wa CHASO Mkoa.
Ikumbukwe kuwa kuanzia mwaka jana WanaCHASO walipewa maagizo ya kuendelea kutumia rasimu ya katiba ya CHASO ambayo bado inafanyiwa kazi ambapo watatumia muda huo kuangalia kama katiba hiyo inatakidhi haja. Katika rasimu ya katiba ya CHASO ngazi ya Mkoa inaongozwa na viongozi watano kitu ambacho mi naona ni sahihi kutokana na sababu nitakazotaja hapa chini. Nafasi zinazopendekezwa kwenye hiyo rasimu ngazi ya mkoa ni:
(a) Mwenyekiti
(b) Katibu
(c) Katibu Msaidizi
(d) Katibu Mwenezi
(e) Mweka Hazina
Binafsi sikubaliani na pendekezo kwenye huu waraka bali nakubaliana na pendekezo la rasimu ya katiba ya CHASO kwa sababu zifuatazo:
(1) CHASO Mkoa inajumuisha vyuo vingi ambavyo kimsingi Almanac zao hutofautiana kwa mfano, kwa mkoa wa Morogoro Almanac ya tawi la chuo kikuu Mzumbe ni tofauti na vyuo vingine hivyo kama viongozi wa mkoa wapo wachache uendeshaji wa shughuli za mkoa utakuwa mgumu kwani kuna uwezekano mkubwa Viongozi wote wakawa likizo au wakawa nje ya Mkoa kwa shughuli za masomo kama field na n.k
(2) Kwakuwa, vyuo ndani ya Mikoa viko mbalimbali na geographical conditions ni tofauti hivyo ni vyema kuwa na kundi kubwa kidogo la viongozi ili wasaidiane katika utendaji wa shughuli zao ikizingatiwa kwamba tofauti na shughuli za CHASO, wanamajukumu ya kusoma ambayo nayo ni muhimu kwa maslai ya taifa, chama na wao wenyewe.
(3) Kwakuwa, kuwa kiongozi wa CHASO wakati mwingine ni kutangaza vita na uongozi wa chuo hivyo wakati wowote chochote kinaweza kutokea kama kufukuzwa chuo hivyo tukiwa na viongozi wachache ngazi ya mkoa, kama kiongozi akifukuzwa kuna hatari ya kubaki bila kiongozi wa mkoa au akabakia kiongozi mmoja.
(4) Kwa mara nyingi utakuta vyuo ndani ya mkoa vinatofautiana katika muda wa kufunga na kufungua vyuo, hivyo viongozi wakiwa wengi kidogo itasaidia kwani wengine wakiwa likizo au field, waliobaki wanaendeleza mapambano na shughuli zingine.
(5) Kwakuwa maamuzi ya Mkoa yanahitaji busara, ni vyema kuwa na watu wengi kidogo watakaounganisha mawazo pamoja na kupata maamuzi sahihi.
(6) Kama ngazi ya mkoa watabuni miradi yao hawatakuwa na Mtunza Hazina kama tutakuwa na viongozi watatu kwa mujibu wa waraka toka makao makuu BAVICHA.
(7) Ile rasimu ya katiba ina maelezo ya ziada kwa viongozi kama vile kufanya mikutano, vikao na majukumu ya kila kiongozi tofauti na waraka huu.
Hizo ndio sababu zinazonifanya nipendekeze viongozi watano badala ya watatu. Nilikuwa na mpango wa kuandika barua kwenda makao makuu BAVICHA kuelezea haya mawazo yangu lakini kwa kuwa mimi bado mchanga katika siasa na taratibu za chama, nikaona ni vyema nilete hili wazo humu jf ili mnishauri juu ya mawazo hayo na kama kufanya hivyo ni kuhoji mamlaka ya juu au la. Vilevile mnishauri kama kufanya hivyo sitakiuka kanuni na taratibu za chama. Nawasilisha hoja.
NB: Ni kwa ajili ya wanachama wa CHADEMA na wapenda mabadiliko tu, tafadhali.